1. LENGO LA MIONGOZO HII
- Mwongozo wa Chapa unaelezea masharti yote ambayo ni lazima yafatwe muda wowote ambapo klabu inataka kutumia rasilimali za kidijitali kutoka kwenye Tovuti ya Chapa ya Agora Speakers International.
- Klabu zilizosajiliwa tu ambazo zimepewa namba ndio zinaweza kutumia rasilimali za kidijitali za Shirika.
- Rasilimali zinaweza kutumika tu kwa madhumuni yanayohusiana moja kwa moja na malengo na dhamira ya Shirika na lazima zitumike kulingana na Kanuni za Msingi.
- Rasilimali zote za Agora Speakers International zinalindwa na hakimiliki. Kwa kuongezea, nembo na mwale (mwako wa moto) ni alama za biashara zilizosajiliwa.
- Miongozi hii haiwakilishi uhamishaji wa hakimiliki wa aina yoyote. Masharti ya kusimamia matumizi ya rasilimali za kidijitali zinaweza kubadilika muda wowote. Idhini inayotolewa kwa klabu kutumia rasilimali hizi zinaweza kutenguliwa muda wowote kama Shirika likigundua kuwa rasilimali zinatumika vibaya.
2. DHUMUNI LETU
Agora Speakers International ni shirika lenye watu waliojitolea kusaidia watu kuendeleza ujuzi wao wa kuzungumza mbele ya hadhira, mawasiliano, umanikinifu, majadiliano, na uongozi.
3. VIPENGELE VYA MAANDISHI
Jina Letu
Jina letu kamili ni Agora Speakers International. Unaweza kutuita kwa njia yoyote ile ifuatayo:
- Agora
- Agora Speakers
- Agora Speakers International
- Shirika la Agora Speakers International
Hata hivyo, tafadhali kumbuka, kuwa "Agora" ni neno lenye asili ya Kigiriki na, kwahiyo, ukitumia tu "Agora," kunaweza kuwa na mchanganyiko na makampuni mengine ambayo yanatumia neno hilo na ambayo hayahusiani na sisi.
Jina letu haliwezi kurekebishwa, kutafsiriwa, au kutoholewa. Daima linaandikwa kwa kutumia seti ya herufi za Kilatini, bila kujali lugha lengwa. Kwa mfano, yafuatayo ni matumizi yasiyo sahihi ya jina:
- Агора
- Ágora Speakers
- Agoras Foundation
Kwa kawaida, kwa lugha ambazo alama ya kubainisha matamshi inaonyesha lafudhi ya neno (kama vile Kihispania), Agora inaweza kusisitizwa tu kama itakuwa pekee yake. Kwa mfano, Ágora inaweza kuwa sawa, lakini Ágora Speakers - hapana.
Dhamira yetu
Dhamira yetu ni ifuatayo:
“Agora inakuwezesha kuwasiliana vizuri na kuwa kiongozi anayejiamini ambaye atajenga dunia iliyo bora.”
Dhamira haiwezi kurekebishwa kwa aina yoyote ile, isipokuwa:
- Kutafsiri kwenda lugha tofauti.
- Kubadilisha “Agora inakuwezesha” kwenda “Tunakuwezesha” pale inapofaa kwenye nyenzo, pale ambapo nembo ya Agora Speakers International pia inapoonekana. Hamna mabadiliko mengine yanaruhusiwa (kwa mfano, hauwezi kuibadilisha iseme "Agora Speakers Madrid inakuwezesha...")
Hamna maandishi yoyote ambayo yanaruhusiwa kuongezewa kwenye dhamira.
Sehemu zote za Agora Speakers na klabu zote shirika zina dhamira hii moja.
