Motisha
Makamu wa Rais wa Uongozi wa Jamii ni jukumu jipya la uofisa kwenye klabu za Agora.
Tangu Agora Speakers International inaanzishwa, moja ya malengo haikuwa tu kuunda mazingira rafiki ya klabu ambapo wanachama wanaweza kusoma na kujifunza uzungumzaji wa mbele ya hadhira na maarifa ya uongozi lakini pia kuwapatia fursa za kuzungumza na uongozi nje ya mazingira ya klabu. Zaidi ya hayo, moja ya malengo ya Agora ilikuwa ni kuwaruhusu wanachama kuwa na matokeo mazuri kwenye jamii zao wakati wa mchakato wenyewe wa kujifunza kupita uongozi wa miradi iliyopo kwenye maeneo yao ambayo yanaleta mabadiliko kwa watu.
Tunatakiwa pia kutofautisha "Uongozi" kutoka "Usimamizi". Wakati usimamizi unaweza kufundishwa kwa kiwango fulani kwa kusimamia timu ndogo ya watu, klabu, au tukio la ngazi ya juu la Agora, Uongozi unahitaji maarifa makubwa kabisa na ya tofauti. Kamwe haiwezi kufundishwa ndani ya vizuizi vya shirika lenye muundo wake.
Wakati tunajitahidi kufika duniani pote – aidha nchi au duniani - kupitia kushirikiana na taasisi tofauti (kibiashara, kiserikali, kielimu, nk.) na kuongeza kwa shirika letu, kuna mengi ambayo yanaweza kufanyika katika ngazi ya kidunia. Kwa kweli, pengine fursa nyingi zitakuwa kwenye matukio ya eneo husika - maonyesho, mikutano, mikutano ya makundi yenye kupenda vitu sawa, nk.
Kuhusu suala la uongozi, tunapitia changamoto sawa – fursa nyingi za kusaidia zitakuwa kutoka kwenye eneo lenu mliopo, kwa kiwango kidogo, kukabiliana na matatizo maalum.
Jukumu la Makamu wa Rais wa Uongozi wa Jamii
Makamu wa Rais wa Uongozi wa Jamii (VPCL) ni jukumu ambalo linahitajika kwenye klabu zote na ana kazi ya kuweka kati kazi zote za uongozi wa jamii na miradi.
Kama VPCL, wewe:
- Unakuwa kama pointi moja ya mawasiliano kati ya klabu na mashirika ya nje yanayotaka kushirikiana, ikiwemo mamlaka za maeneo yako.
- Una jukumu la kutafuta fursa au nafasi za kuzungumza, kuongoza, na kujitolea kwa wanachama.
- Una jukumu, pamoja na VP wa Elimu, ya kutambua wanachama wapi wanastahiki fursa tofauti za kuzungumza, kutegemea na ujuzi na maendeleo kupitia Mpango wa Kielimu na muda ambao wanajitolea kwenye klabu na wanavyojishughulisha na klabu.
- Una jukumu la kuratibu shughuli za klabu pamoja na klabu nyingine za Agora kwenye eneo fulani.
- Una jukumu la kuidhinisha mapendekezo ya miradi ya uongozi ya wanachama, ikiwemo kutathmini kama upeo wa mradi unafaa (isiwe kubwa sana au ndogo sana) ukizingatia ujuzi wa uongozi wa mwanachama maalum.
- Pendekeza na idhinisha ushiriki wa mwanachama kwenye miradi ya uongozi ambayo ipo.
Na kama majukumu yote ya maofisa wa klabu, isipokuwa Rais wa Klabu, zaidi ya mtu mmoja anaweza kuwa VPCL kama juhudi na muda unahitaji, na wanaweza wakapata msaada kutoka wanachama wengine kwenye kazi maalum. Pia, mtu anaweza akawa na nafasi zote mbili za VPCL na ofisa mwingine kwenye klabu ndogo.
VPCL anatakiwa kuratibu na maVPCL wa klabu nyingine kwenye eneo husika ili kuzuia juhudi zisitumike mara mbili. MaVPCL wa klabu zote kwenye eneo husika wanatakiwa kushirikiana na kamwe wasiwe kwenye mashindano ya "nani anapata hiki au mradi gani au fursa ya kuzungumza". Taarifa kuhusu chaguo zilizopo zinatakiwa kusambazwa kwa wote, na maVPCL waliobaki wanatakiwa kuwasaidia maVPCL ambao wana shida ya kutafuta uongozi wa jamii au fursa za kuzungumza kwenye eneo. Kiukweli, lengo kubwa ni kutengeneza hifadhidata ya duniani kote ya fursa ambayo imetengenezwa na maVPCL ambayo wanachama wanaweza kuchagua.
Fursa za Nje za Uzungumzaji wa Mbele ya Hadhira
Wanachama ambao watakuwa wamemaliza vipande viwili vya kwanza vya Mpango wa Kielimu wa Msingi ("Miradi ya Tatu ya Kwanza" na "Misingi ya Kuzungumza") wanastahiki fursa za kuzungumza mbele ya hadhira za nje.
