Agora ilianzishwa rasmi Agosti 21, 2016,  kwa tangazo la Facebook kutoka kwa Alexander Hristov. Kila mwaka, tunasherekea siku ya kuanzishwa Agora kwenye Agora International Convention.

Japokuwa tangazo la mwanzo lilizungumzia "muundo wa ada wa kimo cha chini" (ambao mwanzoni ulikuwa unategemea na kiwango cha "per-capita GDP" (wastani wa pato la taifa kwa kila mwananchi) cha kila nchi), ada zilitolewa mwaka 2016 na 2017. Mwishowe, mwaka 2018, ilitangazwa kuwa, kiukweli, Agora itakuwa bure kwa klabu zote za umma. Muundo wa kiuchumi ulibadilika kuwa mmoja ambao unategemea michango, ruzuku za serikali, malipo kutoka klabu za shirika, na kozi za kitaaluma. Daima Agora imekuwa na dira kubwa sana ya mabadiliko kabambe - zaidi ya uzungumzaji wa mbele ya hadhira - na faida za kuweza kufikia watu wengi, kila mahali, bila kujali kiwango chao cha kipato au daraja lao la kijamii, na kuwasaidia kuwa viongozi wa baadae kwa kiwango kikubwa sana kilishinda upotevu wa mapato.

Mwanzo wetu haukuwa mwepesi - nyenzo zote za kielimu zilibidi ziandikwe kutoka mwanzoni. Mfumo mpya wa kielimu ilibidi utengenezwe, miundombinu mipya kabisa ya teknolojia ya habari (IT), seti mpya kabisa ya chaneli za mitandao ya kijamii.

Kwa kuongozea kwenye "maumivu ya kuanzilishwa" yaliyotarajiwa, tulipitia baadhi ya ugumu usiotarajiwa - mashirika shindani waliiona Agora kama kitisho kwenye muundo wa wa kibiashara: tulikuwa tunatoa bure kitu ambacho walikuwa wanatoza, kwa miongo mingi, na wanachama wa mashirika hayo waligundua na wakawa wanahamia Agora.

Mwanzilishi na wafuasi wengi wa mwanzoni walitukanwa, walitumiwa barua za chuki, vitisho binafsi, na hata vitisho rasmi vya kisheria kutoka mawakili wa ngazi ya juu wa ndani ya nchi vya kuacha. Watu wenye nafasi za uongozi ndani ya mashirika mengine waliombwa waachie nafasi zao kwa kuonyesha msaada kwa Agora. Tulipitia pia uharibifu na hujuma za ndani ya shirika. Kutajwa kokote kwa Agora kulithibitiwa, na mtu ambaye alikuwa anaposti alionywa. Watu waliambiwa dhahiri kuwa wasiongelee kuhusu Agora na wasiposti chochote kuhusu sisi. Matukio yote kwenye kipindi hiki yangetosha kuandika kitabu cha kusisimua. Kuna wakati, ilibidi tumuhusishe mwanasheria wetu wenyewe ili kutoa onyo la dhahiri kuwa hatuwezi kuvumilia unyanyasaji wa wanachama wetu kuendelea. Sakata lote hili lilituhamasisha kuposti hiki kifuatacho:

 

 

Lakini, tulivumilia, tukaendelea kusukuma, tukaendelea kukua, na tangu mwanzoni mwa 2021, Agora ilikuwa na klabu zaidi ya 160 ndani ya nchi 70. Sasa tupo thabiti, na tupo hapa kubaki. Na huo ndio kwanza mwanzo... Moto ndio kwanza umeanza kusambaa sasa.

 

Matukio Muhimu ya Agora

Hii ni kazi inayoendelea. Bofya kwenye picha ili kuikuza. Kama unadhani tumesahau tukio la muhimu (haswa kama ni kuanzishwa kwa klabu ya kwanza ndani ya nchi, tafadhali tutumie picha za mkutano, na tutaziongeza.

 

2021

 

2021
Ago (iliyopangwa) Agora imefanikiwa kutafsiri nyenzo za msingi kwenda lugha 20.
Mei 19 Klabu ya kwanza ya Agora nchini China ilianzishwa - Agora China Connectors - ikiongozwa na Aaron Leung
Feb Klabu ya kwanza ya Agora nchini Kanada ilianzishwa - Stand By Me Speakers - ikiongozwa na Fred Jones na Wayne Stanton.  
Feb 14 Mfumo wa Uanachama wazinduliwa
Jan 30 Marathoni ya Pili ya Agora iliandaliwa na Clara Manzo - masaa 36 ya mikutano ya klabu iliyofuatana
Jan 29 Majarida yenye Umakini yaliongezwa kwenye Mpango wa Kielimu

 

 

