"Agora Speakers International ni shirika lisilo la kibiasahara lililopo duniani kote lenye watu waliojitolea kusaidia watu kuendeleza ujuzi wao wa kuzungumza mbele ya hadhira, mawasiliano, umakinifu, mdahalo, na uongozi."
Kufanya midahalo ilikuwepo kwenye azimio la Agora Speakers tangu mwanzoni. Lakini, mpaka sasa, imekuwa ikipuuziwa kwenye nyenzo za kielimu, na kwenye mwendelezo wa pili wa Mpango wa Kielimu na Mwongozo wa Agora, ni muda wa kulifanyia kazi hili.
Kuna ongezeko la utafiti ukionyesha faida kubwa za mdahalo kama zana ya kielimu:
- Midahalo inaongeza umakinifu, zaidi ya uzungumzaji wa mbele ya hadhira pekee yake (Allen, Berkowitz, Hunt, & Louden, 1999), (Howell, 1943), (Hill, 1993), (Greenstreet, 1993)
- Midahalo ni zoezi la ufanisi zaidi kwa kampusi za chuo kwa ajili ya kufundisha ujuzi wa utafiti.
- Midahalo inatoa faida nzuri kwa watu wanaoingia kwenye ajira kwenye sekta zote (Center, 1982) (Hobbs & Chandler, 1991)
- Kuna mahusiano ya wazi kati ya kushiriki kwenye mdahalo na kuongezeka kwenye ujuzi wa kuandika na kusikiliza.(Mezuk, Bondarenko, Smith, & Tucker, 2011), (Peters, 2009), (Huseman, Ware, & Gruner, 1972)
- Kuna uwiano kati ya kushiriki kwenye mdahalo na kupata nafasi za uongozi kwenye jamii (Keele & Matlon, 1984), (Union, 1960)
- Washiriki wa mdahalo wenye ujuzi wana alama ndogo ya ukali wa sauti kwenye maisha ya kawaida (Colbert, 1993)
- Kufanya midahalo kunapunguza (kwa kama mara tatu) uwezekano wa kuacha shule (Anderson & Mezuk, 2012)
- Kufanya midahalo ni moja kati ya mazoezi yanayopendekezwa na washiriki waliopita. Kiuhalisia, inapendekezwa kwa pamoja na wanafunzi (99.26%), zaidi ya zoezi lolote la kielimu. (Parcher, 1998)
Mashindano mengi ya mdahalo na mifumo ya masharti ya mdahalo ambayo ipo, mengi yao ni kulingana na mifumo ya bunge na utaratibu wa bunge (haswa Utaratibu wa Bunge la Uingereza). Kwa kawaida, inafanywa kwa zamu na mpangilio mkali wa nini kinaweza kusemwa na wakati gani na wakati gani hoja mpya na ushahidi unaweza kutambulishwa. Hata hivyo, kwenye dunia iendayo kasi ya sasa, tunatakiwa pia kuzingatia mifumo mingine ya mdahalo, haswa ile ambayo inafanywa kwenye runinga, redio, au vyombo vya habari sawa, ambapo matendo hayana mpangilio na yenye kasi, au masuala ya aina ya mdahalo ambayo pia yana unyumbufu zaidi, kama vile kesi za kortini au mazungumzo ya biashara.
Midahalo pia ina matatizo yake. Tafiti inayojulikana iliyofanywa na Profesa Nancy Tumposky (Tumposky, 2004) ilihoji kuwa midahalo inasimamia pande mbili, inashawishi washiriki kuangalia masuala kwa mitazamo miwili na kuzingatia kwenye kushinda au kushindwa. Kwa kuongezea, tafiti mbalimbali inaelezea kuwa midahalo ina uasili ya uadui ambayo sio ya kiuhalisia kwa jinsi wanawake na baadhi ya makundi ya wasiowengi wanafikiria na kuwasiliana.
Masharti yaliyopendekezwa ya mdahalo yanajaribu kuweka uwiano kati ya:
- Kutofanya mikutano iwe mirefu sana
- Ina dhumuni ya kielimu
- Iwe ya kiuhalisia sana
- Kuendeleza ujuzi ambao unaweza kutumika kwenye upeo mkubwa wa midahalo ya kweli au masuala ya kufanana na midahalo.
- Kutotengeneza mazingira mabaya ndani ya klabu.
- Kuruhusu midahalo kuwa zaidi ya vipengele vya kulinganishwa ambapo timu moja inashinda na nyingine inashindwa ili kuhimiza kujengwa kwa makubaliano.
Sehemu (1) ni rahisi sana kufanikisha kwa kubadilisha mahitaji kuwa mikutano yote inatakiwa kuwa na seti ya kiwango cha chini ya majukumu ili klabu ziweze kuchagua kuwa na mkutano ambao ni mkutano kamilifu wa kitamaduni, au mkutano wa mdahalo-pekee, au mchanganyiko wa vyote viwili kama muda unaruhusu. Hata hivyo, kutakuwa na hitaji la kuwa na japo midahalo minne kwa mwaka, VPE akiwa na mamlaka ya kuongoza yote. Mdahalo unategemea kuwa kati ya dakika 30 na 90, inategemea na idadi ya timu na muda ambao VPE ameweka kwa ajili ya kila kipengele.
Lakini, inabidi tuwe waangalifu ili tusibadilishe klabu za Agora kuwa klabu za midahalo, kwasababu hili sio lengo. Hii ni hatari kwasababu midahalo huwa inafurahisha na inasisimua zaidi kuliko hotuba zilizoandaliwa kwahiyo zinaweza kuunda aina fulani ya "uraibu". Midahalo inatakiwa kusaidia na kuongea mpango wa kielimu ambao upo tayari, na sio kuwa mbadala wake. Pia, tunatakiwa kukumbuka kuwa lengo la midahalo ya Agora ni ya kielimu sana zaidi kwa wanachama ambao wanashiriki.