Tuzo za Mawasiliano
Tuzo ya Mawasiliano inaonyesha maendeleo yako kama Mzungumzaji wa Mbele ya Hadhira.
Mzungumzaji Bora
Baada ya kumaliza Njia ya Msingi ya Mawasiliano, unapewa tuzo ya Cheti cha Mzungumzaji Bora na Beji ya Kidijitali.
Mzungumzaji Hodari
Baada ya kumaliza kila Njia ya Juu ambayo umechagua, unapewa pia tuzo ya Cheti cha Mzungumzaji Hodari na Beji ya Kidijitali kwa njia hiyo maalum. Kwa mfano, kama umemaliza njia ya Hotuba za Vichekesho/Ucheshi, utapewa tuzo ya cheti cha "Mzungumzaji Hodari wa Vichekesho".
Mwenye Mawasiliano Hodari
Baada ya kumaliza Njia za Juu zozote nne (tofauti) ambazo umechagua na Njia ya Umakinifu, utapewa tuzo ya Mwenye Mawasiliano Hodari, ambayo ni tuzo ya juu inayohusu mawasiliano ambayo Agora Speakers inatoa.
Beji za Kidijitali zinafuata viwango vya Open Badges (openbadges.org ), ambavyo tayari vinatumiwa na maelfu ya makampuni. Open Badges zinaweza zikawekwa kwenye kurasa yako ya kitaaluma (kwa mfano., LinkedIn, Xing, na mitandao mingine ya kijamii), wasifu wa kitaaluma (CV), kadi za biashara, au sehemu nyingine za kidijitali. Picha ya beji ina metadata ambayo inatoa taarifa zaidi kuhusu beji na inaweza kuthibitishwa kwa kujitegemea. Kwa mfano, mwajiri anaweza kubonyeza kwenye beji na kupata taarifa zaidi kuhusu inamaanisha nini na kuangalia ni lini na kwa namna gani mtu anayeionyesha ameipata.
Vyeti vyote vina namba ya kipekee ya uthibitisho (uhakiki) ambayo mtu yoyote anaweza kutumia kuhakiki uhalisi wa cheti.
Kwa hiari, unaweza kuagiza vyeti vilivyochapishwa kutumwa kwa sanduku la posta kama unahitaji vyeti vyako kwa muudo wa karatasi. Tafadhali tambua hii ni huduma ya kulipiwa, na inategemea na wapi ulipo, inaweza kuchukua mpaka mwezi mzima kwa cheti kilichochapishwa kufika.
Jinsi ya kupata cheti chako
Pale utakapomaliza mradi wa mwisho wa njia, wasiliana na VPE au Rais wa klabu yako ili waweze kuomba cheti kwa ajili yako.
Vyeti vinatolewa na Balozi wa klabu kulingana na maombi kutoka kwa VPE au Rais wa klabu. Kama hamna Balozi wa nchi, VPE au Rais wa klabu anatakiwa kutuma ujumbe kwenda [email protected] akitoa maelezo ya kina ya mwanachama na kila mradi: kichwa cha cheti, tarehe, na wapi kinapelekwa.
Tuzo za Uongozi
Kiongozi wa Klabu
Tuzo ya Kiongozi wa Klabu inawakilisha hatua za kwanza za uongozi, na hususan kwenye aina ya uongozi ambao tunahamasisha: uongozi wa utumishi na kuongoza kwa mfano: viongozi wanaohamasisha wengine kwa matendo yao na sio maneno yao. Mahitaji yanaelekezwa ili kuhakikisha kuwa unaboresha ujuzi wote wa msingi ambao viongozi wanao, haswa kwenye maeneo ya ari, ustahimilivu, kusikiliza kwa umakini, uwezo wa kutoa maoni ya kujenga na hisia, na kwa wakati huo huo kutoa msaada wa majukumu muhimu ndani ya klabu.
Ili kupata tuzo ya Kiongozi wa Klabu, unahitaji:
Kiongozi Bora
Tuzo ya Kiongozi Bora inawakilisha hatua za kwanza za uongozi wa nje ya klabu. Inajenga kwenye ujuzi ambao umejifunza kama Kiongozi wa Klabu na kupanua uwezo wako wa kufikia kwa usahihi na kuwasiliana kwa ushawishi dira yako na kutekeleza dira hiyo kwa kuongoza miradi midogo kwenye dunia ya kweli.
Ili kupata tuzo ya Kiongozi Bora, unahitaji:
- Kupata tuzo ya Kiongozi wa Klabu.
- Kumaliza Njia ya Msingi ya Kielimu.
- Kumaliza Njia za Juu za Umakinifu na Uongozi.
Kiongozi Hodari
Tuzo ya Kiongozi Hodari ni hatua ya kati kwenye safari yako ya uongozi. Mahitaji yameundwa kuhakikisha kuwa wewe ni mtu ambaye una mawasiliano mazuri na unajua kutumia njia za juu za ushawishi na kuhamisha watu na ni mtu mwenye ujuzi uliyepitia/umeshawahi kuunda na kuandaa miradi kwa mafanikio na kuwasilisha matokeo.