3. SIFA ZA KUONA
Paleti ya Rangi Kuu
NYEKUNDU |
HEX Web safe: CC3300
RGB: 206, 60, 23
CMYK: 13%, 90%, 100%, 3% |
NJANO |
HEX Web safe: FF9900
RGB: 247, 175, 15
CMYK: 2%, 34%, 100%, 0 |
ZAMBARAU ILIYOKOLEA |
HEX Web safe: 660033
RGB: 86,15,59
54%, 99%, 46%, 47% |
Paleti ya Rangi za Sekondari
HEX Web safe: FFCCCC
Hex: F9D7CF
RGB: 249,215,207
CMYK: 1%,17%,13%,0%
|
|
HEX Web safe: FF6666
Hex: F47C60
RGB: 244,124,96
CMYK: 0%,64%,62%,0% |
|
HEX Web safe: cc3300
Hex: CC3C17
RGB: 204,60,23
CMYK: 14%,90%,100%,4% |
|
HEX Web safe: 993333
Hex: A0353B
RGB: 160,53,59
CMYK: 26%,90%,75%,19% |
HEX Web safe: FFFFCC
Hex: F4F2D4
RGB: 244,242,212
CMYK: 4%,2%,19%,0% |
|
HEX Web safe: FFFF99
Hex: F7E99A
RGB: 247,233,154
CMYK: 4%,4%,49%,0% |
|
HEX Web safe: CC9933
Hex: D1952A
RGB: 209,149,42
CMYK: 17%,43%,100%,0% |
|
HEX Web safe: 996633
Hex: 976B1E
RGB: 151,107,30
CMYK: 34%,54%,100%,18% |
HEX Web safe: CC99CC
Hex: CCB2D6
RGB: 204,178,214
CMYK: 18%,31%,0,0 |
|
HEX Web safe: 666699
Hex: 765285
RGB: 118,82,133
CMYK: 62%,77%,22%,4% |
|
HEX Web safe: 003366
Hex: 15416E
RGB: 21,65,110
CMYK: 99%,80%,32%,18% |
|
HEX Web safe: 333366
Hex: 351C4D
RGB: 53,28,77
CMYK: 88%,98%,37%,37% |
Nembo
Muundo Kamili wa Mlalo |
|
Muundo wa Mraba |
|
|
|
Muundo kamili wa mlalo. |
|
Muundo wa mrabo unaweza kutumika tu kwenye vyombo vya habari vya kidijitali ambapo nembo ya mraba inahitajika (ikoni, zana tumizi, nk.) |
Muundo wa Mlalo Uliorahisishwa |
|
|
Inaruhusiwa tu kwenye nyenzo ambazo zinashikika ambapo ukubwa wa logo na rezolusheni ya nyenzo lengwa inafanya isiwezekane kuwa na uzuri wa kina. Kwenye masuala haya, upana wa nembo lazima usiwe mkubwa zaidi ya sentimita 5.
|
Nafasi na Ukubwa wa Nembo
Nafasi ya Nembo |
|
Ukubwa |
Daima acha nafasi ya japo ukubwa wa herufi "S" kuzunguka nembo, kama inavyoonyeshwa. |
|
Chapa
sm2 |
|
Tovuti
128px |
|
Utofauti wa Nembo
Utofauti ufuatao wa nembo ni pekee unaokubalika. Zote zinaweza kupakuliwa kwenye Tovuti ya Chapa.
Kijivu juu ya uwazi |
Rangi juu ya rangi iliyokolea |
Nyeupe juu ya rangi iliyokolea |
Marufuku za Nembo
Nembo haiwezi kubadilishwa kwa namna yoyote ile. Haswa usifanye yafuatayo:
Usibadilishe vipengele |
|
Usibadilishe rangi. |
|
Usibadilishe maandishi |
|
Usiweke mbwembwe |
|
Usibadilishe uwiano wa vipengele. |
|
Usizungushe au kupinda |
|
Usiweke kwenye ulinganuzi wa chini. |
|
Usiweke kwenye rangi ambazo hazipo kwenye paleti. |
|
Usiweke chochote juu au chini ya nembo. |
|
Usijumuishe nembo na vipengele vingine. |
|
Usitumie nembo kwa nyuma. |
|
Usitenganishe vipengele vya nembo. |
|
Usitafsiri nembo. |
|
Usitumie nembo zenye rezolusheni ndogo au ambazo zimeskaniwa. |
|
Usitumie picha ambazo zinazuia kusomeka vizuri. |
|
Usichapishe kwenye wino unaong'aa. |
|
|
|
|
Kuunganisha na nembo nyingine
Nembo haiwezi kutokea, bila idhini iliyoandikwa, pamoja na nembo nyingine zisizo za klabu isipokuwa kwenye muktadha wa kuorodhesha wathamini, kumbi za mikutano, au mikutano saidizi inayohusiana na mashirika sawa, na hizi zinaorodheshwa wazi. Kwenye suala hili la mwisho, nembo ya klabu (za klabu) au matukio ambayo yanathaminiwa lazima yatokee pia, na lazima kusiwe na mchanganyiko kwamba ni klabu/tukio ndio linathaminiwa na sio Agora Speakers International.
