Kila mdahalo utakuwa na swali ambalo limeelezewa kwa uwazi, na fupi, na kila timu itatetea jibu maalum, lisilo na utata, na lililoelezewa kwa uwazi kwa swali hilo. Kwa mfano, mada ya mdahalo inaweza kuwa "Je Elimu ya Juu Inatakiwa kuwa Bure?", na kunaweza kuwa na timu tatu, kila moja ikitetea sampuli hizi za majibu:
- Timu Y: "Ndio, daima Elimu ya Juu inatakiwa kuwa bure."
- Timu N: "Hapana, Watu wanatakiwa kuwekeza kwenye elimu yao wenyewe."
- Timu D: "Elimu ya Juu inatakiwa kuwa bure kwa wale wenye chini ya kiwango fulani cha kipato."
Tunahimiza sana kutokuwa na mitazamo miwili ya masuala magumu, kwahiyo tunapendekeza kujaribu kuepuka "timu za ndio" na "timu za hapana" kwasababu ni nadra sana kwa masuala ya dunia ya kweli kuwa na jibu rahisi la "ndio/hapana".
Mada zinatakiwa kuwa za dunia ya kweli, mada zenye umuhimu na zinaweza kupendekezwa kwa VPE na mwanachama yoyote.
Mada ambazo hazifai kwa midahalo (APDA, 2016):
- Zenye upendeleo mkubwa mada ambazo hamna hoja isiyo ya kupendelea inaweza kuwasilishwa. Kwa mfano., Dini gani ni ya "kweli"?.
- Kesi ngumu (Mada ambazo ni vigumu sana au haiwezekani kutoa hoja ya tofauti ya upande wa nafasi ya msingi). Kwa mfano, Mtu yoyote hatakiwi kuteswa na serikali bila sababu.
- Marudio marudio (Mada ambazo jibu moja tu la kimantiki lipo). Kwa mfano: Je Dunia ni ndogo kuliko Jua?.
- Masuala yanayohitaji maarifa maalum (Mada ambazo zinahitaji maarifa maalum ili kuweza kufanya mdahalo vizuri). Kwa mfano: "Kutupa PVC: msombo mbadala."
Wakati wa kuandaa mdahalo, inapendekezwa kuwa VPE awasilishe tu mada kwa wanachama (aidha kwa kielekroniki au katika mkutano) na asubiri watu kuchagua misimamo ambayo wanataka kutetea, kuliko kuwasilisha mada na seti ya chaguo ambayo imeandaliwa kabla. Muundo wa kwanza unaruhusu timu "kuibuka" kiuhalisia na kuepuka kupewa lebo ya kuwa na upendeleo au kuwa upande mmoja.
Inapendekezwa kuwa watu wajiandikishe kwenye timu ambazo zinawakilisha kweli misimamo yao, kuliko kutetea kwa nusu moyo misimamo ambayo hawaiamini.
Ni jukumu la VPE kuamua muundo wa mwisho wa timu.
Midahalo ya Muda / Eneo (kama ilivyo kwa APDA) ni aina maalum ya mdahalo ambapo timu zinaombwa kufanya jukumu la mtu maalum (kwa kawaida kiongozi wa kisiasa) au taasisi (serikali, bodi ya wakurugenzi) katika kipindi maalum kwenye historia. Kwa mfano: "Wewe ni John. F. Kennedy wakati wa Mgogoro wa Makombora wa Kuba. Ndio umepokea picha za setilaiti za hivi karibuni zikionyesha Umoja wa Kisovyeti zikiweka ICBM ndani ya Kuba".
Midahalo inaweza au haiwezi kutoa eneo maalum. Kwenye suala la hapo juu, sio lazima - eneo ambalo Kennedy aliamua mwelekeo wa matendo haukushawishi maamuzi yake. Hata hivyo, kama mada ya mdahalo ingekuwa "Wewe ni Jenerali Gordon Meade; ndio umemshinda Robert Lee pale Gettysburg", basi eneo (eneo la vita ambapo maelfu walipoteza maisha yao) linaweza kuwa na ushawishi fulani kwenye maamuzi yake ya kutowafuatilia jeshi la Confederate.
Midahalo ya Muda/Eneo inaendelea kama midahalo ya kawaida, isipokuwa: kwasababu ni midahalo inaiga masuala ya kihistoria, timu inayowakilisha msimamo maalum haiwezi kutumia taarifa ambayo haikuwasilishwa kwa mtu au taasisi katika muda huo.
Kwa mfano: kama timu inamwakilisha Kaisari wa Japani kwenye Vita Vikuu vya Duniani vya Pili, hawawezi kutumia taarifa za uwepo wa Silaha za Nyuklia. Tambua kuwa sharti hili linazuia utumiaji wa taarifa ambayo haikujulikana na mtu anayewakilishwa, lakini sio taarifa ambazo zilijulikana lakini zikajulikana zaidi mpaka baadae. Kuendeleza mfano sawa, ni sawa kudhania kuwa Kaisari wa Japani alikuwa anajua kuhusu mipango ya mashambulio ya Pearl Harbor kwenye mdahalo unaofanyika tarehe 1, Disemba 1941, japokuwa mashambulio yalitokea tarehe 7.
Taarifa ambazo uwepo wake haujakubaliwa na wanahistoria zinatakiwa ziepukike. Kuendeleza mfano wa hapo juu, haijakubaliwa bado na wanahistoria kama serikali ya Marekani ilitoa au haikutoa taarifa ya shambulio kabla, kwahiyo timu ambayo inawakilisha serikali ya Marekani mnamo tarehe 1, Disemba 1941, shambulio la Pearl Harbor halitakiwi kutumiwa.
