Zifuatazo ni kanuni za msingi ambazo Shirika na klabu zote za Agora Speakers zinafuata.
Klabu haziwezi kuwatenga wanachama kwasababu ya asili, rangi, dini, mwelekeo wa kimwili, utambulisho wa jinsia au uonyeshaji jinsia, umri, kiwango cha kipato, utaifa, kabila, au ulemavu wa kiakili au kimwili, ili mradi mwanachama, kupitia juhudi zake binafsi, aweze kushiriki mipango yote ya kielimu ya Shirika.
Pale ikiombwa, na kulingana na kesi tofauti, Agora Speakers International inaweza kutoa ruhusa ya kuunda klabu ambayo haifuati kanuni hii ili kuendana na sheria za eneo hilo au masuala maalum (kwa mfano, kama vile klabu ya gereza) kulinda walio wachache au sababu zingine. Ruhusa inaweza kutenguliwa muda wowote.
Hamna ubaguzi haimaanishi kuwa kila mtu ana haki ya kuingia kwenye klabu yoyote ambayo anataka. Ubaguzi unatokea tu pale ambapo kuna sera ya kimfumo (kwa dhahiri au bila kupingika) ambazo zinazuia kundi fulani la watu kujiunga. Klabu zina uhuru wa kukataa wanachama - kwa misingi binafsi au kwa kila kesi - watu ambao wanadhani kuwa wana matatizo au hawatochangia kitu chanya kwenye klabu.
Ada za klabu – ikiwemo ni mara ngapi na gharama gani – ni maamuzi ya klabu.
Fedha zinazokusanywa na klabu - bila kujali chanzo chake - zinatakiwa kutumiwa tu kwenye uendeshaji wa ujumla wa klabu na sio manufaa binafsi ya kiuchumi. Kama klabu inatoza ada, kuna masharti maalum kuhusu matumizi sahihi ya fedha na uwazi wa kifedha ambao klabu inahitaji kufuata.
Ada za klabu haziwezi kuwa za ubaguzi, isipokuwa kama imeelezewa kwenye masharti ya fedha za klabu.
Wanachama ndani ya klabu lazima wawe wanasaidiana, wawe na heshima, na wavumiliane, hata kama mada ya hotuba ya mzungumzaji au maoni ni ambayo watu wengi hawakubaliani nayo.
Hii inatumika haswa kwa viongozi wa vipengele tofauti vya mkutano (Kiongozi wa Mkutano, Kiongozi wa Hotuba za Papohapo, Msimamizi wa Mdahalo, nk.) na Maofisa wa Klabu.
Isipokuwa kama hotuba ipo dhidi ya Masharti ya Maudhui ya Hotuba ambayo klabu imeidhinisha kabla na imeweka wazi, viongozi wa vipengele au maofisa wa klabu hawawezi kumkataza au kumzuia kwa namna yoyote ile mzungumzaji ambaye anatoa hotuba ambayo hawakubaliani nayo au wanahisi inakwaza.
Tunahimiza kwa dhahiri kwa kila mtu kuzungumza kwa shauku na kwa ujasiri kuhusu vitu ambavyo wanavijali. Pia tunalinda kwa dhahiri ukosoaji, ucheshi, na mzaha.
Isipokuwa kwa hotuba zenye maudhui ambayo yanamlenga sana mtu kibinafsi kwa namna iliyo hasi (yanamlenga dhahiri mwanachama maalum), hakuna "haki ya kutochukizwa" ndani ya klabu za Agora au Shirika.
Pia, hakuna "haki ya kujibu" kwenye mkutano wa klabu. Kama umechukizwa sana na hotuba ya mtu, kitu ambach unaweza kufanya ni kutoa hotuba inayofuata ya kupinga ukifuata taratibu za kawaida za jukumu la klabu na ikiwa imo ndani ya mradi wa kielimu au jukumu.
Mwisho, hakuna "haki ya utendaji sawa wa mada" ndani ya klabu. Kwa mfano, kama mtu alitoa hotuba ya dakika 15 kwenye mada kwasababu huo ndio muda wa mradi na ukahisi kuchukizwa, majibu yako yatakuwa na kizuizi chochote cha muda ambao upo kwenye mradi wako wa kielimu.
Klabu za Agora haziwezi kutumiwa kutangaza ajenda zozote za kidini, kiitikadi, au kisiasa au duniani kote au kutangaza taasisi, makampuni, bidhaa, au huduma zozote. Hatupo/hatushirikiani na uharakati.
Tafadhali tambua kuwa kanuni hii inatumika na Shirika kwa ujumla na klabu zote za Agora na wawakilishi. Kwa mfano, klabu haiwezi kutangaza Ukristo. Au Ujamaa. Au Haki za Wanawake. Au Matendo dhidi ya Mabadiliko ya Tabia Nchi.
Hata hivyo, hii haitumiki na wanachama. Mwanachama binafsi, kwa kutenda au kuzungumza kwa niaba yake mwenyewe, anaweza kutetea au kutangaza chochote kile ambacho kina maana kwake. Kiuhalisia, tunawahimiza wanachama wetu kuzungumza kwa ujasiri na kuchukua msimamo kwenye vitu ambavyo vina umuhimu, bila kujali ni ipi itakuwa.