Inaruhusiwa |
Hairuhusiwi |
|
|
Fonti
ABCDEFGHIJKLMNOPRQR
STUVWXYZ |
Fonti kuu ni CapitalisTypOasis. Inajumuisha herufi kubwa (na seti ya Latini-1 tu), namba, na vituo vya uandishi. |
ABCDEFGHIJKLMNOPRQRSTUV
WXYZabcdefghijklmnopqrstuwxyz
01234567890[]()!?={}*/&%\
áéíóúâêîôûàèìòùñÑäëïöüçÇ |
Fonti ya sekondari ya American Garamond BT ambayo ni fonti kamili ya MSIMBOSARE |
4. NYENZO MAALUM
Agora Speakers International inaruhusu klabu kuwa na unyumbufu kwenye matumizi ya nyenzo za chapa na rasilimali za kidijitali kutengeneza nembo, vyeti, tuzo, vifaa vya ofisini, hata bidhaa, na kutengeneza vyote hivyo kwenye maeneo yao au kuagiza kutoka kwa mtengenezaji ambao klabu inaona anafaa.
Nyenzo Maalum zinaweza kutengenezwa kwa ajili ya matumizi ya klabu, matukio (kama vile mikutano mikubwa, mashindano, nk.), maeneo ya kijiografia (kwa mfano., kipeperushi cha klabu zote kwenye mji), makundi ya lugha (kwa mfano, Wazungumzaji wa Kijerumani), nk., lakini haziwezi kutengenezwa na wanachama kwa ajili ya matumizi yao binafsi (kwa mfano, kadi ya biashara iliyobuniwa maalum kwa ajili ya matumizi ya mwanachama mmoja au wawili wasiojulikana).
Kwenye mwongozo huu, kwa ufupi, tutaviita vyote nyenzo za "klabu" na jina na nembo ya klabu, tukio, eneo la kijiografia, kundi la lugha, au vinginevyo vitaitwa kama "jina la klabu na nembo".
Nyenzo zote maalum zinahitaji kufuata masharti yafuatayo:
- Lazima zifuate sheria.
- Zinaweza tu kutengenezwa na kutumiwa na klabu.
- Lazima zihusiane na dhamira ya Agora Speakers International.
- Ushirikiano na Agora Speakers International lazima uonyeshwe.
- Utumiaji wa nembo ya Agora lazima ufuate Mwongozo wa Chapa.
- Mwandishi wa nyenzo atakuwa na jukumu pekee kama kutakuwa na madai ya hakimiliki dhidi yake na mhusika wa tatu.
- Jina la klabu na/nembo daima lazima viwepo, lazima iwe kubwa zaidi ya Agora, na lazima daima ionekane zaidi kuliko nembo nyingine ambazo zipo.
(Ili kuzuia watu kufikiria kuwa nyenzo maalum ambayo imeundwa na klabu ni nyenzo rasmi ya Agora Speakers International).
- Klabu zinaweza kuzitengeneza kwenye eneo lao au wanaweza kuagiza kutoka mtengenezaji yoyote ambae wanaona wanafaa.
- Kama taarifa za mawasiliano zinapatikana, taarifa za mawasiliano za klabu na taarifa za mawasiliano za Agora Speakers International lazima ziwekwe wazi kwa kutenganishwa, na japo tovuti ya Agora Speakers International lazima iwepo (www.agoraspeakers.org)
5. RASILIMALI ZILIZONYAMBULIWA
Nyenzo zilizonyambuliwa ni vitu ambavyo vimebadilishwa kutoka violezo rasmi au ambavyo vinajumuisha sehemu ya rasilimali za kidijitali za Agora Speakers International (kwa mfano, sehemu za nembo, sehemu ya dhamira, fonti, na paleti za rangi ya jina la Agora, nk.)
Kwa mfano:
Sehemu hizi zinafanya nembo hii kuwa «iliyonyambuliwa»
Rasilimali zote ambazo zimenyambuliwa lazima, ukiongezea na masharti ya rasilimali maalum, zifuate masharti yafuatayo:
- Hakuna haki za Hakimiliki zinaweza kuwekwa au kudaiwa kwenye nyenzo zozote ambazo zimenyambuliwa. Hii inamaanisha, kwa mfano, kama unatengeneza baadhi ya kadi za kibiashara au nembo za klabu yako inayotumia rasilimali za kidijitali za Agora, hauwezi kuzisajili kama hakimiliki au alama ya biashara.
- Haziwezi kuhusishwa kiitikadi, kidini, vyama vya kisiasa, au mitazamo ya kiduniani.
