Kwa kawaida, unaweza ukaipa klabu yako jina lolote unalotaka, isipokuwa hivi:

  • Jina lazima liandikwe kutumia seti ya herufi za Latin-1 (ISO 8859-1)
     
  • Jina lazima liwe la kipekee ndani ya eneo lako. Kama jina linataja eneo la kijiografia (kwa mfano mji wako), lazima liwe la kipekee ndani ya nchi yako. Kwa mfano, kama klabu yenu inakutana mjini Paris, hauwezi kuipa klabu yako jina la "Wazungumzaji wa Madrid".
     
  • Jina la klabu za Manufaa ya Umma na Shirika lazima yajumuishe au kutaja shirika ambalo linahusiana nalo.
    • Wazungumzaji wa Juu wa IBM Paris
    • Shule 114 Agora Speakers
    • Wazungumzaji wa Juu wa Paris
       
  • Jina halitakiwi kuwa na maneno yenye hakimiliki, isipokuwa kama ni klabu ya shirika ambayo imeruhusiwa rasmi na kampuni, na kampuni ina hakimilliki ya hilo neno, na mmeruhusiwa na uongozi kulitumia. Kwa mfano, hauwezi kuipa klabu yako jina la "Wazungumzaji wa IBM Washington" isipokuwa kama una ruhusa rasmi kutoka IBM.
  • Jina halitakiwi kuonyesha au kuonekana kwamba ni mwakilishi wa shirika zima au tawi rasmi la Agora Speakers International. Majina yafuatayo, kwa mfano, hayatokubaliwa :
    • Agora Speakers Kuu
    • Makao Makuu ya Agora Speakers
    • Taasisi ya Uongozi ya Agora
    • Agora Speakers wa Kijerumani
    • Agora Speakers International Paris
    • Klabu rasmi ya Agora Paris
  • Kwa sasabu sawa, jina halitakiwi kuweka jina la kijiografia kubwa zaidi ya mji (kwa mfano, "Ufaransa", au "Ulaya", au "Kimataifa"). Lakini, unaweza kutumia jina la mji wa klabu kama hamna klabu nyingine kwenye mji wako ambao wanatumia jina hilo hilo.
    • Agora Speakers Ufaransa
    • Agora Speakers Ulaya
    • Wanafunzi wa Agora Speakers International
    • Advanced Speakers International
    • Advanced Speakers Ufaransa
    • Wasafiri Dunia wa Kimataifa
    • Agora Speakers Paris

 

  • Jina halitakiwi kuna na neno la kuudhi au la chuki kwa makudi mengine ya watu.
  • Jina halitakiwi kuwa na neno la kukashifu na lazima sheria za eneo lao zinazohusu kutoa majina kwa mashirika na makampuni zizingatiwe.
  • Jina halitakiwi kupotosha ni aina za shughuli zinazofanywa ndani ya klabu au zinazoidhiniwa au zinazotambulika. Haswa, haitakiwi kudai kuwa ni shule, chuo kikuu, au taasisi ya aina sawa ya kielimu. Kumbuka, kama klabu ni ya aina hiyo ya taasisi, kujumuisha jina ni sahihi.
    • Shule ya Uongozi
    • Shule ya Uzungumzaji mbele ya Hadhira ya Paris
    • Chuo Kikuu cha Midahalo cha
    • Klabu ya Agora ya Chuo cha Harvard
  • Jina halitakiwi kuwa na tamko la taswira ya kisiasa, kidini, au kiitikadi (hii inaweza kuonyesha kuwa klabu inakubali aina hiyo ya wanachama tu, kitu ambacho kinapinga kanuni ya kutokuwamo). Kwa mfano, majina yafuatayo ya klabu hayaruhusiwi:
    • Klabu ya kumwamini Mungu
    • Klabu ya Agora ya haki za Wafanyakazi
    • Klabu ya Wapinga Mabadiliko ya Tabia nchi
    • Wazungumzaji wa chama cha Republican
    • Wazungumzaji wa Mrengo wa Kushoto
  • Sio lazima requirement kuweka "Agora" kwenye jina la klabu. Majina yafuatayo ni sahihi:
    • Wazungumzaji wa Juu wa Paris
    • Wasafiri Dunia wa Paris
    • Wazungumzaji wa Spring wa Paris
    • Wazungumzaji wa Seine
    • Wahutubu wa Green Hill
    • Wasomi wa Sayansi
  • Kama unataka kutumia Agora kwenye jina la klabu, basi linatakiwa kujumuishwa bila mabadiliko. Hautakiwi kuifanya kuwa wingi au kulibadilisha kwa njia yoyote:
    • Wazungumzaji wa Agora wa Paris
    • Agora Speakers ya Paris
    • Agora ya Paris
    • Agoras Paris
    • Agoritos de Madrid
    • Agoreans United

 

Kama kuna mashaka yoyote, tutumie ujumbe kwenda [email protected]

Tafadhali jua kuwa kuna muda tunaweza kukataa jina la klabu wakati wa kujiandikisha kwa sababu ambazo hazijatajwa hapa, lakini hiyo itakuwa dhidi ya malengo na mtazamo wa ujumla wa Shirika au inaweza isifae kwa njia ambazo hazikuonekana kabla.