Miongozo na mapendekezo ya jinsi ya kutafuta na/au kuunda fursa za nje za kuzungumza mbele ya hadhira zitachapishwa pale ambapo maoni na mapendekezo ya jukumu hili yatakapopokelewa. Kwa ujumla, hii itajumuisha:
- Mhadhara na warsha kwenye mashule, vyuo vikuu, na makundi ya harakati za jamii
- Matukio ya wazi yaliyopangawa na klabu
- Mashirika mengine ya uzungumzaji wa mbele ya hadhira
- Mikutano na maonyesho
- Channeli na podikasti za klabu/Agora
- Makundi ya kimtandao ya biashara na matukio
- Matukio ya kijamii (harusi, sherehe, nk.)
Vigezo vya Kushiriki
Kukiwa na fursa za ushiriki wa nje, uangalifu wa ziada lazima uchukuliwe ambao unalingana na kanuni na dhamira za Shirika. Hasa, yafuatayo lazima yaangaliwe:
- Ushiriki wa nje lazima utolewe kwa wanachama wote wa klabu kwa njia isiyo ya ubaguzi. Kwa mfano, Klabu za Agora haziwezi kujihusisha na mashirika au matukio ambayo yanataka wazungumzaji kulingana na vigezo vya kibaguzi ("Tunatafuta wanaume wazungu wakuzungumza kwenye tukio", "Tunatafuta Mkristo wakuzungumza kwenye tukio la kanisa").
- Ushiriki wowote ni wa hiari kwa wanachama wote wa klabu.
- Ushiriki wowote unafanywa kwa msingi binafsi (na kamwe sio kama mwakilishi wa klabu, wala mwakilishi wa Agora Speakers International).
- Ushiriki huu haumaanishi kuwa ni ubia wa kudumu au ushirikiano kati ya klabu na shirika la wahusika wa tatu.
Mara nyingine, ushiriki huu utakuwa unatokea mara kwa mara na kuhitaji ulinganifu (kwa mfano, wanachama wa klabu ya Agora wanazungumza katika eneo X, na kwa kubadilishana, wanachama wa X wazungumze kwenye klabu ya Agora). Kwenye suala hilo, tafadhali jua kuwa:
- Huu ushirika wa kawaida wa nje kwenye mikutano ya klabu ya Agora lazima uidhiniwe na wanachama waliowengi wa klabu, na idhini hiyo ni ya mwaka mzima. Idhini hii inaweza kubatilishwa muda wowote na wanachama wa klabu waliowengi.
- Hakuwezi kuwa na ubaguzi kati ya wageni (mgeni ni mtu asiye mwanachama wa Agora anayehudhuria kwa njia yoyote - kwa uso kwa uso au kwa sibayana - mkutano wa klabu wa Agora).
- Wageni wote wanatakiwa kufanya majukumu sawa bila kujali ni wapi wametoka na historia yao, na majukumu yao yanatakiwa yalingane na taarifa za uandikishaji wa klabu.
- Ushiriki wote wa nje wanatakiwa kufuata mwongozo wa kielimu wa Agora. Hasa, ushiriki wote una kizuizi cha muda, unafuatiliwa na mwanasarufi, unatakiwa kuwa na seti ya malengo yanayojulikana kabla, na kutathminiwa kulingana na miongozo ya utathmini ya Agora.
- Ushiriki wa nje hautakiwi kuwa na mabadiliko yoyote kwenye uendeshaji wa kawaida wa mikutano, muundo wa mkutano, au majukumu maalum ambayo yametolewa. Kwa mfano, mshiriki wa nje hatakiwi kutaka kuwa wa kwanza kuzungumza au kuwa mtu, hasa, amtathmini.
- Kiongozi wa shughuli ya mkutano na mtathmini wake hawawezi kuwa wa nje ya klabu. Kwa maneno mengine, na maalum kwa ajili ya hotuba zilizoandaliwa - aidha mzungumzaji au mtathmini lazima awe mwanachama wa klabu.
- Ushiriki huu wa nje hautakiwi kukiuka Kanuni za Msingi zozote zile. Hasa, hakutakiwi kuwa na ushiriki wa nje kutoka mashirika ambayo yanatanganza mitazamo ya kidunia ya kisiasa, kiitikadi, au kimaadili, na ushiriki huu hautakiwi kutangaza mashirika ya wahusika wa tatu, huduma, au bidhaa. Ushiriki wa mashirika ambayo yanatangaza mitazamo ya sayansi isiyo ya kweli hayaruhusiwi.
- Idadi ya ushiriki wa nje kwa mwaka lazima uzuiliwe na idadi ambayo imewekwa kwenye orodha ya Mahitaji ya Uendeshaji wa Klabu (inategemea na aina ya klabu).
Unatakiwa kudhania uwepo wa uzungumzaji wa nje kama zawadi na fursa kwa wanachama. Isipokuwa kama unajua kwa uwazi kuwa kuna bajeti ambayo imewekwa pembeni kwa ajili ya wazungumzaji, usijaribu au kutaka kujadiliana kuhusu ada kwa niaba ya klabu au mwanachama.
Fursa za Nje za Uongozi
VPCL pia ana jukumu la kutafuta fursa za uongozi kwa ajili ya wanachama. Kipindi hiki kitaendelezwa kwa kikamili katika hatua ya baadae, pamoja na chapisho la Njia ya Uongozi na miongozo ya Miradi ya Jamii.