Karibu kama mwanachama mpya wa Agora Speakers International. Klabu ambayo umejiunga ni moja kati ya klabu nyingi za Agora duniani kote.
Sasa nini kinafuata?
Kama mwanachama mpya, unaweza kuhisi vitu ni vingi sana mwanzoni, na unaweza pia kufikiri kuwa wanachama wote ambao tayari wapo ni wazungumzaji wa hali ya juu. Ukweli ni kwamba mwezi mmoja au miwili kabla, walikuwa kama wewe ulipo sasa.
Jinsi ya kuanza
Kwanza kabisa, soma sura ya utambulisho yote, na pia kuhusu mpango wa kielimu wetu, ili uweze kuelewa ni jinsi gani klabu inafanya kazi.
Kwa uhalisia, unatakiwa kujaribu kushiriki kwenye mikutano kwa kuchukua majukumu. Haijalishi kama ndio kwanza unajaribu - daima kuna mara ya kwanza kwa kila jukumu.
Angalia kwenye ajenda ambayo imepostiwa kwa ajili ya mkutano ujao (kama ipo), angalia majukumu ambayo yapo, na jitolee kuyafanya. Hata kama hauna jukumu, ni muhimu kuhudhuria mikutano ya klabu - japo mara mbili kwa mwezi.
Orodha kamili ya majukumu inapatikana hapa. Tunapendekeza uanze na majukumu haya marahisi kama vile Mtunza Muda, Mwanasarufi, Mhesabu Kusita kwa Maneno, au Wazo la siku. Ili kujitolea kufanya jukumu, uliza kwenye kundi la maongezi la klabu au orodha ya kupokea habari, au andika kwenda karatasi ya mpango.
Nyaraka kamili za Agora zipo kwenye wiki. Kielezo hiki hapa. Sio lazima kuzisoma zote kwa pamoja (kiukweli, unaweza ukaona ni vitu vingi). Inatosha kusoma kuhusu jukumu ambalo utakuwa unalifanya kwenye mkutano. Majukumu mengi yana video za kufunza namna ya kuzifanya.
Unaweza pia kushiriki kwa kutoa maoni kwa ujumla kwa wazungumzaji. Usione aibu kuelezea ni nini ulifikiria wakati wa hotuba maalum, na usione aibu kuelezea kama kuna kitu ambacho ulikiona hakipo sawa. Wakati huu sio utathmini rasmi, maoni yoyote ya kujenga (haswa kwa wanachama wapya) daima yanakubaliwa na wazungumzaji.
Mwisho, muulize VP wa Elimu wako au Rais wa klabu yako akupe Mkufunzi. Mkufunzi ni mwanachama ambaye ana ujuzi zaidi ambaye atakusaidia kufanya mengi zaidi kwenye uanachama wako wa klabu na kukuongoza kwenye miradi kwanza.
Vitu vya muhimu:
- Kuhudhuria japo mara mbili kwa mwezi - hata kama hauna jukumu kwenye mkutano. Kama hauwezi kuhudhuria kwa muda mrefu, tuambie ili tusikutoe kwasababu haufanyi kitu.
- Klabu nyingi zina njia za ndani za mawasiliano. Inaweza kuwa kundi la maongezi la Facebook, kundi la Whatsapp au telegram, au njia yoyote sawa. Kusoma ujumbe kwenye kundi japo mara moja kila baada ya siku mbili ni muhimu ili kujua mabadiliko yoyote na habari za klabu.
- Kujitolea kwenye majukumu na kuyaandaa.
- Kufuatilia Kundi la Kimataifa letu, kwasababu kwenye kundi hilo ndio tunachapisha habari zote kuhusu Shirika.
Tunatumai Agora itakuwa na umuhimu kwako na pale utakapokuwa na ujuzi wa kutosha wa muundo wetu, utaanzisha klabu yako mwenyewe ya Agora kwenye mji wako.
Tupo
wazi zaidi kupokea mawazo mapya, ukosoaji, mapendekezo, maoni - kila kitu unachotaka kutuambia. Shirika linakua kupitia busara, maarifa, na ujuzi wa pamoja wa wanachama wake wote. Unakaribishwa kututumia ujumbe kwenda
[email protected].