Daima Msimamizi wa Mdahalo ndio anayempa nafasi ya kuongea mwanachama wa timu, jaji, au mtu wa kutoka kwenye hadhira kuzungumza. Pale mzungumzaji atakapoanza kuzungumza, anatakiwa kuachia nafasi/jukwaa pale atakapoambiwa na Msimamizi wa Mdahalo or Mtunza Muda.
Wanachama kutoka timu za mdahalo lazima wasimame wakati wanazungumza - bila kujali kama wanawasilisha hotuba iliyoandaliwa, wanatoa POI / POA / nk., au kuuliza swali. Ili kuzuia kupoteza muda, inapendekezwa kuwa wazungumze kutoka nafasi yao walipo kuliko kutembea kwenda kwenye jukwaa kuu.
Kusoma hotuba zilizoandikwa kabla kunatakiwa kuzuiliwa, isipokuwa dondoo za data – takwimu, matukio ya kihistoria, nukuu za watu wengine, nk., au kurejea hoja ambazo zimetolewa na upande wa pili.
Ili kuzuia ubinafsi kwenye mdahalo, wazungumzaji wote wanatakiwa kuwaita watu wa timu kwa nafsi ya mtu wa tatu ("Timu nyingine", "Mzungumzaji kutoka Timu ya 2", "Wapinzani wetu") badala ya misemo kama ("wewe" au "John, hiyo sio kweli"). Kuwa rasmi, hata hivyo, hakuhitajiki.
Pointi za Taarifa zimesambaa vizuri kwenye mitindo mingi ya mdahalo na ni kukatizwa kwa kidogo kwa mzungumzaji na wanachama wa timu nyingine ili kupinga hoja,
POI zinaweza kuombwa na wanachama wa timu nyingine. Ili kufanya hivyo, mwanachama wa timu nyingine ananyoosha mkono. Mzungumzaji ambae POI ilielekezwa anaweza kukubali au kukataa POI ambaye imeombwa. Kwenye suala la kwanza, anaweza kusema kwa urahisi "Ndio?" na kutoa nafasi kwa mpinzani. Kwenye suala la pili, anaweza kusema "Hapana asante", au akaonyesha ishara ya mkono ya kukataa ombi na kuendelea.
POI haiwezi kuwa zaidi ya sekunde 15.
Kwa kawaida, mifumo mingi ya hotuba inafafanua "muda uliolindwa" wa hotuba, ambapo POI hazitakiwi kufanywa. Ukizingatia urefu wa raundi zetu, muda huo unaolindwa utakuwa sekunde 45 za kwanza na za mwisho wa hotuba.
Pointi ya Amri inaweza kuinuliwa na mwanachama yoyote wa timu ambae anaamini kuwa masharti ya mdahalo yamevunjwa, na lazima ifanyike hapo hapo baada ya kugundua ukiukwaji.
Utaratibu wa kufanya Pointi ya Amri ni kama ifuatavyo:
- Mshiriki wa mdahalo ambaye anataka kuleta mbele POO anasimama na kusema, "Pointi Ya Amri."
- Mzungumzaji ananyamaza.
- Mshiriki mwenye POO anamuelezea Msimamizi wa Mdahalo suala lake. Katika kipindi hiki, muda unasimamishwa.
- Baada ya kusikiliza suala hili, Msimamizi wa Mkutano anafanya maamuzi.
Kwa ujumla, Pointi ya Amri:
- Inaweza kumkatiza mzungumzaji.
- Sio za majadiliano
- Haiwezi kubadilishwa au kuzingatiwa tena
- Zinaamuliwa na Msimamizi wa Mkutano, na maamuzi ni ya mwisho.
Pointi za Makubaliano ni kipengele cha ubunifu kwenye midahalo ya Agora ambayo inataka kuelekeza midahalo kwenye makubaliano/kufikia muafaka. Lengo la POA ni kuelezea timu kukubali hoja ambayo imependekezwa na timu tofauti. Kukubali huku hakuwezi kuondolewa baadae. Ili kupata POA, wanachama wote wa timu inayotoa lazima wakubaliane (lazima kuwe na makubaliano).
