Mkutano wa Kwanza
Wakati wa kuanza safari na na mshauriwa wako mpya, unatakiwa kwanza kupanga mkutano wa kwanza wa "kutaka kujuana". Kama unaweza, jaribu kukutana na mshauriwa kibinafsi - inaweza kuwa katika mgahawa wa kahawa, kwenye bustani, sehemu ya kuchangia ya kufanya kazi, nk. Mnaweza mkakutana kwenye mahali pa mkutano, kabla au baada ya mkutano.
Kama hiyo haiwezekani, unaweza kutumia teknolojia nyingine za mikutano ya mtandaoni - simu kupitia Facebook au WhatsApp, Skype, nk. Cha muhimu ni kuonana ili uweze kutambua kuwa unaongea na mtu wa kweli.
Uliza kuhusu nini mshauriwa wako anapenda. Watu wengi wanapendelea moja kati ya "miguu" mikubwa ya mpango wa Agora - inaweza kuwa uongozi, inaweza kuwa midahalo / umakinifu, inaweza kuwa kuzungumza mbele ya hadhira. Uliza kuhusu matarajio yake, alichopitia mpaka sasa. Mwambie kuhusu ujuzi wako mwenyewe kwenye maeneo hayo - bila kujali kama hayo aliyopitia yalikuwa ndani ya Agora ama kwingine.
Unatakiwa kutoka kwenye mkutano wa kwanza na:
- Uelewa wa wazi wa matarajio ya mshauriwa na malengo yake ya muda mfupi na muda mrefu.
- Seti ya wazi ya masharti ya jinsi ya kuelekea mbele, ikiwemo ni mara ngapi na lini mtakutana au kuwa na vipindi vya ushauri (yaani, ratiba)
- Makubaliano ya njia ya mawasiliano ambao mtatumia kuwasiliana. Msitawanyike na mbaki na njia moja tu ya mawasiliano - inaweza kuwa barua pepe, WhatsApp, simu, Facebook, nk. Kwenye masuala ya kipekee (kama vile mtu akihitaji kutuma kiambatanisho au video, nk.) hapo mnaweza kuamua njia nyingine za kuwasiliano kama vile huduma ya kutuma viambatanisho au barua pepe.
- Lengo la muda mfupi kwa ajili ya mkutano ujao.
- Makubaliano ya muda ambao mshauriwa atajitolea kwenye zoezi.
Shughuli za kuwa Mshauri wa Uzungumzaji wa Mbele ya Hadhira
Kwa kawaida, kuwa mshuri wa uzungumzaji wa mbele ya hadhira kuna vipengele viwili:
- Maudhui ya Hotuba
- Uwasilishi wa Hotuba
Kwenye maudhui ya hotuba, utataka kuona jaribio la awali la hotuba kabla. Angalia vitu vyote vya msingi - muundo, hoja, lugha, utambulisho, hitimisho, nk. Alafu toa mapendekezo ya jinsi ya kuboresha. Utaratibu huu unaweza kurudiwa mara kadhaa mpaka hotuba itakapokuwa tayari. Kumbuka kuwa lengo lako ni kumsaidia mshauriwa kuendeleza namna yake mwenyewe ya uandishi wa hotuba, na nidhamu, kuliko wewe kurekebisha masuala hayo. Onyesha matatizo na toa mapendekezo, lakini usiandike tena hotuba kwa ajili ya mshauriwa wako.
Kwenye kuwa mshauri wa uwasilishi wa hotuba, ni bora zaidi kumuuliza mshauriwa kuwasilisha hotuba uso kwa uso - aidha kwa kuonana au kutumia maongezi ya video. Hotuba zilizorekodiwa sio kiashiria kizuri kwasababu hauwezi kujua ni mara ngapi majaribio yalifanyika kurekodi, kama imehaririwa, au inaweza kuwa suala la kuwa mshauriwa yupo huru zaidi kuzungumza mbele ya "webcam" kuliko mbele ya mtu uso kwa uso.
Haswa kuhusu miradi kutoka Njia ya Kielimu, hakikisha kuwa mshauriwa anaelewa malengo ya kila mradi na ana fahamu vigezo vya utathmini. Mfahamishe kuwa anaweza kuwasiliana na mtathmini wake kumuomba awe macho na baadhi ya vitu maalum ambavyo mshauriwa ana mashaka navyo. Kwa mfano, hata kama mradi maalum ni kuhusu Lugha ya Mwili, mzungumzaji anaweza muuliza mtathmini kufuatilia matumizi yake ya vifaa vya balagha.
