Mwezeshaji wa Mkutano ni jukumu la hiari la ofisa ambaye anatakiwa kuhakikisha kuwa kila kitu kipo sawa ili mkutano uende vizuri. 

Maelezo ya kina yameelezewa kwenye jukumu la Mwezeshaji wa Mkutano, na jukumu linafanana sana na lile la Sajenti wa kuhakikisha utaratibu kwenye mashirika mengine. 

Ni maamuzi ya kila klabu kama Mwezeshaji wa MKutano ni jukumu la kila mkutano ambalo mtu tofauti anafanya kila mara au ofisa wa klabu ambaye habadiliki. 

Kwasababu jukumu lina shughuli za "karaha" kama vile kuhakikisha ukumbi upo sawa kabla ya mkutano, kuusafisha baadae, nk., tunapendekeza kuwa mtu tofauti alifanye kwa kila mkutano, kuliko kuwa na ni jukumu la ofisa mmoja tu.