Mdahalo ndani ya mkutano

Mdahalo ni kipengele cha kujitegemea kwenye mkutano, kama vile kipengele cha "Hotuba za Papohapo". Kiongozi wa Mkutano atampa jukwaa Msimamizi wa Mdahalo, ambaye atachukua uongozi kutoka hapo mpaka mwisho wa mkutano, ambapo jukwaa litarudishwa kwa Kiongozi wa Mkutano.

Kama kipengele cha mkutano kipo kwenye mkutano, ni maamuzi ya VPE kuamua ni wapi kwa kuiweka. Hata hivyo, tunapendekeza iwe baada ya hotuba zilizoandaliwa (kwasababu wazungumzaji walioandaliwa kwa kawaida wanakuwa na wasiwasi na wanataka kumaliza haraka iwezekanavyo), na kabla au badala ya "Hotuba za Papohpao" (kama mdahalo unafanywa kabla, kipengele cha Hotuba za Papohapo kinaweza kutumia chochote kilichotokea kwenye mdahalo kama chanzo cha mwongozo wa maswali).

VPE anaamua muda wa kwa ajili ya mdahalo, ambao hauwezi kuwa chini ya dakika 4o, na kama mdahalo utakuwa wakati wa mkutano wa "kitamadhuni" au utakuwa mkutano wa mdahalo tu.

Mada ya hotuba, mitazamo ya kutetewa, na pia timu zinazotetea kila mtazamo lazima zijulikane wakati wa mkutano. Hata hivyo, kwenye ajenda za mkutano, mada ya mdahalo na mitazamo tu ndio inaandikwa, sio muundo wa kila timu inayotetea kila mtazamo.

Hili hapa ni pendekezo la ingizo la ajenda ya mkutano:

Mpangilio wa kuzungumza wa timu unaamuliwa na Kiongozi wa Mkutano kabla ya mkutano kwa droo isiyo na mpangilio na Msimamizii wa Mdahalo anapewa.

Mwanachama wa timu ambaye amekosa kuja kwenye siku ya mkutano haitokuwa sababu ya kutofanya mdahalo.

Mwezeshaji wa Mkutano anatakiwa kuhakikisha kuwa kura za Kuingia na Kutoka zimechapishwa na zipo tayari kwa ajili ya mkutano na zimeshasambazwa kwa wahudhuriaji wote, au japo kuwekwa kwenye meza au viti ambavyo watakuwa wanakaa, pamoja na penseli au peni. Violezo vya kura za Kuingia au Kutoka zinakuwepo kwenye tovuti ya chapa.

 

Muundo na Muda

Mdahalo unaendelea kama ifuatavyo (na mapendekezo ya muda yameonyeshwa)

 

#

JINA LA RAUNDI

MUDA WA CHINI

MUDA WA JUU

1

Utambulisho wa Mkutano na Mkuu wa Mdahalo

1

2

2

Kura za Kuingia

2

2

3

Utambulisho wa Timu na mitazamo yao

1

2

4

Utambulisho wa Majaji

2

2

5

Raundi ya Utambulisho

4 x  # ya timu

6

Raundi ya Maswali na Majibu

0

10

7

Raundi ya Kuhoji

3 x # ya timu

8

Raundi ya Kukanusha

3 x # ya timu

9

Raundi ya Maswali na Majibu

0

10

10

Raundi ya Kuhoji

3  x # ya timu

11

Raundi ya Kufunga

3 x # ya timu

12

Kura za Kutoka

2

2

13

Maoni ya Majaji

5

7

14

Kufungwa kwa Mdahalo

1

1

 

Hii inawapa muda ufuatao kulingana na idadi ya timu:

 

Idadi ya timu

muda wa chini

muda wa juu

2

dakika 45

saa 1 dakika 10

3

saa 1

saa 1 dakika 25

4

saa 1 dakika 20

saa 1 dakika 40

5

saa 1 dakika 35

saa 2

 

Utambulisho wa Mdahalo

 

Pale utakapopokea jukwaa kutoka kwa Kiongozi wa Mkutano, Msimamizi wa Mdahalo anatambulisha mada ya hotuba na anatokea taarifa ya historia fupi ya mada, kama vile kwanini mada hiyo ni muhimu au ni habari gani za hivi karibuni zimetokea ambazo zinaifanya kuwa ya kuvutia au kuipa umuhiu. Msimamizi wa hotuba pia anaorodhesha mitazamo ambayo itatetewa, bila kutoa maoni kuhusu yoyote na bila kuonyesha kupendelea au kukubali yoyote ile.

