Kuwa mshauri na kuwa kocha vina baadhi ya sifa sawa:

  • Vyote vinahitaji kiwango kikubwa cha kujitolea kutoka kwa mshauriwa/mteja.
  • Vyote vinazingatia kuendeleza matarajio ya baadae ya mshauriwa/mteja (tofauti na kuwa mshauri, kwa mfano, mwenye lengo la kutatua masuala yaliyopita).
  • Vyote vinahitaji kiwango kikubwa cha kushirikiana kibinafsi.
  • Vyote vinajumuisha kutoa maoni na ushauri.

Pia kuna tofauti muhimu:

  KUWA MSHAURI KUWA KOCHA
Muda Kulingana na washiriki Inategemea mafanikio
Upeo Inazingatia kujenga uhusiano wa uaminifu na mzunguko wa maendeleo Inazingatia kufanikisha lengo maalum (lakini uaminifu pia ni muhimu)
Mtazamo Inategemea na mshauriwa Inategemea na lengo la kufanikishwa
Asili ya Uhusiano Inanufaisha wote Kitaalam zaidi
Uwazi Ni kwa usiri Inaweza ikawa wazi au kwa usiri kulingana na muundo
Mwelekeo Mshauriwa anachagua Wote wanaweza kuchagua
Utaratibu Kwa kawaida sio rasmi Inatumia muundo rasmi
Mtaalam wa Mada Mshauri Mteja
Mtaalam wa Utaratibu Mshauri Kocha
Matarajio Maendeleo ya ujuzi kwa ujumla Kufanikisha kiwango cha utendaji
"Ugawaji wa Hotuba" Mshauri anazungumza zaidi kulika Mshauriwa Mteja anazungumza zaidi kuliko kocha