Shirika la Agora Speakers International ni shirika lisilo la kibiashara, lisilo la kidini, la kielimu la Ulaya ambalo linawezesha watu kuwa wanaweza kufanya mawasiliano vizuri na kuwa viongozi wenye kujiamini ambao wataongoza kwenye kujenga dunia iliyo bora zaidi.
Tunatoa mpango wa kielimu maalum ambao unazingatia kwenye kuendeleza ujuzi wa uongozi, uzungumzaji wa mbele ya hadhira, umakinifu na midahalo.
Mfumo wetu wa mafunzo hauhusishi walimu au madarasa. Ili kujifunza na kujiendeleza, wanachama wetu wanatumia nyenzo za mafunzo za mtandaoni na kujiunga kwenye klabu moja au zaidi za Agora kwenye eneo lao ambapo wanakutana, kufanya mazoezi, na kupokea maoni ya wanachama wenzao mara kwa mara kwenye mazingira yaliyo rafiki na yenye usaidizi. Wakati huo huo, wanashiriki na kuongoza miradi ya uhalisi ambayo yana matokeo ya muda kwenye jamii yetu.
Ilianzishwa mwaka 2016, sasa tuna uwepo kwenye zaidi ya nchi 70 kupitia klabu zaidi ya 150 duniani kote.
Kama shirika la lisilo la kibiashara kabisa, kwa klabu ambazo zipo wazi kwa kila mmoja, mazoezi yetu yote na nyenzo za kielimu ni bure, bila ada zozote za kujiandikisha, za uanachama au za unazilishi, au aina yoyote ya manunuzi ya lazima. Kuanzisha klabu kwenye eneo lako ni bure pia.