Tatizo la kawaida ni la mshauriwa kuishiwa na mawazo ya nini cha kuzungumzia. Daima wahimize washauriwa kuzungumzia vitu ambavyo vina umuhimu kwao au ambavyo wana hisia kali navyo, hata kama ni vya utata au ni kavu. Kwa uhakika, ni changamoto nzuri kwa mshauri ni kumpa mtu ushauri wa kuwasilisha maoni ya utata kwa namna ambayo haitotenga au kupingwa na hadhira au kuwasilisha mada ambayo isiyo ya kusisimua kwa namna ambayo wengine watasikiliza kwa umakini na kuona inafurahisha.
Kama mshauri, unatakiwa kuwepo kwenye mkutano ambao mshauriwa wako atawasilisha mradi wake. Usikae mstari wa mbele - tayari umeshapata uwasilishaji wa "mstari wa kwanza" wa kutosha wakati wa vipindi vya faragha. Badala yake, kaa nyuma. Hii itakuruhusu kuiona hotuba kupitia mtazamo wa hadhira. Kwahiyo, utaweza kugundua matatizo hapohapo ambayo hayawezi kuonekana vinginevyo, kama vile visaidizi kuonekana kidogo tu, sauti haisikiki vizuri, matatizo ya kuangalia watu machoni kwa sehemu ya hadhira, nk.
Jaribu kuongea kwa faragha na mshauriwa wako baada ya uwasilishi kuisha. Muulize alijisikiaje, kama ana furaha na jinsi vitu vilivyotokea, nk.
Kuwa Mshauri wa Miradi ya Jamii
Kuwa mshauri wa miradi ya jamii kutajumuisha mikutano ya kabla na baada ya kila hatua ya mradi.
- Kwenye mkutano wa baada, unachambua na mshauriwa wako.
- kama alikuwa amejiandaa kikamilifu kwenye hatua ambayo inafuata,
- kama imeandaliwa vizuri na
- kama matarajio ni ya kiuhalisi na yapo kwenye nyaraka.
Toa mapendekezo na ushauri wa jinsi ya kuboresha mpango uliopo, lakini kumbuka - usifanye kazi ya mshauriwa. Pia, kumbuka kuwa haya ni mahusiano ya mshauri-mshauriwa na sio uhusiano wa ubia. Hivyo, jaribu kujizuia kuingia kwenye mawazo ya "mradi wetu", ambao umekuwa mshiriki sawa na mshauriwa, ambapo unafanya vipindi vya kufikiria mawazo na kupeana mawazo tofauti. Utataka kutoa ushauri na mapendekezo, lakini mradi lazima ubaki kuwa mradi wa mshauriwa.
Kwa mfano, mradi unaweza kuwa na hatua ya "kuchangisha pesa". Kutana na mshauriwa wako kabla ya zoezi la kuchangisha pesa halijafanywa na jadiliana kuhusu vitu kama:
- Je kuna mpango wa kuchangisha pesa unawezekana?
- Je kuna vitu maalum vya kufanywa, watu maalum wa kuyafanya, na washirika maalum wa kuwasiliana nao wa zoezi hili?
- Je ni rahisi kwa washirika wote walioombwa kutoa msaada?
- Je gharama kamili imetajwa?
- Je haya matarajio ni ya kiuhalisi?
- Ni nini kinaweza kwenda vibaya? Je hatari zimefikiriwa? Ni mikakati gani imewekwa ili kuishughulikia?
· nk.…
Baada ya hatua hii kufanywa, angalia matokeo na mshauriwa wako. Je kulikuwa na matatizo yoyote? Yaliyotarajiwa, yasiyotarajiwa? Ni nini kinaweza kufanyika kuboresha?
Kama hatua fulani ya mradi wa kijamii ni ndefu (zaidi ya wiki moja), ni wazo zuri kupanga mikutano kadhaa ili kuona jinsi gani kazi inavyoenda.
Kuwa Mshauri wa Majukumu ya Mkutano
Kwa kawaida, kuwa mshauri wa jukumu maalum kutajumuisha mkutano wa mara moja ambao utakuwa na:
Maswali ya ufafanuzi kuhusu jukumu. Kumbusho, lakini, hautakiwi kuelezea jukumu. Kumbuka sharti kuwa washauriwa wanatakiwa kufanya kazi zao wenyewe. Hii inajumuisha kusoma nyaraka kuhusu jukumu na kuangalia video ambazo zinaendana. Jibu maswali ambayo hayajajibiwa kwa uwazi kwenye nyaraka.
Kufanya uwasilishaji mfupi wa jukumu na kutoa maoni ya namna ambayo limefanywa.
Kumsaidia mshauriwa kwenye mawasiliano yake kwenye Jukwaa la Agora la Mtandaoni na/au na maofisa wa klabu ili kumsaidia kupata jukumu hilo kwenye mkutano ujao.