Balozi wa Agora anakuwa kama kiongozi au mwinjilisti wa shirika wakati wa hatua za mwanzo za Agora kwenye nchi, anawakilisha shirika, kanuni zake, na maadili yetu ya msingi. Wanajumuisha kiinitete cha Bodi ya Wakurugenzi wa baadae.
Vigezo
Kutimiza dhumuni hili, mabalozi wa Agora wanatakiwa kuwa na maadili, uwezo wa kutoa msaada, na wawe na nia ya kuwasaidia watu ndani ya nchi zao kuanza na kuanzisha klabu na Agora na kusaidia shirika kupanuka ndani ya nchi. Kunaweza kuwa na balozi mmoja au mabalozi kadhaa, inategemea na ukumbwa na idadi ya watu kwenye nchi.
Mabalozi wanatakiwa kuwa na vigezo vifuatavyo:
- Wanaendesha Klabu ya Rejea kwenye nchi yao.
- Awe ana uzoefu wa kikamilifu na habari zote kuhusu Agora - dhumuni letu na dhamira, mpango wetu wa kielimu, vipengele vyote vya mkutano, na majukumu na miongozo ya kuunda na kuendesha klabu.
- Wawe wameunda japo klabu moja mpya kwa mwaka ndani ya nchi yao. Hii haimaanishi kuwa wanaiendesha (isipokuwa kama unataka na una muda wa kufanya hivyo) - kusaidia tu kuanzilisha klabu mpya na kuwa mkufunzi ili iweze kustawi kwa uhuru.
- Wanasambaza kwa wengine (picha na video) kuhusu klabu yao.
- Wanaweza kuweka rasmi cheo cha ("Balozi wa Agora Speakers wa nchi") kwenye mitandao yao ya kijamii.
- Wawe na tabia iliyo sawa na maadili na kanuni za Agora Speakers International.
Kutoka kwa mtazamo wa kiutaratibu na kiuendeshaji, Mabalozi wa Agora lazima:
- Awe anaishi kwenye nchi ambayo anawakilisha.
- Awe ana uwezo wa kupata kompyuta na kuunganishwa na intaneti, na wawe wanaweza kushiriki kwenye orodha ya anuwaini ya Mabalozi.
- Awe ana uwezo wa kuwasiliana kwa Kiengereza na awe na ufasaha wa asili kwenye lugha rasmi ya nchi au kanda ambayo unaishi (Kama nchi ina zaidi ya lugha moja rasmi, basi ufasaha wa asili kwenye lugha moja inatosha).
- Awe anaweza kushiriki mara kwa mara kwenye mikutano ya kila mwezi ya Kibalozi.
Tafadhali tambua kuwa cheo cha ubalozi sio utaratibu otomatiki na unafanywa kwa uhuru na Agora Speakers International Foundation. Hata kama una vigezo vyote vya hapo juu, cheo kinaweza kukataliwa kwasababu zingine. Kinyume pia inawezekana: hata kama hauna baadhi ya vigezo vya hapo juu, unaweza ukapatiwa cheo cha ubalozi kama umefanya michango ya kipekee au umeongeza umeongeza thamani kipekee kwenye Shirika.
Pia, tafadhali tambua kuwa vigezo vya kuwa Balozi vinabadilika na muda na inategemeana sana na maendeleo ya Agora ndani ya nchi.
Kuendesha Klabu ya Rejea
Jukumu la muhimu sana la balozi ni kuendesha "klabu ya rejea" au "kiolezo" - klabu ya Agora ambayo watu wengine ndani ya nchi wanatumia kama rejea na wanaweza kuona mifano ya karibu na iliyo hai ya namna gani Agora inafanya kazi duniani kote. Kwahiyo, klabu za rejea zinahitaji kufahamu mapendekezo ya Muundo wa Mkutano na vigezo vya msingi vya majukumu ndani ya mkutano. Klabu ya rejea ina vigezo vikali zaidi kuliko klabu ya kawaida ya umma kwasababu, baada ya yote, ni zaidi ya klabu ya kawaida - inawakilisha jinsi Agora inafanya kazi. Angalia orodha ya kulinganisha hii kwa ajili ya tofauti maalum.