Ili kuzuia masuala ya "ndio, lakini…" ambayo inaonyesha kutokubaliana kuliko kukubaliana, POA lazima irudie hoja ya timu pinzani kama ilivyoelezewa mwanzoni. Haiwezi kugeuzwa, kupambwa, kufanywa tofauti kidogo, au kwa namna yoyote ile kuelezewea zaidi. Kwa mfano, timu haiwezi kusema, "Tumekubaliana na msimamo wa kuwa kuna kiwango cha wastani cha ulaghai kinatokea kwenye elimu za juu zenye ruzuku, nk….". Aidha tamko au hoja iliyosemwa na timu pinzani inakubaliwa kama ilivyotamkwa, au hakuwezi kuwa na POA.
Utaratibu wa Pointi za Makubaliano ni:
- Wakati wa muda wao wa kuzungumza, timu ambayo inayopendekeza POA inatamka wazi, "Timu yetu inakubaliana na nafasi/hoja ya timu XXXX kuwa : tamko".
- Tamko hilo linatakiwa kurudia vile vile hoja au msimamo ambayo timu nyingine imezungumza.
- Timu lengwa aidha inajibu "Imekubaliwa" (kama tamko ambalo limetajwa kweli linaonyesha msimamo wao) au "Imekataliwa" (kama haionyeshi msimamo wao). Kama ni ya pili, maelezo mafupi yanaweza kuongezwa.
Kuunganisha timu ni sifa ya kipekee ya Midahalo ya Agora Speakers ambayo inahimiza kujaribu kufikia makubaliano.
Katika pointi yoyote ya mdahalo, timu mbili zinaweza kufikia makubaliano na kuungana kuwa timu moja, kutetea mtazamo wao wa makubaliano. Kwenye mfano huu, Timu N na D zinaweza kukubaliana kuungana, kutetea mtazamo mmoja ambao ni "Watu wanatakiwa kulipia elimu yao wenyewe, na kiwango kinatakiwa kuwa ishara kama kiwango chao cha kipato kipo chini ya kiwango fulani":
Pale timu mbili zitakapounganisha msimamo wao na kuwa timu moja, idadi inayofaa ya uanachama wa timu iliyounganishwa lazima wapungue ili kubaki na usawa na sharti kuwa timu zote lazima ziwe na idadi sawa ya wanachama.
Kuunganisha kunahitaji makubaliano ya pamoja ya wanachama wote wa timu mbili na inaendelea kama ifuatavyo:
- Timu inayopendekeza inaamua kutoa ofa ya nafasi ya makubaliano kwa timu nyingine. Wanachama wote wa timu pinzani lazima wakubali maneno ya msimamo wa makubaliano. Pia, timu inayopendekeza lazima iwe imechagua kabla wanachama wa timu ambao wataondoka kama ofa itakubaliwa.
- Wakati wa muda wa kuzungumza wowote wa timu pinzani, mzungumzaji anaanza kwa kuzungumza kwa timu lengwa na kusema kitu kama, "Tungependa kutoa msimamo wa makubaliano ifuatayo kwa timu XXXX : ". Fomula yoyote ambayo imechaguliwa, lazima iwe wazi kuwa haya ni mapendekezo ya kuunganisha msimamo, pendekezo lazima litaamkwa kwa uwazi, na lazima iwe imeelekezwa kwa timu lengwa maalum.
- Baada ya ofa ya kwanza kufanywa, mzungumzaji anaendelea na hotuba yako ya kawaida.
- Pale zamu ya timu inayopendekeza itakapoisha, msimamizi anatoa pumziko la dakika 1 ya mdahalo kwa ajili ya timu lengwa kuamua. Wakati wa mapumziko, timu lengwa inafikiria na kufanya maamuzi, ambayo inaweza kuwa kukubali au kukataa ofa ya msimamo wa makubaliano. Kukubaliwa lazima kuwe kwa pamoja, na lazima iwe wazi kuwa wanachama wa timu kutoka timu inayokubali wataondoka ili kubaki na usawa kwenye timu iliyounganishwa.
