Ndani ya Agora, kuna unyumbufu kuhusiana na kuunda ajenda ya kila mkutano. Tuna shughuli/mazoezi mengi sana ambayo ni vigumu kuvifanya kwenye mkutano mmoja. Hii ni moja ya sababu ambayo inafanya mikutano ya Agora kuwa tofauti sana - daima sio muundo sawa unaotumika mara zote. Ni ya kitofauti sana, yenye kuburudisha na bado inakuwa na uzingatiifu wa kielimu.
Mahitaji ya Mkutano
Klabu ni bure - na tunahimiza - kutambulisha majukumu mapya, kubadilisha mpangilio wa vipengele, kutambulisha mawazo mapya kabisa au kujaribu kubuni mawazo mengine, ili mradi yanalingana na malengo, dhamira, na kanuni za Shirika na yana uhalisia wa kielimu.
Hata hivyo, kuna seti ya mahitaji ambayo yanahitajika kuwepo kwenye mkutano wa kawaida ili kufanikisha kazi kuu ya mkutano: kuelimisha wanachama kuhusu seti maalum ya ujuzi na kufuata mpango wa kielimu wa Agora Speakers International. Hii pia inahakikisha kiwango fulani cha uthabiti wa klabu duniani kote.
Kuna aina za klabu tofauti ambazo zina mahitaji tofauti kulingana na ukaribu ambao unafuata Muundo wa Kielimu wa Agora. Tafadhali angalia makala maalum kwa ajili ya aina ya klabu ambayo unaendesha.
Na zaidi, mahitaji ya chini kwenye mkutano wa kawaida ni haya yafuatayo:
- Kunatakiwa kuwa na Kiongozi wa Mkutano mmoja kwenye mkutano wote.
- Vipengele vyote na washiriki wa mkutano lazima wazingatie muda uliowekwa na Mtunza Muda na matumizi yao ya lugha lazima yatathminiwe na Mwanasarufi.
- Isipokuwa kama klabu imeanzishwa mwezi uliopita, kunatakiwa kuwa na japo hotuba ya mradi mmoja (hotuba ambayo inafanywa kulingana na mmoja ya miradi ya Mpango wa Kielimu).
- Hotuba zote lazima zitathminiwe.
- Kama kuna miradi ya hotuba, inatakiwa kutathminiwa kulingana na karatasi za utathmini wa hotuba na japo mtathmini mmoja.
- Kama hakuna hotuba za miradi, inatakiwa kutathminiwa kulingana na malengo maalum ambayo mzungumzaji ameweka kwa ajili yake mwenyewe, ambayo yanatakiwa kujulikana kabla. Klabu inaweza kuchagua kuwa na mtathmini zaidi ya mmoja wa kutathmini hotuba moja, kuwasilisha kile kwa kawaida kinachoitwa "utathmini wa jopo".
- Japo mtathmini mmoja anatakiwa kuelezea malengo ya hotuba kabla ya hotuba yenyewe ili hadhira wajue ni nini cha kutegemea na ni nini cha kutoa maoni. Hii sio muhimu kama malengo ni sawa na hotuba iliyopita na tayari yameshaelezewa (na inaweza kutokea, kwa mfano, kama wazungumzaji wawili au zaidi kwenye mkutano wanawasilisha hotuba sawa)
- Utathmini wa kila mradi lazima uwasilishwe kwa mdomo na mbele ya watu na mtathmini (watathmini) kwenye mkutano huo huo ili mzungumzaji na hadhira waweze kufaidika na maoni ambayo yametolewa. Utathmini lazima ufanyike kwa kutumia fomu ya utathmini inayofaa kwa ajili ya mradi.
- Hadhira inatakiwa kupewa dakika 1-2 baada ya hotuba ili kuandika maoni ya maandishi kuhusu mzungumzaji.
- Kunahitajika kuwa na Mtathmini wa Mkutano wa kutathmini mkutano kwa ujumla na majukumu ambayo hayakupata maoni kutoka kwa watathmini maalum.
Kuna mahitaji kwa ajili ya mikutano ya kawaida, yamara kwa mara. Kwa matukio maalum, sherehe, mikusanyiko, vipindi maalum, mashindano, midahalo, nk., muundo ni bure. Hata hivyo, idadi ya mikutano hii maalum haiwezi kuwa zaidi ya idadi ya mikutano ya kawaida kwa mwezi.