Timu hazitambulishwi kwenye pointi hii.

Kura ya Kuingia

 

Kama kila kitu ndani ya Agora, tunajitahidi kufanikiwa kupata lengo linalopimika la mafanikio yetu. Lengo la mdahalo ni – ukiachana na kielimu – kushawishi watu kuhusu mtazamo wako. Kwahiyo, kipimo kizuri zaidi cha mafanikio ni kama hiki kweli kimetokea. Hii inafanywa kupitia kura mbili: kura ya kuingia na kura ya kutoka.

Kura ya Kuingia ni kura isiyojulikana inayofanywa kabla ya utambulisho wa timu na wanachama wake, ikiwa na lengo la kujaribu kupata mtazamo kidogo wa kweli wa hadhira wakati inapunguza ushawishi ambao unaweza kutokea unapojua rafiki fulani au mwanachama mwenzako yupo kwenye timu inayotetea mtazamo huu au ule. Bila shaka, muundo wa timu hauwezi kuwa simu, lakini haimaanishi kuwa hatutakiwi kupunguza matokeo.

Baada ya utambulisho wa mada na mitazamo, Msimamizi wa Mdahalo atawaomba wahudhuriaji kujaza Kura ya Kuingia na kumrudishia. Matokeo hayahesabiwi au kutangazwa kwenye pointi hii. Kushiriki kwenye Kura ya Kuingia ni kwa hiari.

 

Kura ya Kuingia na kukusanya kura hakutakiwi kuwa zaidi ya dakika 2.

 

Utambulisho wa Timu

 

Baada ya Kura ya Kuingia kufanywa, Msimamizi wa Mdahalo anatambulisha timu, wanachama wake, na anaelezea mtazamo ambao kila timu itakuwa inatetea. Inapendekezwa kuwa kila timu ipewe jina aidha la namba au herufi moja.

isipokuwa kama haiwezekani, wanachama wa timu wanatakiwa kukaa au kusimama pamoja, tofauti na timu nyingine na hadhira. Timu zote zinatakiwa kukaa pamoja mbali na hadhira – aidha kwenye jukwaa au eneo maalum la kukaa kwenye chumba.

Baada ya Msimamizi wa Mdahalo kutambulisha timu, anatangaza mpangilio wa kuzungumza ulioundwa kabla.

 

Utambulisho wa Majaji

 

Baada ya timu kutambulishwa, na kama kuna Majaji wa Mdahalo, Msimamizi wa Mdahalo anawatambulisha kila mmoja kwa zamu. Kama sio wanachama wa klabu, Msimamizi wa Mdahalo anatakiwa kuzungumza kidogo kuhusu kila mmoja wao na sifa zao. Msimamiz wa Mdahalo hatakiwi kuelezea mtazamo upi (kama upo) ambao Jaji wa Mdahalo kwenye masuala yanayojadiliwa.

 

Raundi ya Utambulisho

 

Wakati wa Raundi ya Utambulisho (sawa na Raundi ya Kukubali au Serikali kwenye mifumo ya kitamaduni ya mdahalo), mwakilishi wa kila timu anaelezea mtazamo wake na hoja ya kusaidia. Mwakilishi anazungumza bila kukatishwa kwa muda wa dakika 3, pamoja na sekunde 30 za kipindi cha nyongeza.

Ishara za muda wa kawaida zinatumika wakati wa hotuba, na Msimamizi wa Mdahalo anatakiwa kumsimamisha mzungumzaji kama amepitiliza muda wa 3:30.

 

Raundi ya Maswali na Majibu

 

Raundi ya Maswali na Majibu ni raundi ambayo Majaji wa Mdahalo na wanachama wa kwenye hadhira (kwa mpangilio huu) wanaweza kuuliza maswali kwa timu. Wanaweza pia kufanya pointi zao kama sehemu ya swali, lakini Msimamizi wa Mdahalo asikubali zigeuke kuwa hotuba.

Kila swali halitakiwi kuwa zaidi ya dakika 1, na kila jibu halitakiwi kuwa zaidi ya dakika 1 pia. Hamna kipindi cha nyongeza kwa ajili ya swali, na kuna kipindi cha nyongeza cha sekunde 30 kwa ajili ya jibu.

Majaji ni wa kwanza kuuliza maswali, na hadhira wanafuata pale majaji watakapokuwa hawana maswali ya ziada.