6. KUONESHA USHIRIKIANO
Klabu zote zinazoshirikiana zinahitaji kuonesha ushirikiano wao na Shirika kwa wazi. Ushirikiano na Agora Speakers International unaweza kuoneshwa kwa kujumuisha nembo ya Agora Speakers logo na kwa hiari pamoja na maneno "kwa kushirikiana na" au maneno yanayofanana. Jina la klabu na/au nembo zinatakiwa kuwa kubwa zaidi ya nembo ya Agora Speakers.
Sio sahihi |
Sahihi |
|
|
7. NEMBO ZILIZONYAMBULIWA
Agora Speakers International zinahamasisha klabu kuunda nembo za klabu zilizonyambuliwa kutoka nembo rasmi.
Nembo zilizonyambuliwa hazitakiwi kujumuisha vipengele vingine kutoka nembo nyingine zinazojulikana au alama za aina yoyote.
Hairuhusiwi |
Inaruhusiwa |
|
|
Nembo iliyonyambuliwa haiwezi kuwa na vipengele vingine vyovyote kutoka nembo nyingine zinazojulikana au alama za aina yoyote.
(Bila kujali masuala ya kisheria ya nembo nyingine, na hata kama wewe ndio mmiliki wa kisheria au una idhini ya kuitumia. “Alama” hapa inahusu alama dhahania na pamoja na namna ya mtazamo wa kidunia (kisiasa, kiitikadi, au kidini) au inahusiana na shirika tofauti. Haimaanishi vitu halisi ambavyo vimefanikiwa kuwa na cheo cha ishara kama vile mnara wa Eiffel kama ishara ya Paris, au Tia kama ishara ya Marekani, au Don Quixote kama ishara ya Uhispania)
Inaruhusiwa |
Hairuhusiwi |
|
|
Ushirikiano na Agora Speakers International lazima utokee kwenye mawasiliano yote.
Sio sahihi |
Sahihi |
|
|
8. VIFAA VYA OFISINI
Bango la Klabu
Ili kuwa na uthabiti wa chapa duniani kote na uwepo wa klabu, klabu yoyote ambayo inataka kuwa na bango lazima itumie muundo na saizi rasmi. Kumbuka kuwa sio lazima kwa klabu kuwa na bango. Kigezo hiki kinamaanisha tu kuwa klabu ambayo inataka kuwa na bango, inabidi itumie iliyo rasmi.
Bango la klabu
Klabu zinaweza kutengeneza bango kwenye eneo lao au wanaweza kununua kutoka kwa mtengenezaji, ili mradi liwe na ubora na nyenzo ziwe sawa.
Vipengele Vingine
Kwa vipengele vingine vyovyote (kama vile kadi za biashara, vipeperushi, vijitabu, nk.), klabu zina unyumbufu kamili wa kutumia violezo vilivyopendekezwa kwenye Tovuti ya Chapa, kuzibadilisha, au kuunda nyingine mpya kabisa, vikiwa na vizuizi vifuatavyo:
- Muundo lazima ufuate Mwongozo wa Chapa na masharti ya kuunda nyenzo.
- Muundo lazima uweke wazi kuwa mawasiliano au vifaa vya ofisini vimeundwa na klabu na sio chapisho rasmi la Agora Speakers International.
9. MACHAPISHO
Machapisho ya klabu
Klabu zinaweza kuunda aina zote za machapisho (vitabu, majarida, vipeperushi, nk.), kwenye muundo wowote (kidijitali, chapa, sauti, nk..) ikiwa tu:
- Muundo lazima ufuate Mwongozo wa Chapa na masharti ya kutengeneza nyenzo.
- Kichwa na muundo hakusababishi mchanganyiko na machapisho mengine ambayo tayari yapo ya Agora Speakers International.
- Hamna maudhui yanaweza kutengenezwa kutoka machapisho mengine (ikiwemo machapisho ya Agora Speakers International) bila idhini ya maandishi kabla.
Inaruhusiwa |
Hairuhusiwi |
|
Kichwa kinagongana na chapisho rasmi |
Muundo unagongana na chapisho rasmi |
Haiendani na dhamira yetu |
|
10. TUZO
Tuzo ni tokeni zozote za utambuzi zinazotelewa na klabu na kupewa mtu (sio lazima mwanachama) au shirika jingine.
