Je unataka kuwa Balozi?
Una uhakika? Kwanza, tafadhali soma kuhusu jukumu la Balozi ili ujue ni nini utakikuta... Kama, baada ya kuisoma, bado unataka kuwa balozi, hivi hapa ni nini unatakiwa kufanya:
Ili kuwa balozi, unahitaji:
- Kujitolea kutangaza Agora nchini kwako - maadili yetu, jamii, kanuni za msingi, na mpango wa kielimu, na kuwahimiza na kuwasaidia wengine kwenye kuanzisha klabu za Agora na kukuza jamii kwa ujumla.
- Kuanzisha na kuimarisha klabu mpya ya Agora nchini kwako. Klabu imara inaweza kukutana na kufanya Mpango wa Kielimu wa Agora bila uwepo wako au kuwaamrisha watu.
- Kutangaza Agora na klabu yako kwa umma kwenye mitandao yako ya kijamii - kutumia posti zako mwenyewe, au mikutano ya klabu, au picha (aidha kutoka klabu zako au nyingine), au kusambaza posti zetu rasmi.
- Unahitaji kuwa Rais wa Klabu kwa japo miezi kadhaa na kuifanya Klabu ya Rejea. (Klabu ya Rejea kimsingi ni klabu ambayo inafuata kwa ukaribu sana mwongozo wa Agora na ambayo inaweza kutumiwa kama muundo wa kuigwa au rejea kwa watu wengine ndani ya nchi ambao wanataka kuanzisha klabu nyingine za Agora).
- Mwisho, unahitaji kuwa na taarifa kamili kuhusu Agora, mfumo wake na mbinu zake za kielimu, masharti yako yote tofauti, na bila shaka, ni nini maana ya kuwa Balozi wa Agora, haswa kuhusu masuala ya muda na na juhudi ambazo utaelekeza kwenye Shirika.
Kama unafikiri upo tayari kuwa Balozi, pale utakapokuwa umetimiza vigezo vya hapo juu, tutumie ujumbe kwenda [email protected] ukielezea kuwa unataka kuwa balozi.
Jukumu la ubalozi linaweza likafanywa na watu kadhaa na ni jukumu la kujitolea ambalo unachaguliwa na Bodi. Haswa kwenye nchi kubwa, kunaweza kuwa na Mabalozi kadhaa kwenye maeneo tofauti.
Muda wa jukumu hili ni mpaka shirika liwe na uwepo wa kutosha na klabu ndani ya nchi ili nafasi za uongozi za kawaida ziweze kupigiwa kura, ambayo kwa kawaida inatokea pale ambapo kuna kuwa na klabu 30 na japo wanachama 300.