Nadharia zinatosha. Kwa sasa, utakuwa na swali moja maalum, "nikijiunga, ni nini haswa najifunza na kuendeleza?"
Maendeleo kwenye mikutano ya klabu
Mikutano ya klabu za Agora sio "vipindi vya mafunzo" au "semina". Hakuna "wataalam" au "walimu" kwenye klabu ya Agora Speakers - kila mmoja yupo hapo kwa ajili ya utaratibu wao wa kujifunza, kila mtu ana kitu cha kujifunza na kujiendeleza, kila mtu ni rika lako na mpo sawa.
Mlolongo wa kujifunza unatokea kwa kutumia mafunzo mapana ambayo yanatumiwa kwenye sekta yanayoitwa "Mzunguko wa Maendeleo" na mbinu za "kusoma kwa kufanya".
Kwenye kila mradi, utapitia hatua zifuatazo:
Jifunze
Kwenye awamu ya "Jifunze" ya mradi wowote, uta- :
- Utajifunza nyenzo za mtandaoni na rasilimali kwa ajili ya mradi
- Utatathmini yale ambayo wazungumzaji waliofanikiwa na viongozi wanafanya.
- Utauliza maswali na kupata ushauri kutoka jamii yetu ya duniani kote.
- Utashiriki na mkufunzi wako kwenye mazoezi maalum ya mradi.
Jiandae
Sasa utakuwa umejifunza nadharia, ni muda wa kutumia kila ulichokisoma. Bila kujali aina ya mradi - uzungumzaji wa mbele ya hadhira, umakinifu, uongozi, au kingine, utahitaji kufanya mwenyewe. Kwa hilo, utahitaji kujiandaa kwa:
- Kuandika hotuba au kupanga mazoezi ya uongozi kulingana na malengo ya mradi.
- Fanya mazoezi, fanya mazoezi, fanya mazoezi.
- Jadiliana na pata mwongozo kutoka kwa mkufunzi/mshauri wako.
Mazoezi
Sasa ni muda wa kufanya mazoezi kile ambacho umejifunza kwa kuwasilisha mradi wako. Utakuwa:
- Unawasilisha hotuba zilizoandaliwa kwenye klabu yako.
- Kuonyesha matokeo ya miradi yako ya uongozi.
- Kufanya mazoezi masuala yote tofauti kama vile uzungumzaji wa papohapo, midahalo ya mada, au kuulizwa maswali mengi kuhusu maamuzi ambayo umefanya.
- Kuchukua nafasi ya uongozi ndani ya klabu na nafasi za ngazi za juu ndani ya Shirika.
- Kuongoza na kuendesha miradi ya dunia ya kweli ambayo itakuwa na matokeo chanya kwenye jamii yako na kuendeleza maisha ya watu ambao wanakuzunguka.
Pata Utathmini na Maoni
Baada ya mradi kuwasilishwa, utapata:
- Utapata utathmini wa kina kutoka kwa wenzako kwenye mkutano wa klabu.
- Utapata maoni kwa njia ya maandishi kutoka kwa wanachama wengine wa klabu.
- Utapata ushauri kwa ujumla kutoka kwa jamii
- Utaandika jarida ambapo utaandika kile ulichokifikiria kuhusu njia yako na mafunzo uliyopata, na itakuwa kama historia ya maendeleo yako na mwongozo wa wapi unahitaji kujiendeleza.
Maoni ambayo utapata daima yatakuwa ni ya kukusaidia na yanatolewa kwa nia njema ya kukusaidia ujiendeleze. Tofauti na masuala ya kihalisia ya dunia, hamna mtu ambaye atakuhukumu, au kujaribu kuthibitisha kuwa umekosea, au kukufanya uonekane mbaya mbele ya wengine. Kiukweli, usaidizi, urafiki, na ukarimu wa jamii yetu, ambapo wote tunajifunza na kujiendeleza pamoja, ni moja ya vitu vingi ambavyo utavikuta ndani ya Agora.
Rudia
Hamna mtu anayekuwa mtaalam kwenye jaribio la kwanza, na usitarajie kuwa Chopin kwenye siku yako ya kwanza kwenye piano au kuingiza mashimo yote kwenye kozi ya gofu. Msingi wa mafanikio ni kurudia, kupata maoni, kusikiliza wengine, na kuendelea mbele. Kama msemo unavyosema, "Mazoezi huleta ufanisi."
