Msimamizi wa Jamii ana jukumu la uwepo wa klabu mtandaoni na kwenye mitandao ya jamii.

Kutengeneza uwepo imara mtandaoni

Uwepo imara wa klabu mtandaoni ni kama sumaku ya wanachama wapya, wageni na vyombo vya habari.

Panga muda maalum kwa wiki ambao utakuwa unatumia kunaendeleza uwepo wa klabu mtandaoni. Amua muda huo kabla na uutumie ipasavyo.

Udumifu na ukawaida ni baadhi ya siri za kuwa msimamizi wa jamii mwenye mafanikio. Jaribu kuposti japo mara moja kwa wiki.

 

Vitu vya kuposti

Haya ni baadhi ya mawazo ya nini cha kuposti:      

  • Bila shaka ... mikutano na matangazo mengine ya matukio
  • Kukaribisha wanachama wapya
  • Kusambaza posti kutoka kwa klabu zingine au Agora Speakers International.
  • Kutambua mafanikio ya wanachama - ya kutoka mpango wa kielimu wa Agora na mafanikio ya nje pia. Kwa hii ya pili, mafanikio hayo yanatakiwa kuwa yanaendana na dhima ya klabu. Kama mwanachama akichapisha kitabu au akitoa hotuba ya msingi (kuu) kwenye kongamano - hii itakuwa ni mifano mizuri. 
Hamna kitu chenye nguvu kama kuona jina la mtu limechapishwa na kuwahimiza wengine kutafuta utambuzi kama huo.
  • Rekodi za mikutano
  • Weka mifano ya hotuba ambazo umezipenda
  • Chati za maendeleo ya lugha, vidokezo, na mchezo wa meneno ambao utakubaliwa vizuri, haswa kama inaongeza msamiati ya wanachama.

  • Muhtasari wa mikutano kwa wale ambao hawakuhudhuria.

Hauhitaji kufanya kila kitu mwenyewe - Wahimize wanachama kupendekeza mawazo na mada.

Kumbuka kuwa kama Msimamizi wa Jamii, utakapoposti maudhui, haufanyi hivyo kama posti yako binafsi lakini kwa niaba ya klabu. Kwahiyo, unahitaji kuzingatia kanuni ya Kutokuwamo.
Hauhitaji kuweka maudhui mapya kwenye majukwaa yote mara zote. Makala ambayo iliwekwa Facebook miezi sita iliyopita inaweza ikatumika tena wiki hii kwenye Twitter.

 

Vidokezo vya Muhimu vya Kuposti

 

Hivi ni baadhi ya vidokezo muhimu ambavyo unatakiwa kuzingatia:    

  • Kutumia "hashtags".  Tumia mchanganyiko wa hashtags za Agora (#AgoraSpeakers, #ZungumzaOngozaWekaHistoria, nk.), pamoja na tagi za klabu yenu, na tagi zinazofaa baadae.
     
  • "Tag" au wataje (@) watu wanaopendwa kwenye posti za klabu za mitandao ya kijamii -  (Shughuli hii inatakiwa kuratibiwa pamoja na Makamu wa Rais wa Masoko). Kutag watu ambao wanaweza kuvutiwa (vyombo vya habari, viongozi, watu mashuhuri, wanachama watarajiwa, nk) kwenye posti zinazovutia ni njia nzuri yakupata umakini wao, lakini inatakiwa kufanywa kiuangalifu.
     
  • Fuatilia makundi ambayo unaweza ukatoa majibu yenye maana.  Kuna makundi mengi ambayo watu wanauliza maswali ya aina yote ambayo wewe unaweza kujibu - makundi ya kukutana, makundi ya Facebook, Quora, Reddit, nk.  Kwa kawaida, unatakiwa kufuatilia seti za mada kama:
    • Uzungumzaji wa mbele ya hadhira
    • Midahalo
    • Umakinifu
    • Uwoga wa kwenye jukwaa
    • Kuzungumza kitaalam
    • Uwasilishaji wa mauzo
    • Uongozi
    • Maendeleo ya kazi
    • Kujiendeleza
    • Kujiamini
    • ... kwa ujumla, ujuzi wowote ambao tunatoa 

  • Pale utakapoona maoni au posti inayovutia ambayo unaweza kuongezea kitu, andika majibu. Kwa kawaida, jibu linatakiwa kuwa la maana na litoe ufahamu na maudhui kidogo, utatakiwa kuwa na "hashtag" chache za kutangaza, hata kiunganishi cha klabu.

