Ajenda ya Msingi inakusudiwa kwa klabu ambazo zimeanzilishwa na ambazo wanachama hawana ujuzi wa kabla na Agora. Inatakiwa kutumiwa mpaka pale ambapo klabu itakuwa inajiamini na majukumu ambayo yapo ndani yake. Pale ambapo wanachama watakuwa na uelewa mzuri wa jinsi vitu hivi vinavyofanya kazi na Makamu wa Rais wa Elimu ameshachaguliwa, wanaweza kuongeza shughuli au mazoezi mapya kwenye seti ambayo tayari ipo.
Inafaa hata kwa mkutano wa kwanza, na inahitaji idadi ndogo ya watu kutekeleza na kwa wakati huo huo kuwa wa kielimu na wenye kufurahisha. Kati ya shughuli zinazowezekana za mkutano zote, ina seti ya vipengele vya msingi:
Ajenda
Ajenda hii ya msingi inahitaji japo watu 8, na ina majukumu yafuatayo:
- Kiongozi wa Mkutano.
- Mzungumzaji ambaye atafanya hotuba ya mradi wa kwanza. "Kuzungumzia Kuhusu Vitu Unavyovipenda" (Mradi wa #2 kutoka Njia ya Kimsingi ya Kielimu)
- Mtu ambaye angependa kufanya zoezi la "Wazo la siku".
- Mtunza Muda
- Mwanasarufi. Anatakiwa kuwa pia Mhesabu kusita kwa maneno (maneno ya kujaza sentensi).
- Mtathmini wa Hotuba wa kutathmini mzungumzaji. Mtathmini wa hotuba anatakiwa pia kusoma makala hii ya jinsi ya kufanya utathmini fanisi na mradi wa hotuba wenyewe, ambao una kadi ya utathmini na vigezo.
- Kiongozi wa Hotuba za Papohapo.
- Mtathmini wa Mkutano.
Washiriki wanatakiwa kujitolea kufanya majukumu tofauti, au wanaweza kuchanguliwa bila mpangilio kama hamna makubaliano.
Pale watakapopangwa, kila mmoja anatakiwa kufahamu mahitaji ya kila jukumu alilopangiwa kwa kusoma nyenzo zilizounganishwa.
Kama kuna washiriki zaidi ya 8, unaweza kuongeza majukumu ya "Wazo la siku" au hotuba na utathmini.
Nyenzo - Mikutano ya uso kwa uso
Kwa kufanya mkutano kwa namna hii, utahitaji nyenzo zifuatazo: .
- Ajenda yenye vipengele na nani atakuwa anafanya kipi. Hapa una kiolezo cha word kilichopendekezwa ambacho unaweza kubadilisha. Hamna haja ya kujaza majukumu ya Ofisa katika kipindi hiki.
- Saa ya kusimama au simu ya mkononi yenye "timer" kwa ajili ya mtunza muda.
- Seti ya ishara za nyekundu, kijani, na njano (zinaweza kuwa karatasi tatu za rangi) ili kufanya kazi ya ishara za muda.
- Karatasi kwa ajili ya ripoti ya mtunza muda. Unaweza kutumia kiolezo cha word hiki.
- Karatasi kwa ajili ya ripoti ya mwanasarufi. Unaweza kutumia kiolezo cha word hiki.
- Fomu za utathmini za kawaida. Utahitaji moja kwa kila anayehudhuria kwa kila hotuba. Kwahiyo, kwa mfano, kama una watu wawili ambao wanafanya mradi wa hotuba na watu 10 wamehudhuria, unahitaji fomu 20. Hapa una kiolezo rahisi (PowerPoint) na kiolezo chenye ufafanuzi zaidi (photoshop). Unaweza kubadilisha zote mbili na kuweka taarifa za klabu yako. Kama hauna PowerPoint au muda wa kubadilisha, unaweza kutoa chapa fomu hii ya kawaida ya PDF.
- Kadi ya utathmini kwa ajili ya kila mradi wa hotuba. Kadi za utathmini zipo kwa chini kwenye kila mradi, kwahiyo kwa ajili ya "Kuzungumzia Vitu ambavyo Unapenda", shuka mpaka chini ili uweze kuipata.
- Mwanasarufi atahitaji kuandaa karatasi yenye neno la siku ambalo amelichagua. Neno linatakiwa kuandikwa kwa herufi zenye ukubwa wa kutosha ili kila mtu aweze kuona.
- Peni kwa kila mmoja.
Nyenzo - Mikutano ya Mtandaoni
Kama mkutano upo mtandaoni, hamna vingi vya kufanya kwasababu elementi zote zinapatikana mtandaoni, na Kitengeneza Rasilimali chetu kinaweza kuzitengeneza.
Kitu muhimu sana kwa nyenzo za mkutano wa mitandaoni ni kuhakikisha kuwa:
- Watathmini wanajua wapi kwa kupata Kadi za Utathmini kwa ajili ya mradi husika. (Hizi zinapatikana chini ya kila mradi, jukumu, au shughuli)
- Mtunza Muda anatakiwa kuamua ni kwa namna gani ataashiria muda. Tena, unaweza kutumia Kitengeneza Rasilimali chetu kutengeneza mandharinyuma za Zoom zenye rangi husika.
Kwa bahari mbaya, "zoom bombing" au udukuaji wa mkutano vimekuwa tatizo kubwa sana. Kwa kawaida, Mwezeshaji wa Mkutano ana mamlaka ya kuhakikisha kuwa watu ambao wanasumbua au kuvuruga mkutano wanatolewa hapo hapo. Kama hamna Mwezeshaji wa Mkutano, unaweza kumuomba mwanachama yoyote ambaye unamuamini kufanya jukumu hilo. Vyovyote vile, hakikisha kuwa una mkakati ambao umeandaliwa wa kukabiliana na wasumbufu kuliko kufikiria hapo hapo nini cha kufanya.