Hii inasaidiwa kwa kurekodi baadhi ya mikutano, hotuba, na majukumu na kuzisambaza kwa wengine kwenye jamii ya Agora na haswa vyombo vya habari, blogu, na machapisho mingine ndani ya nchi yao. Mabalozi wa Agora wanatakiwa kufuata maadili, masharti, na kanuni za msingi za shirika; ndio maana ni muhimu sana klabu ifanye shughuli za klabu kwa ufanisi wa hali ya juu iwezekanavyo.
Klabu ya rejea lazima iwe ya umma na inakaribisha wageni - kutoka umma kwa ujumla na kutoka Agora na mashirika mengine na inaweka vizuizi na vigezo vya kuhudhuria vichache viwezavyo. Lazima wakutane japo mara mbili kwa mwezi.
Ifuatayo, kwa mfano, haipendekezwi kwa klabu za rejea:
- Mahali pa mkutano kwenye sehemu za mbali au sehemu ambazo hazifikiwi kirahisi kwa usafiri wa umma
- Mahali pa mkutano au ukumbi ambayo ina vizuizi vikali vya usalama
- Kuhitaji wageni kujiandikisha kwenye makundi au orodha ya watu wanaopelekewa matangazo kabla ya kuhudhuriwa
- Muundo wa mkutano ambao upo tofauti sana na muundo wa mkutano ambao unapendekezwa
Klabu za Rejea zinatakiwa kuwa na gharama ya chini iwezavyo ya ada na isitoze ada yoyote kwa wageni ambao wanahudhuria.
Mitandao ya Kijamii
Agora Speakers ina kurasa nyingi za mitandao ya kijamii, ikiwemo makundi ya Facebook, majukwaa, nk. Balozi ana jukumu la kuendesha kurasa zote za mitandao ya kijamii ya Agora kwa ajili ya nchi na ana mamlaka nayo. Kurasa hizi lazima zinatakiwa kuendeshwa kirahisi iwezekenavyo, ambayo inamaanisha kukubali maombi ya wanachama haraka iwezekanavyo, kujibu maswali, kuondoa maudhui ambayo hayapendezi, nk.
Hakuna haja ya Mabalozi kuchapisha mara kwa mara au kuwa na aina yoyote ya blogu au jarida. Lakini, kama wana muda na wanataka kufanya hivyo, basi hiyo inakaribishwa. Hata hivyo, tunapenda kuwaomba Mabalozi wa Agora waweke mara kwa mara picha au video wakionyesha jinsi klabu zao zinafanya kazi.
Bila kujali lugha rasmi zinazotumiwa ndani ya Agora, Mabalozi wanahimizwa kutumia kwenye mitandao yote ya kijamii lugha ya nchi ambayo wapo ili waweze kuongeza ufikivu wa ushirika.
Mazoezi mengine
Mabalozi wa Agora pia:
- Kusimamia uwepo wa Agora kwenye mitandao ya kijamii ndani ya nchi (kama vile makundi ya Facebook, Twitter, nk.)
- Wanafanya kama pointi au kituo cha kuonyesha kama shirika linakuwa.
- Kutoa zawadi kwa wanachama na klabu ambazo zimefanya vizuri zaidi kwenye maeneo tofauti.
- Kupendekeza watu ambao wanaweza kutafutwa ili shirika liweze kukua zaidi, ndani ya nchi yao au kwingine.
- Kutoa ufahamu wa masuala ya eneo hilo ambayo shirika litakuwa halijui, kama vile masuala ya kidini au kisiasa, mahitaji ya kutafsiri, miradi ya maendeleo yaliyopendekezwa, nk.
- Kuwa kituo cha kwanza cha mawasiliano na vyombo vya habari na masuala yanayohusu vyombo vya habari.
- Kutangaza shirika kikamilifu na kuhimiza na kusaidia kwenye uundaji wa klabu mpya.
- Kwa muda wao wenyewe, wanaweza kwenda kwenye mikutano ya uwasilishaji kwenye taasisi ambazo wanaweza kufanya nao kazi.