Usimamizi wa Maudhui na Masharti ya Makundi

Kama Msimamizi wa Jamii, una jukumu pia la mazingira, ustaarabu, na uangalifu wa makundi ambayo wanachama au wageni wanaweza kuposti maoni. Baadhi ya kanuni za Agora zinatakiwa kuzingatiwa kwenye makundi yote:               

  • Hotuba/maneo ya chuki ya aina yoyote hayaruhusiwi.
  • Utangazaji wa mada ambazo zipo dhidi ya sheria (ikiwemo sayansi ya uongo) hairuhusiwi.

Ukiachana na hizo, una uhuru wa kuamua vipengele kwa ujumla vya uwepo wa klabu mtandaoni:

  • Je utaruhusu wageni na wanaozuru kuposti?
  • Je utakubali posti za kibiashara? Zipi hizo?
  • Je ni mada zipi zinazingatiwa kuwa sahihi?

 

Kufanyia kazi Maoni

Kama Msimamiz wa Jamii, sehemu ya majukumu yako ni kufanyia kazi maoni kwa ujumla na maswali kutoka vyanzo tofauti.

  • Anza kwa kumshukuru mtu aliyeandika, hata kama ni ukosoaji mkali sana.
  • Jaribu kujibu maombi yote ndani ya muda usiozidi siku moja.
  • Hata kama utoaji wa taarifa au kufanyia kazi ombi maalum litachukua muda, andika jibu fupi kuwa utamrudia huyo mtu na jaribu kutoa makadirio. Kwa mfano, "Nafikiri zipo klabu kama 200 duniani tayari, lakini acha nipate idadi kamili, na nitakurudia."
  • Kama swali ni kuhusu Agora na jinsi tunavyofanya kazi, kama haujui jibu, waulize maofisa wenzako wa klabu na sisi ([email protected]) ili tuweze kukusaidia.
  • Haijalishi maoni ni ya hasi kiasi gani, jaribu kulitumia kama nafasi ya kujifunza.
  • Kamwe usianzishe majibishano na mtu. Hautakuwa tu unachochote moto, lakini pia unamfanya aliyeposti kupata wafuasi zaidi. Hapa unaweza kuona baadhi ya mifano ya kushughulikia maoni hasi kiufasaha.
Please note that Feedback and questions may come not only directly (kama ujumbe au barua pepe kwa klabu) lakini pia kwa njia nyingine nyingi, kama vile kama posti kwenye kundi, maoni, kutajwa kwa klabu (@) kwenye posti au akaunti ya mtu binafsi, nk.
Jaribu kufuatilia vyanzo vyote hivi ili uhakikishe kuwa hamna swali au maoni ambayo hayajibiwi.

 

Ukumbusho wa faragha

Faragha ni kitu cha muhimu sana katika dunia ya leo, na lazima uwe makini ili kuepuka kukiuka bila kukusudia haki za watu za kusimamia taarifa zao wenyewe. Kushindwa kufanya hivyo inaweza kuleta nia mbaya, na pia unaweza kupoteza mwanachama, kupata maoni mabaya kuhusu kile klabu kimeposti, na hata matatizo ya kisheria kwenye maeneo kama vile Umoja wa Ulaya. 

  • Kamwe usitumie mifumo ya mawasiliano ya makundi ambayo yanaweka taarifa za faragha za mtu kuwa wazi. Kwa mfano, kuunda kundi la WhatsApp linaonyesha namba za simu za kila mtu kwa watu wote.
     
  • Pale utakapoulizwa taarifa za mawasiliano, daima muombe anayehusika ruhusa, au pindua mtiririko wa taarifa.
    Kwa mfano, fikiria umepata ombi lifuatalo:

    "Habari. Sisi ni Shirika la SpeakersOfTomorrow. Nataka kuwasiliana na Rais wa Klabu John Doe, kwasababu tunatafuta wazungumzaji wa msingi kwa ajili ya mkutano wetu na tungependa kujadiliana naye kiundani. Naweza kumpata kwenye namba gani?"

    Badala ya kutoa hapo hapo namba ya mtu mwingine, unatakiwa

    1) Muulize rais kwanza, alafu toa taarifa au mawasiliano kama amekubali
    2) Geuza mtitiriko wa mawasiliano: "Asante sana kwa ombi lako. Nitamwambia Joe akupigie. Anawezaje kukupata, na ni muda gani utafaa zaidi?".