Taarifa za Usajili
Agora Speakers International imesajiliwa kama shirika lisilo la kibiashara Shirika Lenye Kujali Umma, chini ya Bulgarian Trade and Nonprofit Registry (Търговски регистър и регистър на ЮЛНЦ), ikiwa na namba ya usajili (EIK): 205228771.
Hali ya Shirika inaweza kuhakikiwa kwa kutumia namba ya hapo kwenye ukurasa huu: https://portal.registryagency.bg/CR/reports/VerificationPersonOrg.
Makao Makuu ya Shirika yapo Madrid, Uhispania
Malengo
Malengo yaliyosajiliwa ya Shirika la Agora Speakers International ni:
- Kuunda na kuimarisha mtandao wa kimataifa wa klabu za maeneo husika ambazo zinasambaza, zinaunda na zinatekeleza malengo ya Shirika katika kiwango cha eneo husika.
- Kuhimiza maendeleo na ukuaji binafsi wa watu, haswa vijana, kwenye taaluma za kutoa hotuba, mawasiliano ya umma, uongozi, umakinifu, na maoni yanayojenga.
- Kuchochea shauku ya miradi ya kijamii na ya kusaidia jamii na ujasiriamali kwenye maeneo hayo.
- Kusaidia kwenye maendeleo ya ujuzi ili kuunda, kupanga na kusimamia miradi yenye kuhusu umma.
- Kuhimiza kubadilishana tamaduni na kuunda mitandao isiyo rasmi na viunganishi kati ya jamii tofauti za wanachama.
- Kuhimiza udadisi wa weledi na shauku kwenye maeneo ya sayansi na teknolojia.
- Kuchochea shughuli za kisayansi, kiteknolojia, za uundaji na zingine za ubunifu kwa vijana.
- Kuhimiza kuendeleza ujuzi wa umakinifu kama njia kuu ya kujitetea dhidi ya kurubuniwa na ubaguzi wa makundi ya jamii.
- Kuhamasisha ustahimilivu na masuluhisho ya amani ya ugomvi kupitia ushirikiano, midahalo, na kufikiria kwa ubunifu.
Shughuli/Mazoezi
Njia ambazo zimesajiliwa na Shirika la Agora Speakers International kufanikisha malengo yake ni:
- Kuandaa na kushiriki kwenye makongamano, mikutano, kozi, na matukio mengine ya kitaifa na kimataifa kuhusu malengo ya kawaida na rasmi ya Shirika.
- Kuandaa kozi, vipindi vya mazoezi, na mazoezi mengine ya nje ya mitaala ya shule ambayo inahusiana na maendeleo ya uongozi na ujuzi wa mawasiliano ya umma ya wanafunzi.
- Kuunda, kuandaa, na kutekeleza mipango ya mafunzo.
- Kuunda na kuchapisha (kwa njia zote mbili, kwa karatasi na kielektroniki) nyenzo zinazohusiana na malengo yetu.
- Kushirikiana na mashirika mengine, taasisi, na watu katika kiwango cha kitaifa na kimataifa kufanikisha malengo ya Shirika.
- Kuandaa mashindano na tuzo.
- Kuunda utaratibu wa kushirikiana na kujenga mitandao ndani ya Shirika.
- Kuunda mfuko wa fedha ili kusaidia na kuendeleza watu ambao wanaweza kusaidia kufanikisha malengo ya Shirika.
- Kazi za hisani
- Shughuli za kuchangisha fedha
Taarifa za Mawasiliano
Unaweza kuwasiliana nasi kupitia [email protected]. Hii ndio njia ya haraka, na tunajibu ndani ya siku moja au mbili za biashara.
Barua zinaweza kutumwa kwenda:
Agora Speakers International
Calle Laguna de Antela 9
28980 Parla, Madrid
Spain
Tafadhali tambua kuwa inaweza kuchukua mpaka siku 15 za biashara kujibu barua. Kwa sasa, hatuwezi kuhudumia wageni.
Hatutoi huduma za mawasiliano kupitia simu.
Michango
Unaweza kutuma mchango kupitia akaunti ya benki ifuatayo:
Agora Speakers International Foundation
IBAN: BG24BUIN95611000609882
BIC BUINBGSF
Kupitia Paypal:
{HTML()}
{HTML}