Ili kupata beji ya Kiongozi Hodari, unahitaji:
- Kupata beji ya Kiongozi Bora
- Kutumikia mwenyewe kama ofisa wa klabu kwa japo miezi 6. "Mwenyewe" inamaanisha kuwa jukumu halikufanywa na watu wengine kwa pamoja. Kwa mfano, kama ulikuwa VP wa Elimu, lakini kulikuwa na VPE wengine wawili kwenye klabu yako, hii haustahili.
- Kupata beji ya Mweneza Mawasiliano Hodari kwa kumaliza kwa nyongeza za Njia za Juu zifuatazo:
- Kuadithia Hadithi
- Hotuba za Ushawishi
- Usimamizi wa Mradi
- Ujuzi wa Kibinafsi
Kama tayari una beji ya Kiongozi Hodari na unatafuta nyingine ya pili (au inayofuata), basi beji ya pili ya Mwenye Mawasiliano Hodari, unaweza kuchagua kati ya Njia za Juu nne zozote ambazo unataka.
Mbeba Mwenge wa Agora
Tuzo ya Mbeba Mwenge wa Agora ni tuzo ya juu ya Uongozi ambayo Shirika la Agora inatoa. Haihakiki tu ujuzi wako wa uongozi lakini pia kuwa umefuata na umetumia kanuni na dira za Agora za kusaidia watu wa duniani kote.
Ili kupata beji hii ya mwisho ya Agora, unahitaji:
- Kupata beji ya Kiongozi Hodari
- Kuwa mwanzilishi wa klabu ya Agora ya uso kwa uso ambayo inafanya kazi wakati wa muda wa tuzo ya beji (Inafanya kazi inamaanisha kuwa klabu inakutana mara kwa mara na ina kiwango cha chini cha wanachama na inafuata miongozo ya Agora). Klabu inatakiwa kuwa japo na miezi 6. Hauhitaji kuwa ofisa ndani ya klabu hiyo.
- Moja kati ya:
Kuongoza kuonekana kwa Agora kwenye vyombo vya habari ndani ya nchi yako. Kuonekana huko lazima kuelezee sisi ni nani, kanuni zenu na dira, na aidha kuelekeza watu kwenye tovuti, wiki, au barua pepe. Mwonekano unaweza kuwa kwa muundo wowote - unapohojiwa, kwenye makala iliyochapishwa, muhtasari kwenye mradi uliofanya, nk. Chombo cha habari ambapo hii inatokea lazima kiwe na mzunguko au kuwa na hadhira ya japo watu 5,000.
AU
Kuongoza Mradi wa Kijamii ambao una umuhimu wa kutosha wa kuripotiwa au kutajwa kwenye vyombo vya habari ya eneo lako (au nchini). Ripoti inahitaji kutaja mradi huo, nini umefanikiwa na kutaja Shirika la Agora Speakers International, jukumu letu, na ni nini tunafanya. Unahitaji kuhakikisha kuwa ni wazi kuwa huu ni mradi wako kama kiongozi, sio mradi wa Shirika. (Sio tu kwasababu ya kutambuliwa kuwa mradi ni wa kwako, lakini pia kuhakikisha kuwa kanuni ya Kutokuwamo haikiukwei).
Chombo cha habari ambapo hii inatokea lazima kiwa na mzunguko au kuwa na hadhira ya japo watu 5,000.
Tuzo Nyingi
Unaweza kupata tuzo mara nyingi kwa kumaliza mahitaji yote ya tuzo hiyo. Kwa mfano, unaweza kupata tuzo ya Mzungumzaji Bora mara mbili kama umemaliza Njia ya Kimsingi ya Kielimu mara mbili.
Tuzo za Mafanikio
Kwa kuongezea kwenye tuzo za kumaliza njia za kielimu, ndani ya Agora, unaweza kupata Tuzo za Mafanikio kwa ajili ya matukio ya kihistoria maalum. Kuna vipengele vinne vya tuzo:
- Tuzo za Uendeshaji - Inatolewa kwa matukio au utendaji wa kipekee kwenye uendeshaji wa klabu, kama vile kuendesha klabu kwa mwendelezo wa mwaka mmoja (1).
- Tuz ya Jamii - Inatolewa kwa mafanikio yanayohusiana na kukua na kuimarika kwa jamii ya Agora, kama vile kuanzisha klabu mpya au kuwa mwenyeji wa Kongamano.
- Tuzo ya Kielimu - Inatolewa kwa kufanikiwa matukio maalum ya kielimu, kama vile kumaliza vyeo vya kielimu vya hapo juu.
- Tuzo za Kijamii - Inatolewa kwa matendo ambayo yana matokeo chanya kwenye jamii yako, kama vile ufikivu wa vyombo vya habari au kumaliza kwa mafanikio mradi wa kiajmii.