- Baada ya mapumziko, bila kujali ni zamu ya nani kuzungumza, msimamizi atazungumza na timu lengwa na kuwauliza kama wanakubali au wanakataa msimamo uliotolewa. Timu lengwa inaweza tu kujibu kwa kukubali au kukataa; hamna majadiliano au hotuba zinazoruhusiwa katika pointi hii.
- Kama timu lengwa itakataa, mdahalo unaendelea kama kawaida, msimamizi akitoa jukwaa kwa timu inayofuata yenye zamu ya kuzungumza.
- Kama timu lengwa itakubali, basi wanachama wa timu waliochaguliwa kabla wanaondoka, na timu moja iliyounganishwa inaendelea. Timu mpya haiwezi kuzungumza kwenye raundi hii, kwasababu inazingatiwa kuwa tayari zamu yao imeshatumika kwenye pointi ya 3.
Kugawanya tena timu zilizounganishwa hairuhusiwi.
Timu zilizounganishwa zinazingatiwa kutoka kwenye pointi ya kuunganishwa kwao kama timu moja, inayofurahia zamu moja ya kuzungumza na kuuliza maswali, pamoja na muda wa kawaida unaotumika na timu yoyote ya kawaida.
Mdahalo unaisha hapo hapo na "Makubaliano" kama hakuna timu nyingine za kuunganisha.
Kama hii ni shindano la mdahalo, timu zote ambazo zimeunganishwa kwenda fainali, na timu ya mwisho itatangazwa "Washindi wenye Makubaliano". Mashindano yanatakiwa kuhimiza aina hii ya matokeo.
Kumbusho kama kuna aina yoyote ya tuzo za kibinafsi ambazo zipo, zote zinatakiwa kupewa kwa wanachama wa mwanzo wa timu zilizounganishwa, bila kujali kama waliondoka kwenye mdahalo wakati wa kuunganisha ili kuzingatia usawa wa timu.
Ni muhimu kwa afya ya mdahalo na mazingira ya klabu kuzuia aina yoyote ya matusi, hoja binafsi, hotuba zisizo na heshima, au kubadilika kwa sauti au kupiga makelele. Hivyo vyote haviruhusiwi na inaweza kusababisha kuondolewa kwa mwanachama wa timu au timu yenyewe. Kumbuka kuwa matusi yanaweza kuwa yasiyo na maneno (kwa mfano, kwa kutumia ishara), na bado yanakatazwa.
Hoja binafasi ni hoja yoyote (au swali, au maoni) inayolenga sifa au vipengele vya mtu kwenye timu ya upinzani au vitu kwenye nyanja ya mdahalo, ikiwemo (lakini sio tu):
- Umri, Jinsia, Mapendekezo ya kijinsia au utambulisho, Utaifa, Asili, Rangi, Dini, Itikadi, Matatizo ya kiafya.
- Historia ya Kielimu au Kitaaluma.
- Mtindo wa kimaisha, jambo unalopendelea, na unachofurahia.
- Machapisho au tamko ambazo zimefanywa nje ya klabu. (Midahalo imejifunika yenyewe, na hoja pekee ambazo zinaweza kupingwa ni zile ambazo zitatokea wakati wa mdahalo wenyewe).
Hoja binafsi ni pia hoja ambazo zinatumika kujumuisha makundi ya watu kutokana na vigezo vya hapo ju, hata kama anayezungumzia hayupo kwenye kundi hilo. Kwa mfano, "Wahispania wote ni wazembe" ni "ad hominem", hata kama hamna mtu kwenye mdahalo anayetoka Uhispania. Lakini, kumbuka, kuwa kutoa ushahidi wa utafiti usiokuwa na lengo la kuhukumu makundi ya watu inakubalika. Kwa mfano, ni sawa kusema "Watu wa Elbonia wanafanya kazi masaa 12.6 kwa wiki, kinyume na masaa 37.4 kwa wiki ya Ufaransa".