Hii inajumuisha, kwa mfano:
Vyeti
|
|
Pini
|
|
Riboni
|
|
Vikombe
|
|
Medali
|
|
Medali za Kidijitali
|
|
|
|
|
Tuzo Rasmi
Tuzo na Vyeti rasmi vya Agora Speakers International vinaweza kutengenezwa na kutolewa tu na Agora Speakers International.
Tuzo Maalum
Klabu zinaweza kutengeneza vyeti, tuzo, riboni, na ishara nyingine za utambuzi wao wenyewe, na kuzitoa wanavyotaka, ili mradi:
- Tuzo zinatolewa kwa matendo au matukio muhimu ambayo yamefanywa na kumalizwa tayari (kama vile, vyeti haviwezi kutolewa tu kwa "kujaribu tu")
- Tuzo inatolewa kwa matendo ambayo yanaendana na dhamira ya Agora Speakers International na inafuata sheria zake.
- Matokeo ya matendo au matukio yanategemea kwa dhahiri juhudi, ujuzi, na maarifa ya mpokeaji tuzo (ikimaanisha: tuzo haziwezi kutolewa kwa vitu ambavyo vinategemea bahati au kuingiliwa kati na wahusika watatu)
- Tuzo hazina ubaguzi (ikimaanisha kila mwanachama anaweza kuipata)
- Tuzo haitakiwi kuwa na fidia yoyote ya kiuchumi pamoja nayo.
- Muundo unafuata Mwongozo wa Chapa.
- Tuzo haichukui nafasi au kuingiliana na tuzo rasmi ambayo tayari ipo.
- Kusiwe na mchanganyiko wowote kuwa mtoaji wa tuzo ni klabu na sio Agora Speakers International.
- Hakuwezi kuwa na maandishi au muundo ambao unaonyesha kuwa Agora Speakers International imeidhinisha tuzo na vyeti hizi.
- Japo mwezi na mwaka ambao tuzo imetolewa lazima iwepo. Isipokuwa, kwa tuzo ambazo zinatolewa mara moja kwa mwaka tu, mwezi unaweza kuondolewa.
|
|
Mifano ya Tuzo Sahihi
Inaruhusiwa
(Vyeti vimetumiwa kama mfano, lakini masharti yanatumika kwenye aina zote za tuzo)
Mifano ya Tuzo zisizo Sahihi
Hairuhusiwi
(Vyeti vimetumiwa kama mfano, lakini masharti yanatumika kwenye aina zote za tuzo)
Haihusiani na dhamira ya Agora
Speakers International |
|
Agora Speakers International
inaonekana kama mfadhili shiriki |
|
Ina ubaguzi |
|
Inakiuka sharti la kutokuwamo |
|
Haifuati Mwongozo wa Chapa kuhusu utumiaji wa nembo |
|
Hakuna ushirikiano umeonyeshwa |
|
Inaingiliana na tuzo rasmi ambayo ipo |
|
Haifuati Mwongozo wa Chapa wa nyenzo maalum (slaidi ya 18) |
11. BIDHAA
Klabu zinaruhusiwa kubuni na kutengeneza bidhaa zao wenyewe kwenye maeneo yao chini ya masharti yafuatayo:
- Muundo lazima ujumuishe nembo ya klabu kama kipengele muhimu sana kinachoonekana. Kwa hiari inaweza kujumuisha nembo ya Agora Speakers International kwenye nafasi isiyoonekana sana na kwa saizi ndogo.
- Muundo lazima ufuate Mwongozo wa Chapa.
- Bidhaa zinaweza kuuzwa katika bei iliyo juu ya gharama ya kutengeneza, ikiwa kuwa tofauti kati ya hivyo viwili inatumiwa kwa madhumuni sawa ambayo yanaruhusiwa na fedha za klabu.
- Bidhaa zinaweza kuuzwa na kutumwa duniani kote.
Mfano wa bidhaa inayoruhusiwa:
12. KADI ZA UANACHAMA
Klabu zinaruhusiwa kubuni na kutengeneza wenyewe kadi za uanachama kwenye eneo lao, tagi za jina, na vinginevyo, ikiwa tu:
- Muundo unafuata Mwongozo wa Chapa.
- Jina la klabu na/au nembo ya klabu lazima iwepo.
- Muundo lazima uwe wazi ambao unawakilisha uanachama wa klabu.
- Muundo hautakiwi kupendekeza kuwa ni kadi rasmi ya uanachama wa Agora Speakers International.
Inaruhusiwa |
Hairuhusiwi |
|
|
Jina lingine la kurasa: chapa_mwongozo