Pia, klabu zinaweza kutangaza maendeleo ya Sayansi na Teknolojia, kwasababu haya ni malengo, yasiyo na asili ya kiitkadi, na sehemu ya sheria za Shirika.
Kuandaa na Kushiriki kwenye Matukio
Swali maarufu linalohusiana na kanuni hii ni aina gani ya matukio klabu inaweza kuandaa au kushiriki.
Msingi ambao unatumika kwenye kanuni ya Kutokuwamo ni kuwa Shirika letu linataka kufikia na kusaidia watu kila sehemu, bila kujali asili na muundo wa utawala wa mahali wanapoishi. Kusiwe na shaka yoyote kuwa aidha Agora au klabu zake haziashiriki kwenye harakati za aina yoyote ile na hawana ajenda (ya kisiasa, kiitikadi, kimaadili, nk.) zaidi ya malengo yaliyotajwa kwenye sheria.
Tunaamini kuwa ni afadhali kufikia kila sehemu kuliko kuwekewa kizuizi kwasababu ya kung'ang'ania kuhutubia sababu kwa kwaya ya watu ambao wameshashawishika.
Kwa maneno mengine, bila kujali umaarufu wa sababu au wazo kwenye eneo fulani (inaweza kuwa Haki za Kibinadamu, Demokrasia, Uhuru wa Kujielezea, Mabadiliko ya Tabia Nchi, Utoaji wa Mimba, Uhuru wa Dini, nk.) klabu za Agora haziwezi kushiriki kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja kwenye kuitangaza au kuisaidia, kwasababu msaada huu unaweza kusababisha mamlaka kwenye nchi nyingine kukasirishwa na shughuli za Agora na kusababisha matatizo mazito, hata kutishiwa maisha, kwa wanachama kwenye nchi hizo.
Japokuwa haiwezekani kufafanua seti za masharti ambayo bila utata yanazungumzia suala lolote linalowezekana, hii hapa ni baadhi ya mifano ya matukio ambapo ushiriki wa klabu hauruhusiwi:
- Tukio lolote lile ambapo muandaaji mkuu ni mhusika wa tatu mwenye itikadi ya wazi (mfano: sherehe za kidini, PAC na washauri bingwa, matukio ya kutetea-maisha au kutetea-chaguo, nk.).
- Tukio lolote lenye dhamira au lengo ambalo linahusu itikadi ya wazi, ajenda, au lengo la kiharakati. Kwa mfano, tukio lolote ambalo linaomba matendo yafanyike kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi, Haki za Kibinadamu, haki za LGBTQ, nk.
- Tukio lolote ambapo waandaji walio orodheshwa (bila kujali ukubwa wa ushiriki wake) wanajihusisha na matendo ambayo yapo dhidi ya sheria, maadili, na dhamira ya Shirika la Agora Speakers Foundation - hii inajumuisha mashirika ambayo yanatangaza ubaguzi, chuki, ugomvi, sayansi isiyo ya kweli, nk.
Tena, tunasisitiza kuwa vizuizi hivi vinahusu kushiriki kwa klabu kama taasisi na muonekano wa Agora au nembo ya klabu katika tukio. Wanachama binafsi, au kundi la wanachama, wana uhuru wa kushiriki kwenye matukio yoyote ambayo wanataka ilhali hazikiuki kanuni za kawaida za tabia.
Mwisho, tafadhali tambua kuwa kanuni ya Kutokuwamo haizui Agora au klabu zake kutoa huduma (aidha ya bure au kwa gharama) kwa mhusika wa tatu, ilhali ipo wazi kabisa kuwa utendaji huu haumaanishi uidhinishi, msaada, au utetezi wa mhusika wa tatu au mawazo yao.
Wanachama wa klabu wanatakiwa kuwa na uaminifu wa weledi. Kama watafiti wa kisayansi, wanatakiwa kuwa na uwazi wa kupokea mawazo mapya, kuendelea kuchambua mitazamo yao na yale wanayoyaamini kwa umakini, na wawe tayari kuyaachilia kama ushahidi au majadiliano mapya wamewasilishwa. Hawatakiwi kushiriki kwenye mbinu za upotoshaji au udanganyifu ili kushawishi malengo yao au kuonyesha mitazamo yao. Wanatakiwa kutambua vikomo vya maarifa yao na kufanyia kazi zaidi namna ya kuvimaliza.
Kama vile hamna ubaguzi haimaanishi kuwa kila mtu ana haki ya uanachama wa klabu, uaminifu wa weledi haimaanishi kuwa kila mtazamo uwezekanao kwenye mada una haki ya usawa au muda sawa ndani ya klabu. Kwa mfano, Uaminifu wa weledi unahitaji kutambua kuwa kuna watu ambao wanaamini kuwa Dunia ni Tambarare, lakini haimaanishi kuwa nadharia ya Dunia ni Tambarare inapata nafasi sawa na maarifa ya kisayansi makuu.