Msimamizi wa hotuba lazima atende hapo hapo atakaposikia hoja binafsi. Kama hii haitotokea, mwanachama ambaye hoja binafsi ilielekezwa anaweza kunyoosha mkono nakusema "Ad hominem" ili kumfanya mwezeshaji kulifanyia kazi, na ambapo msimamizi atatakiwa kujibu aidha "Nakataa" au "Nakubali". Kama msimamizi anamini kuwa hoja binafsi imetumika, anatakiwa kufanya moja ya yafuatayo:
- Kuonya timu ambayo inatumia ad hominem kujizuia kutumia hoja sawa baadae.
- Msimamishe mzungumzaji ambaye anazungumza, na wanyime timu husika kuzungumza kwa zamu moja.
- Kumtoa mwanachama na kumuondoa kwenye timu husika.
- Kuitoa timu yenyewe kama wanachama wa timu wanaendelea kutumia hoja binafasi baada ya mmoja ya wanachama wa timu kutolewa kwa sababu hiyo.
- Kuvunja mdahalo wote kama anaona imekuwa mechi ya ad hominem.
Aina nyingine ya tabia zisizo kubwa lakini zisizokubali ni:
- Kukatisha mara kwa mara wazungumzaji na POI na POA za uwongo
- Kujivuta vuta ili "kula" muda wa timu nyingine, haswa kwenye raundi ya kuuliza maswali tena.
- Kutumia muda mwingi uliopitiliza.
- Kuvunja au kutumia vibaya masharti
Ushahidi ni ukweli, picha, video, data, nukuu nk., ambavyo vinasaidia hoja ya mzungumzaji.
Masharti yafuatayo yanatumika kwenye ushahidi:
- Kila kipande cha ushahidi lazima kiwe kimetenganishwa kwa uwazi kutoka maoni ya mzungumzaji mwenyewe na kutoka vipande vingine vya ushahidi.
- Ushahidi wote unatakiwa kutambuliwa, kutoka kwenye vyanzo, na kuhakikiwa kwa kujitegemea. Hii inakataa dhahiri "ushahidi wa kudhahania au hafifu" kwenye matamko sawa na "Utafiti unaonyesha kuwa …". Badala yake, matamko hayo yanatakiwa kuundwa kama "Utafiti uliofanywa unaonyesha kuwa …"
- Ushahidi hauwezi kubadilishwa, kunukuliwa kwa kimakosa, kunukuliwa kwa kiasi kidogo, au kunukuliwa nje ya muktadha. AIna hii ya tabia haikubaliki.
- Ushahidi wote ambao umetumika unatakiwa kuwa kupewa kwa timu nyingine, hadhira, na majaji, ili yoyote aweze kuutumia wakati wa zamu yao. Hii inamaanisha, kwa mfano, kama unatumia chati iliyochapishwa kuonyesha pointi yako, chati iliyochapishwa lazima iwekwe kwenye sehemu ambayo wengine wanaweza kutumia.
- Pale itakapoombwa na timu nyingine au majaji, ushahidi uliotumiwa lazima utolewa kwenye mfumo ulioelezewa na kwa maandishi. Kama ushahidi ni mrefu sana, japo kurasa moja lazima iwepo.
- kila kipande cha ushahidi kinatakiwa kutoa japo taarifa zifuatazo:
- Jina la mwandishi
- Sifa za mwandishi ambazo zinahusu mada iliyopo.
- Taarifa kamili ya chanzo cha bibliografia, ikiwemo tarehe na namba ya kurasa
- Kwenye suala la vyanzo vya mtandaoni, URL yote na tarehe ya kufikia
- Wanachama wa timu hawawezi kupata ukocha wa nje wakati wa kipindi cha mdahalo.
- Hadhira kukatisha wazungumzaji au wanachama wa timu nyingine hairuhusiwi na inatakiwa kushughulikiwa na Msimamizi wa Mdahalo. Kushangilia hakuruhusiwi.