Japokuwa APDA inapendekeza sharti kuwa mdahalo unatakiwa kufanywa ukiheshimu haiba ya kisaikolojia ya kiongozi anayeigwa, tunadhani hii itaelekeza mdahalo kuwa wa kisanaa zaidi, kucheza majukumu, na eneo la utafiti kuliko upande wa kimahojiano/kielimu ambao Agora inazingatia. Kwa mdahalo wa Agora, itakuwa sawa kama timu inayowakilisha serikali ya Wanazi kwenye tarehe 20, Juni 1941(Siku mbili kabla ya mwanzo wa Operesheni ya Barbarossa - uvamizi wa Umoja wa Kisovyeti na Ujerumani.) na kutetea hiyo itakuwa si bora kuendelea zaidi kupata alama ya juu zaidi ya timu nyingine na "kushinda". Japokuwa, matokeo ya aina hii ya matukio hayo yangeweza yasitokee daima kwenye historia kwasababu ya haiba ya Hitler.
Inapendekezwa pia kwenye midahalo ya Muda/Eneo, mada zisichaguliwe kutoka matukio ya hivi karibuni au matukio yenye utata mwingi isipokuwa kama klabu ina utamaduni imara wa midahalo ya kistarabu bila hoja binafsi.
Midahalo inaandaliwa na kupangwa na VPE wa klabu japo wiki mbili kabla. Kila mdahalo unahitaji majukumu yafuatayo yawepo:
- Msimamizi wa hotuba.
- Majaji wa mdahalo, inatumika kwenye muundo wa mashindano.
- Mtunza muda wa mdahalo (anaweza kuwa sawa na mtunza muda wa kawaida wa mkutano)
- Timu mbili au zaidi ikiwa na japo wanachama wawili kila mmoja. Kwa madhumuni ya uhalisia, inapendekezwa kusiwe na timu zaidi ya tano.
- Kama ikiwezekana, kila timu inatakiwa kuwa na japo mwanachama mmoja wa ziada ambaye anaweza kuchukua nafasi ya ambaye hatokuja.
- Timu zote lazima ziwe na idadi sawa ya watu kwenye timu.
- Mhesabu Kusita kwa Maneno na Neno la Siku havitumiki kwenye kipengele hiki
- Mwanasarufi anatumiwa kwenye kipengele hiki kwasababu usahihi wa lugha ni lengo la hotuba zote.
- Kama klabu ina mtathmini wa Lugha ya Mwili na mtathmini wa Usikilizaji, jukumu linaweza kutumika kwenye kipengele hiki pia.
- Mtathmini wa Mkutano anatakiwa kumtathmini msimamizi wa mdahalo.
- Kiongozi wa Mkutano anamtambulisha Msimamizi wa Mkutano na majukumu yaliyobaki kama kawaida.
Orodha ifuatayo ya nyenzo inahitajika kwa ajili ya mdahalo:
- "Kura" za Kuingia na Kutoka, kwa kila mwanachama wa hadhira.
- Seti ya kadi zenye majina ya timu au namba (kwa ajili ya kila mwanachama wa hadhira) kwa ajili ya kipengele cha Maswali na Majibu. Kama timu zina majina ya namba moja au herufi moja kama ilivyopendekezwa, hizi kadi zinaweza zikapigwa chapa mara moja na kutumiwa tena kwenye midahalo yote.
Jukumu la msimamizi wa hotuba ni:
- Kutambulisha mada ya hotuab
- Kufanya kura za kuingia na kutoka na kutangaza matokeo.
- Kutambulisha timu na msimamo ambao kila timu itakuwa inatetea.
- Kutoa nafasi kwa timu kwa zamu na kupokea kutoka kwao.
- Kuhakikisha masharti ya hotuba yanafuatwa.
- Kutumia hatua za kinidhamu wakati wa hotuba ili kuweka upole na heshima.
Mtunza muda anamsaidia msimamizi wa mkutano kuthibiti muda wa zamu za kuzungumza.
Kwenye mashindano, Msimamizi wa Hotuba anawapa muhtasari Majaji wa Mdahalo.
Majaji wa Mdahalo wana jukumu la:
- Kuuliza maswali timu wakati wa kipengele cha Maswali na Majibu.
- Kutoa maoni mwishoni mwa mkutano
- Kama hili ni shindano, kutoa alama kwa kila timu.
Wanatakiwa kutokuwa na ubaguzi (kadri iwezekanavyo) na wataalam wenye sifa. Majaji wa Mdahalo sio lazima wawe wanachama wa Agora Speakers members, na, kwa ukweli, inahimizwa kuwa wasiwe hivyo. Baadhi ya mapendekezo ya majaji yanaweza kuwa:
- Walimu au wafanyakazi wa kitivo cha shule au vyuo vikuu.
- Waandishi wa Habari.
- Wanachama wa klabu nyingine za Agora au mashirika mengine ya uzungumzaji wa mbele ya hadhira.
- Wanasiasa wa eneo au wanachama/viongozi wa chama cha kisiasa
- Wamiliki wa biashara.
- Madaktari
- Wanasheria
Wawili wa mwisho wameonyeshwa haswa kwa ajili ya midahalo inayohusu masuala ya kijamii au kimaadili.