Jina Letu

 

Jiji la Athens linazingatiwa kwa upana kuwa mahali ambapo demokrasia ilizaliwa, na Agora ya Kale ya Athens inazingatiwa kuwa mfano bora kabisa wa agora za kale za Ugiriki. Kwenye miji ya Ugiriki, yalikuwa ni kituo cha maisha ya kisanaa, kisiasa, na kiroho. Wananchi wote walikuwa wanakusanyika hapo kusikiliza wanasiasa wao na wazungumzaji wakiongea na kujadiliana vipengele vyote vya maisha ya jiji. Kutoka kwenye neno hilo linakuja neno la kisasa la Kigiriki ἀγορεύω - kutoa hotuba, kutoa tamko.

 

Ugiriki pia inadhaniwa kuwa sehemu ya kuzaliwa ya balagha ya zamani - ilikuwa na shule za kwanza ambazo zilizisoma na kuzifanyia mazoezi kwa mfumo maalum. Kiukweli, mazoezi yote ya uzungumzaji wa mbele ya hadhira ya kisasa yanaweza kufuatiliwa nyuma mpaka kwenye shule hizi za mwanzo.

 

Matamshi

Agora inataamkwa na lafudhi kwenye herufi A ya kwanza. Matamshi ya kifonetiki kamili ni /ˈa-gə-rə /.

Unaweza kusikia mfano wa matamshi hapa: https://www.dictionary.com/browse/agora

 

Tunaitwaje?

 

Japokuwa hakuna neno rasmi kwa ajili ya "Wanachama wa Agora" zaidi ya... Wanachama wa Agora, wanachama wetu wengi wanajiita "Agoreans". Kwenye suala hili, lafudhi itakuwa kwenye "o"  /a-'go-ri-əns /

 

Nembo Yetu

Nembo yetu inatoa heshima kwenye urithi huu na inawakilisha kila kitu ambacho tunakitaka kwa ajili ya shirika hili. Uwazi, demokrasia, shauku, na madhumuni.

 

 

Ina vipengele vinne: 

  • Nguzo tatu za Kigiriki ambazo zinawakilisha mahusiano yetu na sehemu ya kuzaliwa ya demokrasia, kanuni zisizopitwa na wakati ambazo tunatetea na kuziamini, na uimara na uthabiti wa shirika letu
  • Uwanja wa nusu-duara wa Kigiriki uliowekwa kimtindo ili kuwakilisha hadhira na pia ukweli kuwa viongozi wanatengeneza mawimbi ambayo yanasambaa duniani.
  • Umbo/Kivuli cha mzungumzaji kwenye pozi la utulivu lakini imara, akiwa na ishara ya mkono wazi, inawakilisha uongozi unaofaa - kufikia watu, maongezi, utulivu, na uthubuti.
  • Moto ambao inawakilisha shauku na maarifa yakitoka kutoka kwa mzungumzaji.

 

Agora Speakers International ina makao makuu nchini Uhispania. Baadhi ya watu wakatoa maoni kuwa rangi za Agora zinafanana na zile za bendera ya Uhispania. Kiukweli, haikupangwa, kwasababu muundo wa kwanza wa nembo uliezelea kiufupi kuwa rangi zinatakiwa zizingatie dhana ya moto na shauku.