2020

 

2020
Okt 21 Fred Jones alirekodi Video ya Kwanza ya mafunzo kwa ajili ya majukumu ya mkutano ya Agora.
Okt 15 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Ireland ilianzishwa - Public Speakers Sligo, ikiongozwa na Kieran Timmons.
Okt 15 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Paraguay ilianzishwa - Agora Speakers Ñañe'ē, ikiongozwa na Susana Torres.
Okt 15 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Czech ilianzishwa - Amplion Speakers, ikiongozwa na Radek Bartman.
Okt 15 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Austria ilianzishwa - Agora Speakers Vienna, ikiongozwa na Karin Silvina.
Ago Klabu ya kwanza ya Agora nchini El Salvador ilianzishwa - Agora Speakers San Salvador, ikiongozwa na William Martínez.  
Ago Klabu ya kwanza ya Agora nchini Argentina ilianzishwa -  Agora Speakers Cordoba, ikiongozwa na Fabiana Alicia Fa Luchini.  
Ago 21-22 Marathoni ya Kwanza ya Agora, masaa 24 ya mikutano ya mtandaoni iliyofuatana, iliandaliwa na Clara Manzo, Ravi Bhattarai, Michael Nicholson, na Hélène Kemmere.
Ago 21 Toleo la kwanza la Mpango wa Agora wa Vijana latolewa - kilele cha juhudi ya miezi mingi kilichoongozwa na Fred Jones,  Koka Prasad,  Ravi Bhattarai
Julai 25 Agora yatoa toleo jipya kabisa la wiki ambalo linajumuisha mfumo wa kujiendesha wa uundaji wa rasilimali binafsi za klabu, msaada wa lugha mbalimbali na fomu za kielekroniki za utathmini.
Juni 11 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Guinea-Conakry ilianzishwa - Agora Speakers Conakry, ikiongozwa na with Diané Bangaly.
Apr 1 Kwasababu ya janga linaloendelea, Agora yafanya akaunti za malipo za Zoom kuwa bure kwa klabu zote za umma ambazo zinataka kuendelea na mikutano mtandaoni.
Jan 20 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Ujerumani ilianzishwa- Redeclub Landshut, ikiongozwa na Monika Gräter.
Jan 20 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Ukraine ilianzishwa - Agora Speakers Kharkiv, ikiongozwa na Mohammed Saif.
Jan 13 Kitabu cha Masharti ya Mashindano kwa ajili ya mashindano yetu ya dhamira chachapishwa.
     

 

2019

 

2019
Dis 19 Gea Ban Peng avunja rekodi ya mahudhurio na sherehe kubwa ya mwaka mpya kwa ajili ya Agora Speakers Singapore.
Dis 14 Nchini Ecuador, Klabu ya Kwanza ya Agora yaanzishwa - Agora Speakers Quito, ikiongozwa na Tania Soledad Guerra. klabu yavunja rekodi ya uanzilishi, ikiwa na wanachama waanzilishi 33. Nyuma yake ni klabu ya Guayaquil inayoongozwa na Hector Cedeño, ikiwa na wanachama waanzilishi 23.
Dis 13 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Korea Kusini ilianzishwa - Seoul Agora Speakers, ikiongozwa na Sara Walsh.
Dis 12 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Romania ilianzishwa - Agoramania, ikiongozwa na Gabriela Laslau.
Dis 7 Klabu ya kwanza ya nchini Ukraine ilianzishwa - Agora Speakers Kharkiv, ikiongozwa na Mohammed Saif.
Dis 5 Mwongozo wa Ukufunzi wachapishwa
Okt 23 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Philippines ilianzishwa, ikiongozwa na Celia Alamo Jacob na Fabio Aromatici.
Okt 18 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Uturuki ilianzishwa, ikiongozwa na Ashney Nicolle (Ashinyi Ateghang Nicoline).
Okt 14 Kwasababu ya usaidizi wa Mitch Carson, Agora Speakers International ilizungumziwa na CNN Philippines.
Sep 30 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Ghana ilianzishwa - Agora Speakers Accra, ikiongozwa na Emmanuel Antwi
Sep 29 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Morocco ilianzishwa - Agora Speakers Rabat.
Sep 21-22 Mkutano wa Kwanza wa Kimataifa ulifanyika mjini Lisbon, nchini Ureno.
Sep 19 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Botswana ilianzishwa - Klabu ya Dirisha la Matumaini la Abigail, ikiongozwa na Moiteela Mo-Abi.
Sep 19 Jukwaa la Majadiliano Lilifunguliwa.
Sep 8 "Leo tunasafiri kwenda" Shughuli ya Kielimu iliongezwa.
Sep 6 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Cameroon ilianzishwa, Wazungumzaji 2035, ikiongozwa na Bw. Diangha Clifford
Juni Klabu ya kwanza ya Agora nchini Kenya ilianzishwa - Sura ya Sani Agora Kenya  
Apr 10 Klabu ya kwanza ya Shirika ilianzishwa - kama sehemu ya (Rural Servicios Informáticos), ikiongozwa na Jose Manuel Ropero Tagua.
Machi Klabu ya kwanza ya Agora nchini Malaysia ilianzishwa - Agora Speakers Kota Kinabalu, ikiongozwa na Johan Amilin.
Machi Klabu ya kwanza ya Agora nchini Taiwan ilianzishwa - Wazungumzaji wa Kiingereza Wa Moto wa Taipei - ikiongozwa na Jackie Chen.
Feb Klabu ya kwanza ya Agora nchini Mali ilianzishwa - Agora Speakers Bamako