Maswali ya kufuatilia pia yanaruhusiwa, lakini pia, Msimamizi wa Mdahalo anatakiwa awe mwangalifu hii isigeuke kuwa mechi ya ping-pong au mazungumzo.

Kwa maswali yanayotoka kwa wanachama wa hadhira, mtu anayetaka kuuliza swali moja au zaidi ananyoosha kadi yenye jina la timu ambayo anataka kuuliza na anasubiri Msimamizi wa Mdahalo kumpa nafasi. Maswali yote yanatakiwa kuendana na mada, kuelezewa bila utata, na kuelekezwa kwa timu maalum.

Kiuhalisia, utumiaji wa kadi yenye jina la timu itamruhusu Msimamizi wa Mdahalo kuongoza kipengele cha maswali na majibu, akigawanya maswali ili timu zote zipate idadi sawa ya maswali.   

Baada ya mtu kumaliza kuzungumza, Msimamizi wa Mdahalo anaweza kuwapa nafasi timu lengwa kujibu maswali au anaweza kuamua kuwa swali halikubaliki na kutoa sababu.

Raundi ya Maswali na Majibu inaisha aidha muda uliotengwa kwa ajili yake utakapoisha au pale maswali yatakapoisha.

 

Raundi ya Kuhoji

 

Raundi ya Kuhoji ni sawa na raundi ya maswali na majibu, na ndani yake, timu zinapewa nafasi ya kuhoji timu nyingine.

Mpangilio wa maswali ni kinyume wa mpangilio wa kuzungumza ambao ulipangwa kwenye Raundi ya Utambulisho (kama mpangilio wa kuzungumza ulikuwa Timu ya 2, Timuu ya 3, Timu ya 1, kwa mfano, mpangilio wa raundi ya kuhoji utakuwa Timu ya 1, Timu ya 3, Timu ya 2).

Msimamizi wa Mdahalo atawapa nafasi kwa timu tofauti. Kama kwenye raundi ya maswali na majibu, maswali na majibu hayatakiwi kuwa zaidi ya dakika 1.

 

Raundi ya Kukanusha

 

Raundi ya Kukanusha (sawa na raundi ya Hasi au Kupinga kwenye mifumo mingine ya mdahalo) ni raundi ya pili ya kuzungumza ambapo timu zinaweza kutoa hoja dhidi ya mitazamo ya timu nyingine au kutoa hoja za ziada za kusaidia mtazamo wao wenyewe. 

Muda, ufundi, na mpangilio wa kuzungumza kwenye kipengele hiki ni sawa na Raundi ya Utambulisho.

 

Raundi ya Kufunga

 

Kwenye Raundi ya Kufunga, timu zinatoa matamko yake ya mwisho.

Wakati wa raundi ya kufunga, hamna hoja mpya au kukatizwa kunaruhusiwa.

Mpangilio wa kuzungumza ni sawa na wa raundi ya utambulisho. Hii ni muhimu haswa kwenye kuweka usawa kwenye matokeo ya mwanzo-mwisho.

 

Kura ya Kutoka

 

Baada ya mdahalo kuisha, Kura ya Kutoka inapigwa. Kura ya Kutoka na kukusanywa kwa kura hakutakiwi kuwa zaidi ya dakika 2.

Kama kwenye suala lililopita, Kura za Kutoka ni kura isiyojulikana ambayo inajaribu kupima kama hoja ambazo zimewasilishwa na timu tofauti zimebadilisha mawazo ya hadhira.

Kura ya Kutoka inafanywa bila kujali kama kulikuwa na makubaliano mwishoni au la. Mhudhuriaji anaweza kuchagua kama anataka kushiriki kwenye Kura ya Kuingia tu na sio Kura ya Kutoka, kwenye Kura ya Kutoka na sio ya Kuingia, kwenye zote, au kutoshiriki kwenye zote.

 

Hii inaweza kuwa sampuli ya karatasi ya Kura ya Kutoka (mtindo unaweza kubadilika):

 

Kama kuna muda wa kutosha wa kuhesabu na kufupisha matokeo, matokeo ya kura zote yanatangazwa kwenye mwisho wa mkutano. Kama hakuna, yanawekwa kwenye kurasa ya mtandaoni ya Klabu / kundi la WhatsApp / kundi la Facebook/ blogu, nk. Kama klabu haina yoyote kati ya hii, zinatangazwa kwenye mwanzo wa mkutano unaofuata wa kawaida.