Kuna njia kadhaa ambazo unaweza kuzungumza kwenye Kongamano la Agora, lakini tafadhali tambua kuwa tunapendelea zaidi watu ambao wanashiriki sana kwenye Agora (aidha kama wanachama au wathamini)

Wazungumzaji Wakuu

Wazungumzaji wakuu wanazungumza wakati wa tukio kuu na kuwasilisha hotuba zenye thamani ya kipekee kwa wanachama. 

Ili kuwa mzungumzaji mkuu, unahitaji kuwa mtaalam mwenye sifa kwenye sekta yako na uthibiti imara wa Kiingereza.

Hotuba kuu:

  1. Lazima iwe ya kuvutia kwa ujumla kwa wahudhuriaji wote wa Kongamano.
  2. Inatakiwa kufuata Kanuni za Msingi za Agora na Sheria
  3. Lazima iwe na asili ya kielimu.
  4. Iwe inahusiana na dhamira ya msingi na kanuni za Shirika la Agora Speakers International.
  5. Lazima iwe na ushauri unaoweza kufanyiwa kazi ambao wanachama wanaweza kutumia kuboresha ujuzi wao.
  6. Lazima uwasilishwe kwa Kiingereza (ikiwemo nyenzo zote za uwasilishaji).
  7. Ushauri, pendekezo, au mbinu zozote ambazo zinapendekezwa kwenye hotuba lazima ziwe zinaungwa mkono na utafiti uliokubalika na wenzako kwenye eneo hilo.
  8. Haitakiwi kutangaza bidhaa, huduma, au mashirika ya mhusika wa tatu.
  9. Haitakiwi kutangaza mitazamo maalum ya kiitikadi, au kisiasa, kimaadili, au kidini.

Ili kujiunga, tafadhali tuma pendekezo lako kwenda [email protected] pamoja na taarifa zifuatazo:

  1. Jina lako kamili.
  2. CV yako, ambayo inatoa maelezo ya kina ya ujuzi wako kwenye eneo au sekta ambayo unataka kuzungumzia.
  3. Ufupisho wa hotuba ambayo unataka kuwasilisha na muda wake.
  4. Rejea za kusaidia utafiti
  5. Jibu la sentensi moja, maalum kwa swali lifuatalo: "Ni nini wahudhuriaji wa Kongamano wataweza kufanya vizuri zaidi kwenye maisha yao baada ya kusikiliza uwasilishaji wako?"

Viongozi wa Warsha

Wazungumzaji wa warsha wanazungumza kwenye matukio ya pembeni na wanaongoza warsha na semina.

Ili kuwa kiongozi wa warsha, unahitaji kuwa mtaalam mwenye sifa kwenye sekta yako na uthibiti imara wa lugha ambayo warsha itawasilishwa.

Warsha:

  1. Lazima ziwe za kuvutia kwa japo baadhi ya wahudhuriaji wote wa Kongamano.
  2. Zinatakiwa kufuata kanuni za msingi za Agora.
  3. Lazima iwe na asili ya kielimu.
  4. Ziwe zinahusiana na dhamira ya msingi na kanuni za Shirika la Agora Speakers International.
  5. Lazima ziwe na ushauri unaoweza kufanyiwa kazi ambao wanachama wanaweza kutumia kuboresha ujuzi wao.
  6. Lazima ziwasilishwe kutumia moja ya lugha rasmi za Kongamano (kigezo hiki kinajumuisha nyenzo zote za uwasilishaji).
  7. Ushauri, pendekezo, au mbinu zozote ambazo zinapendekezwa kwenye hotuba lazima ziwe zinaungwa mkono na utafiti uliokubalika na wenzako kwenye eneo hilo.
  8. Hazitakiwi kutangaza bidhaa, huduma, au mashirika ya mhusika wa tatu.

Ili kujiunga, tafadhali tuma pendekezo lako kwenda [email protected] pamoja na taarifa zifuatazo:

  1. Jina lako kamili.
  2. CV yako, ambayo inatoa maelezo ya kina ya ujuzi wako kwenye eneo au sekta ambayo unataka kuzungumzia.
  3. Ufupisho wa hotuba ambayo unataka kuwasilisha na muda wake.
  4. Rejea za kusaidia utafiti
  5. Jibu la sentensi moja, maalum kwa swali lifuatalo: "Ni nini wahudhuriaji wa Kongamano wataweza kufanya vizuri zaidi kwenye maisha yao baada ya kusikiliza uwasilishaji wako?"

Waandaji wa Kongamano / Maofisa wa Agora

Waandaji wa Kongamano wanaweza wakatoa muda wa kuzungumza wakati wa tukio kuu kwa:

  • Wanachama wa Timu ya maandalizi ya Kongamano
  • Mabalozi wa Agora na maofisa wengine wa Agora
  • Maofisa kutoka klabu za Agora.

Washindani

Unaweza pia kuzungumza kwenye tukio la Kongamano kama umejiweka mwenyewe kwenye mashindano yoyote ya kiwango cha chini ya hapo hapo.

Majukumu ya Kawaida na Wazungumzaji wengine wa Kongamano

Majukumu ya kawaida ya MC / Kiongozi wa Mkutano, Mtunza Muda, Mzungumzaji wa papohapo, na mengine ya aina hiyo yamewekwa kando maalum kwa ajili ya wanachama hai wa klabu hai za Agora.

 

Agora na Wathamini wa Kongamano

 

Wathamini wa Shirika la Agora Speakers International au Kongamano la Agora Speakers wanaweza kuongoza warsha zinazohusiana na huduma au bidhaa maalum ambazo wanatoa. Wanafurahia pia faida za chapa na nafasi. Tafadhali tutumie ujumbe kwenda [email protected] kwa maelezo ya kina zaidi.

 

Mahitaji/Vigezo vya Kawaida

Tunatumia Miongozo ya Maudhui ya TEDx (haswa kwenye kipengele cha "Sayansi Mbaya") ili kuhakiki wazungumzaji wa nje na maudhui ya warsha zao. Barua hii ya jamii kutoka kwa TEDx inajadili kwa urefu vigezo vingi vya kugundua sayansi mbaya.

Wazungumzaji wote wanatakiwa kukubali (kupitia fomu ya kutolewa yenye saini) kutoa leseni ya kudumu, isiyo ya kipekee, isiyo na mrabaha (malipo) kwa Shirika la Agora Speakers International ya maudhui ya uwasilishaji wao na nyenzo, inayoturuhusu kusambaza kwa njia na muundo wowote, bila vizuizi.

Hususan, wazungumzaji wote wanahitaji kukubali kuwa:

  • Hotuba zao na nyenzo za uwasilishaji vitaoneshwa hapo hapo kwa wanachama wote wa Agora wa duniani kote.
  • Rekodi ya hotuba zao na nakala ya nyenzo za uwasilishaji wao utakuwa unapatikana kwa wanachama wote wa Agora wa duniani kote.
  • Vyote vya hapo juu havitolindwa na DRM.