Ni juu yako maoni gani unataka kuyachukua na yapi huyataki. Lengo la Agora ni kukusaidia kuendeleza - kwa kutumia mbinu bora - mtindo wako mwenyewe wa uzungumzaji au uongozi, na sio kuiga wa mtu mwingine.
Mpango wetu wa Kielimu hauna kizuizi cha muda - unaweza kujiendeleza kwa mwendo wako mwenyewe, unaweza kurudia mradi mara nyingi uwezavyo, na kuendelea pale utapokuwa unahisi upo tayari. Tofauti na mazingira ya kiuhalisia ya maisha, hamna penalti ndani ya Agora za kujaribu mbinu za uongozi au uzungumzaji na kugundua kuwa haufanya kazi vizuri. Kiukweli, tunahimiza ufanye hivyo ili uwe tayari umejiandaa pale muda utakapowadia kwenye maisha ya kweli ambapo utatakiwa kupatia.
Je mfumo huu unafanya kazi? Je kozi ya kitaalam sio bora zaidi?
Utafiti unaonyesha kuwa hata ustadi wa kati wa ujuzi (iwe tenisi, dansi, kuogolea, au uzungumzaji wa mbele ya hadhira) inahitaji mazoezi, kwa kawaida zaidi ya idadi ya masaa ambayo umeweka pembeni kufanyia mazoezi kozi za kitaaluma.
Zingatia hiki: Fikiria kuwa unataka kujifunza kupika chakula kizuri. Una chaguo zifuatazo:
- Kujiunga na kozi nzito ya wiki 1-2 inayotolewa na mpishi maarufu, kutengeneza baadhi ya chakula mara moja, kutumia pesa nyingi, na matumaini, baada ya hapo, kuwa umeshakuwa mtaalam.
- Kujiunga na kundi la mapishi. Kila wiki, utakuwa unasoma kuhusu kutengeneza chakula kimoja kutoka nyenzo za mtandaoni, na utapika chakula hicho na wanachama wote wa kundi lako. Kila mtua ataonja na kukupa maoni yake. Kama umeridhika, unaweza kuendelea na aina nyingine ya chakula wiki nyingine. Kama hapana, unaweza kurudia. Kila chakula kipya ambacho utapika kitakuwa kigumu zaidi. Utafanya "mzunguko" huu kila wiki kwa miezi kadhaa, bila kutumia pesa yoyote. Kwa kuongezea, kwenye kundi la mapishi, utajifunza ujuzi tofauti wa mapishi.
- Mbadala, unaweza kusoma sana kuhusu mapishi, kuangalia video nyingi, na kuamini kuwa muda utakapofika wa kuandaa chakula kwa ajili ya wageni wako, utakuwa tayari.
Unafikiri mbinu gani itakuwa bora zaidi?
Agora inachukua mbinu ya pili - utakuwa na ufikivu wa nyenzo zote za elimu, zilizoundwa na wataalam na zenye lengo maalum ya kukuchukua kutoka kwenye viwango vya msingi vya uzungumzaji wa mbele ya hadhira, uongozi, na midahalo na kukupeleka kwenye viwango vya juu zaidi.
Lakini usiamini maneno yetu. Jirekodi mwenyewe, jiunge na klabu kwa muda mfupi, jirekodi tena, na utashangaa ni kwa kiasi gani umeendelea katika kipindi hiki kifupi.
Kiuhalisia, utaendelea tu kama utahudhuria mikutano mara kwa mara na kuchukua majukumu kwenye mikutano hiyo. Kama unaenda kwenye klabu yako ya Agora mara moja kwa mwezi, au hata chini ya hapo - unapoteza muda wako. Itakuwa ni kama kujaribu kuwa mcheza piano au mcheza dansi kwa kucheza mara moja kwa mwezi.
Warsha na Makongamano
Shirika na klabu daima zinaandaa warsha na makongamano ya viwango vyote (mji, nchi, kimataifa, nk). Ukiachana na mikutano ya kawaida ya klabu, utaweza kufurahia warsha nyingi, vipindi vya mafunzo, na semina ambazo zinawasilishwa na wataalam kwenye sekta walizobobea.