Kuna aina tano za klabu za Agora Speakers, mara nyingi inategemea idadi ya vizuizi ambavyo vinawekwa kwenye uanachama wao na namna wanavyotii Mpango wa Kielimu wa Agora.

  • Klabu za Umma ni maarufu kuliko zote na ni aina ya klabu yenye vizuizi vichache na aina ambayo tunahimiza waanzilishi wa klabu kuzingatia. Kwa kuongeza, Klabu za Umma hazilipi ada yoyote kwa Agora Speakers International.
    • Klabu za Rejea ni aina maalum ya klabu za umma ambazo zinatambuliwa kwa kufanya kazi vizuri sana na vinafuata kwa ufasaha Muundo wa Kielimu wa Agora. Ni klabu ambazo zinafaa kuigwa, kama rejea ya jinsi klabu nzuri zinavyotakiwa kufanya kazi.
    • Klabu za Vijana ni aina nyingine maalum ya klabu za umma ambazo ni maalum kwa ajili ya watoto. Wanafuata seti ya majukumu yaliyo rahisishwa, maofisa, na mpango wa elimu uliozoelewa. Kwa kawaida, kuna kizuizi cha umri katika ya miaka 6 mpaka miaka 14, japokuwa inategemea na kila klabu.
    • Klabu zenye Ushirikiano wa Nje ni klabu ambazo zipo katika mashirika mengine (kawaida ni mashirika yasiyo ya faida) na zinakuwa kama klabu za umma za Agora.
  • Klabu zenye Vizuizi ni klabu ambazo zina mahitaji maalum kwa ajili ya uanachama, kwa kawaida ni za kitaaluma au ujuzi fulani. 
  • Klabu zenye Manufaa ya Umma (PIC) ni klabu ambazo zina vizuizi kwenye uanachama lakini zina manufaa kwa umma na, kwahivyo, zina msamaha wa ada zozote. Shirika linatoa hadhi au wadhifa wa Klabu zenye Manufaa ya Umma kulingana na msingi wa kila suala.
  • Klabu za Shirika ni klabu ambazo zipo ndani ya shirika na zipo kwa ajili ya waajiriwa (wafanyakazi) wa shirika hilo tu.

Klabu zote za Agora Speakers zina umuhimu sawa, na wanachama wote wa klabu wanatakiwa kufurahia haki sawa haijailshi ni aina gani ya klabu ambayo wanashiriki.