Kufundisha uzungumzaji wa mbele ya hadhira na uongozi sio kitu kipya. Ni kuwa tu neno "uzungumzaji wa mbele ya hadhira" ni la kisasa zaidi, na linasasisha tu kile ambacho kimekuwa kikijulikana tangu zama za Aristotle kama "Balagha".
Muundo wa msingi ambao tunatumia - kujifunza kwa kufanyia kazi miradi maalum, yenye malengo, au yanayozingatia masuala maalum ya ugumu unaoongezeka na kupata maoni na utathmini wa kila mmoja - umekuwepo kwa miaka 2,000 sasa, na kiuhalisia, unasambazwa na mashirika mengine ya uzungumzaji wa mbele ya hadhira, warsha, semina, na klabu.
Angalia maelezo haya ya nini kilikuwa kinatokea kwenye darasa la Waromani miaka 2,000 iliyopita.
Walioanza walifanyia kazi msururu wa mazoezi ya utambulisho wa kupata alama ambao uliwafanya wajue mbinu tofauti ambazo zitahitajika kutumiwa kwa pamoja ili kukamilisha hotuba (kwa mfano, kuhadithia hadithi, kukosoa au kutetea kukubalika kwa mtazamo, kubishana kuhusu tasnifu kwa ujumla). … Wanafunzi wataendelea kwenye mazoezi ya kiwango cha juu … ambapo wanapewa masuala dhahania na kuulizwa kuzungumza kwenye upande mmoja au mwingine wa mzozo wa mahakama au mazungumzo ambayo yanaibuka kutoka hapo
Erika Bailey (2019) A Historical View of the Pedagogy of Public Speaking,
Voice and Speech Review, 13:1, 31-42, DOI: 10.1080/23268263.2018.1537218
Je unakumbuka hayo kutoka hotuba zilizoandaliwa na hotuba za papohapo? Kiukweli, hatutumii kile Waromani wametumia, kama vile ambavyo hatutumii magari yanayovutwa na farasi. Tumechukua vipengele vya msingi na kuviendeleza. Hii hapa ni baadhi ya vitu ambavyo vinafanya shirika letu na muundo wetu kuwa wa kipekee na tofauti na wengine:
Kielimu
- Tunahimiza na tunahitaji kazi nyingi za nje ya klabu na kujihusisha kwenye uongozi wa miradi halisi kwenye jamii isiyohusiana na Agora. Tunataka wazungumzaji wa mbele ya hadhira ambao tunawafunza kutoka nje ya klabu na kuzungumza na viongozi ambao tunawafunza wawe na matokeo ya kiuhalisi na chanya kwenye dunia inayowazunguka.
- Kwa ya hapo juu, klabu zina jukumu maalum la ofisa wa VP wa Uongozi wa Jamii ambaye anazingatia tu kwenye kutafuta fursa za uzungumzaji na uongozi kwa ajili ya wanachama.
- Miradi mingi inahitaji sehemu ya uchambuzi wa hotuba ambayo inazingatia kwenye uchambuzi wa hotuba nzuri kutoka kwenye mtazamo maalum na inaonyesha klabu mitindo mingi tofauti ya uzungumzaji.
- Tuna shughuli/mazoezi ya kipekee mara kwa mara:
- Kuzingatia kwenye umakinifu.
- Midahalo yenye masharti maalum ambayo yanahimiza ushirikiano na yanayoruhusu mitazamo kadhaa ya matatizo.
- Michezo ya Lugha inayozingatia maendeleo ya lugha kwa ajili ya klabu zinazotumia lugha za kigeni
- Miradi inayozingatia ustahimilivu na kuishi kwa amani
- Tunafunza uongozi halisi kupitia miradi ya kijamii ambayo inatekelezwa nje ya dunia ya Agora
- Tunafunza wazungumzaji haswa kwenye kukabiliana na kufeli kusikotarajiwa kwa aina yoyote na hadhira yenye hasira.
- Tuna mashindano ya dhamira duniani kote kama vile Hotuba Bora ya Kielimu, Hotuba Bora ya Ufahamu wa Kijamii, au Uhadithiaji Bora wa Hadithi.