- Kutoa majibu ya maswali ambayo waanziliishi wanayo.
- Kuandaa, kushiriki, au kupendekeza kampeni za matangazo au njia tofauti za matangazo na fursa za kukuza Agora.
- Kutoa msaada wa mawasiliano na watu ambao wanaweza kujihusisha kwenye miradi au kutoa ushirikiano kwenye mamlaka za serikali.
- Kuandaa, kushiriki, au kupendekeza matukio, Mashindano, na Makongamano ya Agora.
- Kushirikiana na mabalozi wengine kwenye majadiliano ya mawazo, mapendekezo, na mitazamo ya jinsi ya kukuza shirika duniani kote.
- Kuwa kama kituo cha rufaa kwenye masuala ya nidhamu
Kama jukumu la kujitolea, hamna kusafiri au mazoezi mengine "yanayohitajika" zaidi ya kuendesha klabu ya rejea ndani ya nchi, kutangaza Shirika, na kudumisha kanuni zetu.
Utambuzi wa Mabalozi
Mabalozi wa Agora wanatambuliwa kwa njia nyingi, ikiwemo kuwa na uwepo kwenye tovuti na kwenye machapisho ya Agora.
Mabalozi wetu wana kipengele cha maelezo mafupi ya kitaaluma kwenye wiki yetu .
Vizuizi
Tafadhali tambua kwamba kuwa Balozi wa Agora haikupi haki ya kuiwakilisha Shirika la Agora Speakers International kisheria, kufanya majadiliano kwa niaba yake, au kuingia kwenye mikataba ya mapatano.
Pia, jukumu lako kama Balozi haliwezi kutumiwa kutangaza mashirika mingine, biashara, huduma, au bidhaa, au kwa njia yoyote ambayo inaweza kuonyesha kuwa Agora Speakers International imeidhinisha, imesaidia, imeshirikiana au inashirikiana kwa namna yoyote ile na mashirika mengine, biashara, huduma au bidhaa.
Mwisho, mabalozi wana jukumu la kuwa wakufunzi, makocha, na kutoa mwongozo, lakini jukumu la Ubalozi halikupi mamlaka ya klabu nyingine, au uwezo wa kufanya maamuzi kwa niaba ya wanachama wake.
Kuwa balozi wa Agora kunaendana na kuwa na jukumu sawa kwenye shirika jingine, ilimradi unafanya jukumu lako la Ubalozi kwa usahihi, kama ilivyoelezewa hapo. Kama, unatangaza bila kuacha mashirika mengine zaidi ya Agora, basi unatakiwa ufikirie kama kuwa Balozi wa Agora kunakufaa. Tunatarajia kuwa utatangaza Agora angalau kama vile unavyotangaza mashirika mengine.
Mabalozi wa Sasa
Orodha ya sasa ya Mabalozi inaweza kupatikana kwenye kurasa hii - /Jamii+kutoka+Sehemu+Nyingine+Duniani -, na orodha hii ni chanzo cha ukweli kwenye suala hili. Baadhi ya nchi hawana Mabalozi, na hiyo ni sawa: inamaanisha kuwa nchi ina wanachama na klabu, lakini hamna mtu ambaye amejitolea kuwa Balozi.
Agora imekuwa maarufu sana hivi karibuni na baadhi ya watu wameanza kudai wao ni Mabalozi, Wawakilishi, Wakurugenzi, na mengineyo.
Kwa sasa, "nafasi" ambazo zinatambulika ndani ya Agora ni:
- Waanzilishi wa Klabu - katika kiwango cha klabu.
- Maofisa wa Klabu - katika kiwango cha klabu.
- Mabalozi wa Nchi - katika kiwango cha nchi.
Hamna "wakurugenzi wa kanda", "mabalozi wa mabara," au majukumu sawa yakuundwa.
Mabalozi wa Heshima
Mabalozi wa zamani ambao walitoa huduma ya kipekee kwa Shirika wanabaki na Ubalozi wa Heshima ambao inawaruhusu kubaki na cheo lakini wanakuwa hawana majukumu ya kuendesha klabu au kuunda klabu au kusimamia mitandao ya kijamii.