Isipokuwa kwa Klabu za Shirika, ambazo zinafuata masharti ya uhasibu na manunuzi ya shirika mwenyeji, klabu nyingine zote ambazo zina simamia fedha zozote (haijalishi kama zinatoka kwa ada au vyanzo vingine) wanatakiwa kuwa na mweka hazina ambaye anafanya utunzaji wa vitabu (uhasibu) wa msingi.
Mweka Hazina anatakiwa kufahamau kikamilifu Masharti ya Fedha za Klabu na ana majukumu yafuatayo:
Mlinzi wa fedha za klabu
Kama mweka hazina, wewe ni mlinzi wa fedha za klabu. Matumizi hayawezi kufanyika bila idhini ya Rais na Mweka Hazina kwa pamoja. Kwa ufanisi, una kura ya turufu ya matumizi ambayo wewe unaamini yanakiuka kile ambacho wanachama walikipigia kura kwenye bajeti kwa ujumla au masharti ya fedha za klabu.
Kama Mweka Hazina na Rais hawakubaliani kama matumizi fulani yana afiki bajeti iliyokubaliwa, wanaweza wakapeleka matumizi mbele ya wanachama wa klabu kupigiwa kura.
Kwa upande mwingine, kama kutokubaliana ni kwasababu ya kama matumizi ya fedha yanafuata masharti ya matumizi ya fedha za klabu, wanaweza wakapeleka swali kwa balozi wa nchi au makao makuu ya shirika.
Utunzaji wa Vitabu vya Fedha na Ripoti
Jukumu la pili la mweka hazina ni utunzaji wa vitabu mzuri wa mizunguko yote ya fedha. Kuna vitu viwili unahitaji kufuata:
- Sheria za eneo husika.
- Mahitaji ya Shirika ya kuripoti utunzaji wa vitabu.
Kwa kawaida, sehemu hii ya pili itakuwa ni ya rahisi sana, kwasababu mahitaji ya kuripoti ni marahisi na hayahitaji zana maalum zozote. Kwa kuongezea, unaweza ukatumia zana za mtandaoni ambazo tunatoa kwa ajili ya kuripoti.
Kiuhalisia, utunzaji wote wa vitabu unatakiwa kufanywa pale malipo yanapopokelewa au yanapotolewa ili wanachama wote wanafuatilia waweze kuona hali ya fedha za klabu. Lakini, kama hilo haliwezekani kwa sababu kadhaa, unatakiwa kuhakikisha kuwa unatakiwa kupakia taarifa za kitu hiko na taarifa za ujumla japo mara moja kila miezi sita.
Majukumu Mengine
Mwisho, kama Mweka Hazina, unahitaji pia:
- Kujibu maswali ya kifedha ya wanachama na wageni. Hakika, wanachama wana haki ya kupata taarifa za kina kuliko wageni.
- Kukusanya ada za klabu na fedha kutoka vyanzo vingine na kuziweka kwenye akaunti moja.
- Kurudishia maofisa pesa zao ambazo walitumia kwa matumizi yaliyoidhiniwa.
- Kushirikiana na waweka hazina kutoka klabu nyingine ili kuhakikisha kuwa Masharti ya Kifedha yanazingatiwa kwenye matukio ya pamoja kama vile kama makongamano au mashindano yanatakiwa kulipiwa.
- Kuthibiti na kutekeleza malipo yaliyoidhiniwa na Rais kwa ajili ya manunuzi ya bidhaa na huduma.