Kuna aina tofauti ya Miradi ndani ya Mpango wa Kielimu. Baadhi ni miradi ya klabu ya "kawaida" tu, na mingine ina sifa maalum, kama vile kufanya kazi nje ya klabu, kufanya utafiti, kuongoza watu ambao sio wanachama, nk. Sifa hizi zinaonyeshwa na ikoni zifuatazo: (tambua kuwa mradi mmoja unaweza kuwa na ikoni moja au zaidi ya kwa wakati mmoja)

 

Miradi ya Msingi

 

Mradi wa Klabu

Miradi mingi inahusisha kuandaa na kuwasilisha hotuba ndani ya klabu yako, kulingana na na malengo maalum. Ili kukusaidia kuandaa hotuba, unaweza kutumia miongozo yetu ya kielimu na rasilimali, na unaweza kuomba ushauri kutoka kwa mkufunzi/mshauri wako. Baada ya kuwasilisha hotuba, utapata utathmini wa kina na maoni ambayo itakusaidia kukuboresha kama mzungumzaji.

 

Miradi ya Uchambuzi wa Hotuba

Miradi ya Uchambuzi wa Hotuba ni sehemu ya kila mradi wa Njia ya Msingi ya Kielimu. Inahitaji uchambuzi wa hotuba maarufu kwa kutumia mtazamo maalum/tofauti na kuwasilisha uchambuzi wako mbele ya klabu. Kwa kufanya hivyo, wewe na wanachama wenzako mtakuwa mmetambulishwa kwa hotuba mbalimbali za duniani kote ambazo zinaweza kuwa mfano wa kuigwa au kuhamasisha.

 

Miradi ya Juu

Jinsi unavyoendelea kwenye miradi ya juu zaidi, haswa ile iliyopo kwenye njia maalum, utakutana na masuala yenye changamoto zaidi na zaidi, yote ikiwa na malengo ya kukufanya uwe na mawasiliano mazuri na kuwa kiongozi mwenye kujiamini.

 

Mradi wa Utafiti

Mradi wa utafiti hauhitaji tu kujiandaa na kuwasilisha hotuba lakini pia kufanya utafiti kidogo kabla na baada. Kwa mfano, kwenye Usahili wa Kazi, hautojiandaa tu kwa ajili ya mahojiano yenyewe ya kazi lakini pia utatafiti kampuni na nafasi ambayo unaitaka. Kwa hotuba ya kushawishi, utataka kujua kabla ni wapi hadhira yako itakuwepo ili kuona kama wanahitaji ushawishi kwanza.

 

Mradi Uliopimwa

Kwenye miradi unaopimwa, utapata maoni kwa ujumla kutoka kwa mtathmini wako na kipimo cha namba cha ufanisi wa mradi wako. Hamna "alama ya kufaulu" au "alama ya kufeli", wala hamna kiwango chochote cha kupita (isipokuwa kama umejiwekea mwenyewe), lakini kipimo kipo kusaidia uwiano kati ya mtazamo wako mwenyewe wa jinsi mradi ulivyoenda na hali halisi.

 

Mradi wa Dunia ya Kweli

Kadri muda unavyoenda na unashiriki zaidi na zaidi ndani ya klabu yako, utazoea na utaweza kuzungumza mbele ya wanachama wenzako. Japokuwa haya ni maendeleo mapya yanayokaribishwa kuhusiana na masuala ya kijamii, sio vizuri kwenye suala la kukufunza au kukupa changamoto. Kwenye njia za juu za Mpango wa Kielimu, utakuta miradi ya "Dunia ya Kweli" mingi sana. Miradi ya Dunia ya Kweli inahitaji uache sehemu yake ambayo umeizoea ya klabu yako na kuwasilisha hotuba au kuongoza watu nje ya mazingira ya klabu. Ikiwa ni kutumbuiza kwenye klabu ya vichekesho, kuwa na nafasi kwenye thieta ya uigizaji wa papohapo, au kuongoza kampeni ya shirika lisilo la kibiashara, miradi hii itakufanya kupaa mbali ya kiota na kuingia kwenye dunia ya kweli na kupitia masuala mbali mbali yenye changamoto.

Miradi yote hii imeundwa kukuhamasisha na kukupa changamoto na kukutambulisha kwa utaratibu kwenye "dunia ya kweli", ambapo vitu havithibitiwi na havitabiriki kama ilivyo kwenye klabu yako.

 

Kuboresha dunia

Mradi wa mwisho na wenye changamoto zaidi (na wa kuridisha) kwenye Mpango wa Kielimu, haswa kuhusiana na ujuzi wa uongozi, hautokuwa tu ni kitu kizuri sana cha wewe kujifunza lakini pia kitakuwa na matokeo chanya kwenye maisha ya watu nje ya Agora. Kwenye "Kuboresha Dunia", utakuwa unaongoza kampeni za mashirika yasiyo ya kibiashara au kampeni za hisani, uchangishaji fedha, utaandaa matukio, na kwa ujumla, utajifunza kuwa hata mtu mmoja - wewe - anaweza kusaidia kufanya dunia iwe sehemu bora zaidi. .