- Tuna mwelekeo imara wa kijamii, na tunataka kuwafunza viongozi wa kweli, na sio washauri wa hotuba wajao.
- Tunahimiza klabu zifanye uchunguzi na kujaribu mawazo tofauti ya shughuli/mazoezi ya kielimu, na kuzifanya zitumike na klabu zote.
- Tunaendeleza nyenzo zetu za kielimu na vitabu vya masharti kupitia maoni kutoka kwa jamii kwa ujumla.
- Tunajitahidi kufanya nyenzo zetu za kielimu zipatikane kwenye lugha nyingi ziwezekanavyo.
- Nyenzo zetu zote za kielimu ni bure kwa wanachama.
Kishirika (Uendeshaji)
- Ni bure. Hamna ada au manunuzi ya lazima. Hamna ada za uanzilishi wa klabu, ada za uanachama, au ada za kujiunga, ilimradi klabu yapo ni wazi kwa wote.
- Nyenzo zote za klabu zinaweza kuzalishwa/kuchapishwa kwenye maeneo husika na mtoaji huduma wako anayefaa. Hamna haja ya kuziagiza kutoka sehemu ya mbali na kulipa gharama za usafiri.
- Kuanzisha klabu kunahitaji japo wanachama 8.
- Klabu inaweza kuanzishwa ndani ya siku moja bila makaratasi yoyote - fomu tu ya mtandaoni.
- Muundo wetu wa shirika na mashindano unalingana na mipaka ya kisiasa na kiusimamizi. Kwahiyo, kama ukishinda, wewe ni "Mzungumzaji Bora wa Kielimu kutoka Uhispania" (kwa mfano), na sio "Mzungumzaji Bora wa Kielimu wa Kifungu cha 43, Sura ya 93" au muundo usioeleweka wa kishirika. Ya kwanza inasomeka vizuri sana kwenye wasifu wa kitaaluma.
- Kwasababu wanachama hawalipi chochote, hatujali sana kuhusu ukuaji wa uanachama. Hatuwapi presha klabu kuwa zinatakiwa kuongeza mara kwa mara wanachama (na kuwapuuza wanachama ambao wapo tayari) au kuwasukuma wanachama kupitia mipango ya kielimu kwa haraka. Ukuaji wetu ni wa kiuhalisia, na tunajali kila mwanachama wa klabu kibinafsi.
- Tunashirikiana na mashirika ambayo yapo na kuyaruhusu kufanya nasi kazi na kutoa manufaa yote ya Agora kwa wanachama wao lakini kwa muda huo huo kubaki na utambulisho wao binafsi.
- Tunaruhusu klabu kuhifadhi fedha zote ambazo wanakusanya na kuzitumia kwenye uendeshaji wao wenyewe.
- Tunaweka sheria kali za uwazi wa kifedha katika viwango vyote ili kuhakikisha kuwa fedha zinatumiwa vizuri, na matumizi yanakaguliwa na kila mmoja.
- Tumesajiliwa kisheria kama Shirika Lenye Kujali Umma, aina ya shirika la misaada lenye masharti makali ndani ya Ulaya. Hii inamaanisha kuwa tunaweza kutoa msaada rasmi kwa ufanisi kwa ajili ya shughuli na mahitaji ya klabu.
- Hatuwathibiti au kuwakataza wanachama kukosoa shirika mbele za watu.
Kiteknolojia
- Tunatoa jukwaa la maongezi ya hapo hapo kwa wanachama wetu wote ambayo linawawezesha kuwasiliana bila kutumia tovuti au mitandao ya wahusika wa tatu.
- Tunatoa mfumo wa jukwaa wa duniani kote pamoja na makundi ya kazi ambapo tunashirikiana kuendeleza - pamoja na maoni - vitabu vyetu vya masharti na nyenzo za kielimu na shughuli/mazoezi.
- Nyenzo zetu za kielimu zipo kwenye Wiki ambapo kila mtu anaweza kuchangia, kupanua, na kutafsiri.
- Seva zetu zote na miundombinu ipo ndani ya Umoja wa Ulaya (zipo Ujerumani) ambayo inamaanisha kuwa data zako zinalindwa vikali (The EU GDPR).
- Na mengine mengi yanafuata.