 

2018

2018
Nov 18 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Thailand ilianzishwa, ikiongozwa na Danupol Siamwalla
Nov 15 Mpango wa Agora wa Vijana ulitekelezwa kwa mara ya kwanza nchini Sierra Leone, ikiongozwa na Angel Zinsel.
Jul 30 Agora Speakers International iliandikishwa rasmi ndani ya Umoja wa Ulaya kama Shirika.
Jul 8 Mpango wa Agora wa Vijana ulizinduliwa, ukiongozwa na Fred Jones pamoja na usaidizi wa Jorge Dias, Ravi Bhattarai, na Koka Prasad.
Juni Klabu ya kwanza ya Agora nchini Japan ilianzishwa, ikiongozwa na Drian Von Golden
Machi 26 Mkutano wa kwanza wa klabu mbalimbali za kanda - Barreiro, nchini Ureno

 

2017

 

2017
Dis Klabu ya kwanza ya Agora nchini Indonesia ilianzishwa - Jakarta Agora Speakers, ikiongozwa na Attie Ringo.
Okt Klabu ya kwanza ya Agora nchini Ethiopia ilianzishwa - Addis Agora Speakers Club, ikiongozwa na Rajendra Singh.
Ago Klabu ya kwanza ya Agora nchini Singapore ilianzishwa  - Agora Singapore Speakers, ikiongozwa na Gea Ban Peng.
Ago Klabu ya kwanza ya Agora nchini Liberia ilianzishwa - Agora Speakers Monrovia
Ago Klabu ya kwanza ya Agora nchini Ureno ilianzishwa - Agora Speakers Barreiro, ikiongozwa na Jorge Dias. 
Jul Klabu ya kwanza ya Agora nchini Jordan ilianzishwa - Amman Speakers, ikiongozwa na Osama Al Mosa.
Mei Klabu ya kwanza ya Agora nchini Mexico ilianzishwa - Agora Speakers Guadalajara  
Apr Klabu ya kwanza ya Agora nchini Nigeria ilianzishwa - Agora Speakers Kaduna  
Machi 26 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Zimbabwe ilianzishwa - "Wazungumzaji wa Baadae", ikiongozwa na Patience Dube.  
Machi Klabu ya kwanza ya Agora nchini Madagascar ilianzishwa -  Agora Speakers Tana - ikiongozwa na Monique (Lene) Vieyra.
Feb 19 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Lithuania ilianzishwa - "Agora Speakers Kaunas", ikiongozwa na Pius Abeshi.
Feb Klabu ya kwanza ya Agora nchini Marekani ilianzishwa - Agora Central Coast Speakers  
Jan 17 Toleo la kwanza la Mwongozo wa Agora lilichapishwa.
Jan Klabu ya kwanza ya Agora nchini Malawi ilianzishwa - Agora Speakers Chisepo, ikiongozwa na Gosten Chikasowa

 

 

2016

 

2016
Dis Klabu ya kwanza ya Agora nchini Uingereza ilianzishwa, ikiongozwa na Hélène Kemmere.
Nov 15 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Afrika Kusini ilianzishwa. "King's Speakers", ikiongozwa na Chris Callaghan
Okt Klabu ya kwanza ya Agora nchini Nepal ilianzishwa - Agora Speakers Kathmandu.
Okt 1 Klabu ya kwanza ya Agora nchini India ilianzishwa, na klabu ya nne duniani kote. - "Visakha Orators", ikiongozwa na Koka Prasad
Sep 28 Klabu ya kwanza ya Agora nchini Poland ilianzishwa, na klabu ya pili duniani kote - "Mówcy Gorzów", ikiongozwa na Michal Papis na Wanda Łopuszańska.
Sep 23 Uandikishaji wa mafanikio wa alama ya Biashara "Agora Speakers International"
Ago 21 Agora Speakers International ilianzishwa rasmi