Muhtasari kwa Ujumla

Mpango wetu wa Kielimu umeundwa na wazungumzaji wenye uzoefu na watu wenye uzoefu wa zaidi ya miaka 20 kwenye elimu ya watu wazima. Unategemea utafiti wa kisayansi imara, uliotathminiwa na watu wa rika moja kuhusu nini kinafanya kazi na nini hakifanyi kazi kwenye suala la uzungumzaji wa mbele ya hadhira, ushawishi, kujiamini, haiba, uthibiti wa wasiwasi, motisha, na uongozi.

Ina mashina makuu mawili: Ujuzi wa Mawasiliano na Uzungumzaji wa mbele ya Hadhira na inaenda sambamba na Ujuzi wa Uongozi. Jinsi unavyoendelea kwenye mpango, utapata vyeti vya utambuzi tofauti.

 

 

Njia ya Uzungumzaji wa Mbele ya Hadhira

Njia ya Uzungumzaji wa Mbele ya Hadhira inajumuisha Njia ya Msingi (moja) ambayo ni lazima na Njia za Juu ambazo nyingi ni za hiari. Inakutoa kwa upole kutoka mwanzo wa unyenyekevu kwenda miradi migumu zaidi na yenye changamoto, ambapo utazungumza kwanza mbele ya wanachama wenzako wa klabu. Kutoka hapo, utaendelea kupanua mabawa yako nje ya kiota na utazungumza mbele ya hadhira kubwa zaidi na pana.

Ndani ya kila njia, kuna miradi tofauti. Kila mradi una nia na malengo maalum ya kufundisha na umeundwa kukusaidia kupata na kufanyia mazoezi ujuzi maalum - uzungumzaji wa mbele ya hadhira na uongozi. Miradi mingi ya Njia ya Msingi ya Kielimu ina sehemu mbili: mmoja ambao unakuhitaji ufanye uchambuzi wa hotuba na mwingine ambao unakuhitaji uwasilishe hotuba ukitumia seti ya mbinu maalum. Sehemu hizi zinatakiwa kufanywa kwenye mikutano tofauti.

 

Nyaraka za kila mradi zinapatikana mtandaoni.

Miradi yote inafuata kiolezo sawa, ikielezea malengo, muda, kitu gani cha kutumiwa na kutotumiwa, jinsi ya kutathmini mradi, vidokezo, na mapendekezo, nk.

Unaendelea kwa mwendo wako mwenyewe, na kuendelea juu pale tu utakapoona upo tayari. Unaweza kurudia miradi au kurudi kufanya miradi ya nyuma. Hamna mwendo wa lazima, na hamna muda uliowekwa kwa ajili ya kumaliza awamu au mradi wowote, japokuwa unatakiwa kujaribu kumaliza Njia ya Msingi wa Kielimu ndani ya mwaka mmoja.

Pale utakapomaliza njia ya msingi ya kielimu, unafungua ufikivu wa njia za juu nyingi maalum ambazo zinafundisha uzungumzaji wa mbele ya hadhira kwenye maudhui au mazingira maalum. Unaweza kujifunza kuwa muhadithia hadithi, mwasilishaji wa kibiashara, mwalimu, au chaguo nyingine nyingi.

Tunaamini kuwa kila mzungumzaji ni wa kipekee, kwahiyo Mpango wa Kielimu umeundwa pia kukusaidia kugundua mtindo wako mwenyewe, badala ya kukulazimisha ufuate mbinu zisizo halisi ambazo matokeo yake hadhira watakuona kama haupo halisi - au mbaya zaidi - sio mwaminifu.

 

Muundo

Mpango wa Njia ya Kielimu ina sehemu kuu mbili

Njia ya Msingi ya Kielimu, ambayo ina sehemu tatu:

  • "Miradi ya Kwanza" - Seti ya miradi ya kwanza ambayo imeundwa kukusaidia kuchukua hatua za kwanza ndani ya dunia ya uzungumzaji wa mbele ya hadhira. Isitoshe, utapoteza uwoga wako wa kuwa mbele ya hadhira
     
  • "Misingi ya Uzungumzaji- Seti ya miradi ambayo itakutambulisha kwa mbinu za msingi za uzungumzaji wa mbele ya hadhira, inayotumiwa kwenye kila aina ya hotuba.
     
  • "Mbinu za Uzungumzaji- Miradi inakuwa migumu zaidi kwenye sehemu hii. Utatumia mbinu za juu zaidi kama vile visa vya kusisimua, hisia, ucheshi, nk., ambayo kwa kiwango kikubwa ina matokeo kwa baadhi ya aina za hotuba.

Njia za Juu za Kielimu - Utakapomaliza Njia ya Msingi, "utafungua" njia za juu za kielimu. Kila njia ina miradi mingi ambayo inafundisha mbinu maalum za uzungumzaji, maudhui, au mazingiria - kama vile maudhui ya uzungumzaji wa kibiashara, kuadithia hadithi, hotuba za kielimu, na nyingine nyingi.

Maendeleo kwenye njia ya juu yanaweza kusimamishwa na kurejewa katika muda wowote. Hapa utakuta baadhi ya miradi mingi ya juu lakini pia miradi yenye kuridhisha zaidi. Utazungumza mbele ya mashirika mengine, kushiriki kwenye kampeni za kweli za uongozi, na kufanya kazi nyingi za nje ya klabu ya nyumbani, kwenye dunia ya kweli kwa hivyo kwenye mazingira ambayo hayajathibitiwa. Njia za Juu za Kielimu zimeundwa kukusaidia "kupaa kwa njia yako mwenyewe" kutoka kwenye kiota.

 

Njia ya Uongozi

Njia ya Uongozi inafuata mbinu sawa za kujifunza kwa matendo kama njia ya mawasiliano kwa kukutoa kwenye mwanzo wa unyenyekevu, kama vile kuongoza shughuli au zoezi maalum ndani ya klabu yako na kukupelekea kwenye malengo makubwa zaidi ambayo yana matokeo kwa jamii yako kwa ujumla.

Utagundua kuwa Njia ya Mawasiliano haihitaji mazoezi yoyote ya uongozi: unaweza kuwa mtaalam na mzungumzaji mwenye mafanikio makubwa (na anayelipwa vizuri) bila kukabiliana na shughuli zozote za uongozi. Lakini, Njia ya Uongozi ni tofauti: viongozi wanahitaji maarifa mapana ya kiufundi na ujuzi na uwezo wa hali ya juu ya uzungumzaji wa mbele ya hadhira.