Kongamano la Kimataifa la Agora (kwa kawaida linaitwa "AgoraCon") ni matukio ya siku kadhaa ambapo wanachama kutoka duniani kote wanakusanyika kwa ajili ya kushindana, kujifunza, kukutana kijamii, na kuunda Agora ya hapo baadae. Japokuwa Agora ndio kiini cha kila kitu, malengo yake, na dhamira yake, ni matukio ya wazi ambayo mtu yoyote anaweza kuhudhuria. Uanachama ndani ya Agora sio kigezo. Kuhudhuria Kongamano la Agora ni, bila kukuza, tukio la kubadilisha maisha. Idadi ya watu ambao utakutana nao, undugu, urafiki, na ukarimu ambao utakaohisi, maarifa ambayo utapata, na mitandao ambayo utaiunda itabaki kwa miaka mingi baadae.
Kila Kongamano la Agora lina nembo na dhamira maalum. Kwa mfano, Kongamano la kwanza la mwaka lilikuwa "Kuwa na Ndoto Kubwa. Hakikisha Inafanyika". Kongamano la Pili (ambalo lilihairishwa kutoka mwaka 2020 mpaka mwaka 2021 kwasababu la Janga la UVIKO19) ambalo lilikuwa na kauli mbiu ya "Viongozi Wapya kwa Wakati Mpya."
Makongamano ya Agora yanafanyika kila mwaka, kwa kawaida karibia na siku ya kuzaliwa - Agosti 21. Kila mwaka mji na nchi tofauti zinachaguliwa kuwa mwenyeji wa Kongamano. Uchaguzi unategemea idadi ya vigezo, kama vile:
- Ukuaji wa klabu kwenye kanda hiyo.
- Uwepo wa miundombinu ya usaidizi ya kutosha (vitovu vya usafiri, hoteli, nk.)
- Ufikivu wa eneo - vya kisiasa (kama vile vigezo vya kuingia ndani ya nchi) na utendaji (kama vile usalama, ufikivu, nk.)
- Kujitolea na uwezo wa waandaaji kuandaa kwa mafanikio tukio la ukubwa huu.
- Eneo la kongamano lililopita (kwa mfano, kongamano la kwanza lilikuwa Ulaya Magharibi, haitowezekana Ulaya Magharibi au hata Ulaya kuchaguliwa kwa kongamano linalofuata).
Tofauti na shughuli nyingine, kuhudhuria Kongamano sio bure na tiketi zinabidi ziuzwe. Manunuzi ya tiketi yanaenda kwenye kulipia gharama kama vile kukodi ukumbi, chakula, na gharama za miundombinu (zana, taa, samani), mahitaji, huduma za kitaaluma kama vile upigaji picha na kurekodi video, na hata gharama za kulipia mgeni mashuhuri au wazungumzaji wakuu.
Shughuli
Waandaji wa kongamano wana unyumbufu kwenye kuamua nini kitatokea wakati wa Kongamano, na ndio maana makongamano mawili hayawezi kuwa sawa.
Katika kiini, kila Kongamano litakuwa na "Tukio Kuu" linalotokea kwenye Ukumbi Mkuu wa Kongamano na litakuwa na:
- Hotuba kuu moja au mbili
- Fainali za Mashindano
- Warsha moja au zaidi
- Gala ya chakula cha usiku
- Mpango wa burudani
- Tukio la kujenga mtandao.
- Sherehe za Tuzo - kwa ajili ya washindi wa shindano na wanachama wengine mashuhuri
Kwa kuongezea, kunaweza kuwa na "Matukio ya Pembeni" kwenye vyumba tofauti ambapo warsha, vipindi vya mafunzo, au matukio mengine yanaweza kutokea.
Hii hapa ni mifano midogo ya shughuli ambazo zilifanyika wakati wa Kongamano la Lisbon 2019 (bonyeza kwenye kila picha ili uone picha kwa ukubwa).
Masuala ya Kisheria
Kabla ya kufanya mipango ya kuhudhuria Kongamano, daima angalia kama unahitaji viza kwenye nchi mwenyeji wa kongamano na, kama unahitaji, ni nyaraka gani unahitaji kuwasilisha.
Pale utakapoamua kwenda, usicheleweshe maombi ya viza - baadhi ya nchi zinaweza kuchukua mpaka miezi miwili kabla ya kukupa viza.
Barua za Usaidizi wa Viza
Kwa mtu yoyote anayetaka kuhudhuria Kongamano ndani ya Umoja wa Ulaya na anahitaji barua rasmi ya mwaliko kutoka kwa Agora kwa ajili ya kuomba viza nchini kwao, tafadhali tutumie risiti ya tiketi yako ya Kongamano na taarifa zako kwa ujumla (jina kamili kama linavyotokea kwenye pasipoti yako na eneo unaloishi) kwenda [email protected] na tutakutumia barua ya mwaliko ndani ya siku moja ya kibiashara. Tafadhali tambua kuwa ni maamuzi ya kila ubalozi kukubali au kukataa barua hii, na hatuwezi kuthibiti hili.
Tunaweza tu kutoa barua ya usaidizi wa viza pale utakapojiandikisha kwa ukamilifu na kulipia kongamano kwasababu ya sababu za kisheria.
Viza kwa ajili ya nchi maalum lazima zichukuliwe nje ya nchi hiyo (na viza za nchi zozote kutoka eneo la Schengen lazima zichukuliwe nje ya eneo). Ukiachana na barua ya hapo juu, hatuna ushawishi au nguvu ya aina yoyote kwenye utaratibu wa viza, na hatuwezi kutoa taarifa za hali ya viza ya mwombaji au kuhusu nyaraka za muhimu.
Pia, kumbuka unaweza kupata maelezo yote ya kisheria ya shirika letu hapa.
Tafadhali tambua kuwa Agora Speakers International imeandikishwa ndani ya Umoja wa Ulaya. Barua zetu za usaidizi zinaweza kukubaliwa na balozi za nchi za Umoja wa Ulaya, lakini sio sehemu nyingine.
Bili
Kwa ajili ya kupata bili yako ya tiketi, tafadhali wasiliana na muandaaji wa Kongamano.