Mfumo wetu wa Kielimu una nguzo tano:
Mpango wa Kielimu
Mpango wa kielimu unajumuisha mazoezi tofauti ambayo wataalamu wameunda kwa ajili ya kukusaidia kuwa mzungumaji fanisi, kufanya mdahalo vizuri, na kiongozi anayejiamini. Imepangaliwa kwa muundo ili uanze na vitu virahisi zaidi, hata kama hauna ujuzi kwenye maeneo hayo au ni mpole sana, na kukuongoza kiutaratibu zaidi na zaidi kwenye miradi ya juu. Kitu kizuri ni kuwa utaanza kuona maendeleo baada ya muda mfupi kabisa.
Mpango wa Kielimu umeundwa na wataalam ambao wana mafanikio na wenye miaka mingi ya ujuzi kwenye uzungumzaji wa mbele ya hadhira, saikolojia, uongozi, uandishi wa hadithi, na maeneo mengine mengi.
Nyenzo zote za Mpango wa Kielimu zinapatikana mtandaoni, bure kabisa, kwa wanachama wote wa Agora.
Kutegemea Kabisa Tafiti za Kisayansi.
Uzungumzaji wa Mbele ya hadhira (na kwa ujumla mafunzo yote ya ujuzi laini) ni, kwa bahati mbaya, moja ya maeneo ambayo vitabu vya kujisaidia mwenyewe vimeneza dhana potofu na ushauri wa uwongo au usio na maana, ulionakiliwa na kusambazwa kwenda vitabu vingine na kozi.
Huu hapa ni mtihani ambao unaweza kufanya: Chagua mpango wowote wa uzungumzaji wa mbele ya hadhira ambao unafundisha kushawishi na angalia kama wamejumuisha Monroe's Motivated Sequence. Labda watakuwa wamejumuisha - na baadhi watakuambia kuwa huo ndio muundo wa uundaji wa "PEKEE" ambao unahitaji kutumia kila mara utakapohitaji kushawishi watu. Basi, utafiti umeonyesha kuwa muundo huu maalum hauna nguvu yoyote ya ushawishi dhidi ya hotuba nyingine yoyote ambayo imeandaliwa na kuwa, kiukweli, unaweza kuchanganya au kugeuza kabisa vipengele vyote vya "Motivated Sequence" na matokeo ya ushawishi yatabaki vile vile.
Huu hapa ni mtihani mwingine: Kozi nyingi za uzungumzaji wa mbele ya hadhira zitakuambia kuwa ujitahidi usiwe na maneno ya kujaza sentensi na vimelea vya maneno kwenye hotuba yako. Basi, utafiti unaonyesha kuwa kama hotuba yako haina kabisa maneno ya kujaza sentensi, utaonekana kama hauna uhalisia, na hautoaminika.
Moja ya vipengele vyetu vya msingi vya Mpango wetu wa Kielimu, na ambao tunajivunia sana, ni kuwa unategemea kabisa tafiti za kisayansi. Kila ushauri ambao utasoma, kila zoezi ambalo utafanya, kila mradi ambao utawasilisha ni matokeo ya utathmini wa machapisho ya kisayansi ili kuhakikisha kuwa ushauri unategemea utafiti ambao unaothibitisha kuwa kila kitu kinafanya kazi.
Klabu za Maeneo Husika
Klabu za Agora ni sehemu ambayo burudani inapotokea. Ni mashirika yanayojitegemea ambayo yana uhusiano na Agora na yanaendeshwa na watu wanaojitolea wanaoishi kwenye eneo husika. Kwa kawaida klabu zinafanya mkutano kila wiki, wiki mbili, aidha uso kwa uso, kwenye mtandao, au mchanganyiko wa mbili.
Klabu zinatoa sehemu ya wanachama wa Agora kukutana, kujifunza, na kufanya mafunzo kutumia mpango wa kielimu - mazingira salama, ya furaha na ya kusaidia ambapo unaweza kufanya majaribio bila kuwa na uwoga na kuboresha ujuzi wako mpaka utakapokuwa tayari "kuruka nje ya kiota".
Kama hakuna klabu ya Agora karibu, unaweza kuanzisha moja mwenyewe. Mtu yoyote anaweza kuanzisha klabu. Vitu vinavyohitajika ni muda, nguvu, na japo wanachama 8. Tunatoa nyenzo nyingi za usaidizi na mafunzo maalum kwa waanzilishi wa klabu, kwahiyo tutumie ujumbe kama umevutiwa.
Klabu zina uhuru mkubwa sana wa kuunda mazoezi yake yenyewe. Utaona kuwa japokuwa klabu kwa kawaida zinafuata mbinu sawa na mwongozo wa Shirika, wana utofauti wa mazingira na hali.
Je unataka kujua jinsi gani mikutano ya klabu ilivyo? Angalia rekodi zetu kwenye Chaneli yetu ya Youtube.
Wakufunzi/Washauri
Klabu inawapa wanachama mfumo wa ukufunzi ambao utawasaidia na kuwaongoza wakati wa hatua za kwanza ndani ya Agora.
Mkufunzi/Mshauri wako atakusaidia na miradi yako ya kwanza, atakusaidia kuelewa tamaduni za klabu, kujijumuisha kwenye mazoezi yote, na kukuongoza jinsi ya kutumia mfumo ya mitandaoni na zana.
Jamii ya Duniani Kote
Jamii yetu ni ya utofauti kutoka duniani kote ni rasilimali yenye thamani kubwa sana. Kwa namna yoyote ile, jihusishe na shirikiana nayo. Hudhuria klabu zingine, uliza maswali, omba ushauri na maoni. Ni tunu kubwa kuwa na uwezo wa kukutana na watu wenye historia tofauti na kutoka nchi tofauti.
Mara kwa mara tunaandaa makongamano ya kanda, ya kitaifa na ya kimataifa. Haya ni matukio ambayo unaweza kuhudhuria vipindi tofauti vya kujifunza, kusikiliza wazungumzaji wenye ustadi na hata kushindana kwenye mashindano yetu ya hotuba na uongozi.
Kwa kuongezea, klabu mara nyingi zinaandaa sherehe, matukio, likizo za uzungumzaji wa mbele ya hadhira, marathoni, mazoezi ya uongozi, miradi ya kijamii, na aina zote za mazoezi. Tunajivunia kuwa familia moja kubwa ya Agora.
Unaweza ukajiunga na jamii yetu kwa kutumia mifuno yetu yoyote ya ndani, lakini pia kwenye mitandao yetu yoyote ya kijamii:
Mifumo ya Mitandaoni
Ukiachana na Wiki, tunatumia mifumo zaidi na zaidi ambayo imeundwa ili kukusaidia na vipengele vyote vya yale utakayoyapitia ndani ya Agora. Kutoka mifumo ya hapo hapo ya mawasiliano, majukwaa, nyenzo za nyongeza za kozi, semina za mtandaoni, mahojiano mpaka mifumo ya kisasa zaidi ambayo itakusaidia kuendesha klabu yako au hata kukusaidia kupata fursa za kujenga mitandao. Tuna mipango mikubwa ya nguzo hii ya Agora, endelea kufuatilia.