Kama Makamu wa Rais wa Uanachama, una mielekeo miwili ya msingi ya kazi: 

  • Kuhakikisha wanachama wa klabu wanajaliwa
  • Kuhakikisha ukuaji wa klabu.

 

Haya hapa ni majukumu yako makuu. 

Kuongeza uanachama

Kazi hii inafanikishwa kwa pamoja na Makamu wa Rais wa Masoko na Msimamizi wa Jamii (kama yupo).

Japokuwa utakuwa unategemea sana matendo yao, kuna vitu vingine vichache ambavyo unaweza kufanya mwenyewe:

  •  "Mlete rafiki" -  Panga vipindi vya "mlete rafiki" ambapo kila anayehudhuria anatakiwa kuleta rafiki mmoja ambaye anaweza akavutiwa na klabu.
     
  • Mashindano ya kujenga uanachama kati ya wanachama wa klabu na toa tuzo kwa watu ambao wataleta wageni wengi.
     
  • Andaa mikutano ya "milango wazi" kwa ajili ya umma na kampeni zingine za kujenga uanachama.
     
  • Shiriki kwenye matukio mengine ya kijamii yanayohusiana na uzungumzaji wa mbele ya hadhira, na zungumzia kuhusu Agora na klabu yako - angalia tovuti za matukio kama vile Meetup.com, Internations,  Airbnb, Couchsurfing, nk.
     
  • Tangaza na andaa midahalo ya umma kuhusu mada za moto moto za sasa (pamoja na VP wa Elimu)

Kama klabu haina VP wa Masoko, basi majukumu haya yatakuwa ya kwako.

Andaa Shughuli za Pamoja

Wakati mikutano yote ya Agora inahitaji kufuata lengo maalum la kielimu na uandaaji wa kawaida, hii haimaanishi kuwa hivi ni vitu pekee ambavyo unaweza kuandaa.

Hii hapa ni baadhi ya mifano ya mawazo ya jinsi ya kuimarisha kipengele cha kijamii cha klabu: 

  • Safari na matembezi
  • Sherehe za kusherekea likizo tofauti
  • Likizo za "Uzungumzaji wa Mbele ya Hadhira", ikiwezekana kuwe na mzungumzaji mgeni maalum anayehudhuria
  • Usiku wenye dhamira maalum
  • Miradi ya jamii ya muda mfupi
Kwasababu shughuli hizi zinaandaliwa kwenye jukumu lako kama VPM na kwa kutumia orodha ya klabu ya uanachama, hawawezi kujishughulisha na shughuli ambazo zinakiuka Kanuni za Msingi au Sheria za Shiriika.

Kwa mfano, kuandaa likizo ya wanachama ili kujua zaidi kuhusu Kuponya kwa Tantric (kipengele cha sayansi isiyo ya kweli) au kuandaa likizo ya mandhari maalum za hotuba za utetezi wa Haki za Binadamu hazikubaliwi.

Ukiandaa matukio hayo, hakikisha kuwa unachukua Bango la Klabu ili kumsaidia VP wa Masoko kwa kutengeneza nyenzo tele:

 

 

Kuhakikisha wageni wanapokelewa na kuhudumiwa vizuri

Kama VPM, kazi yako moja ya msingi ni kuhakikisha kuwa wageni na wanaozuru mikutano wanahisi wamekaribishwa, wamepewa msaada, na wanataka kujiunga. Hii ni muhimu sana mpaka tuna makala tofauti inayoelezea jinsi ya kuwahudumia wageni vizuri.

Kama huwezi kuwahudumia wageni binafsi, hakikisha kuwa unampa jukumu na maelezo ya kikamilifu mtu mwingine ambaye anaweza kufanya hivyo wakati haupo au hauwezi.

Daima waalike wageni kujiunga na klabu, au japo kujiunga na orodha ya barua pepe ya klabu.

Usilazimishe sana - kila mtu anahitaji kupitia njia yao binafsi ya kiakili kufikia maamuzi. Ukiendelea kulazimisha, unaweza usifanikiwe.
Hakikisha kuwaambia kuwa wana uhuru wa kuja mara nyingi watakavyo, lakini kufurahia faida zote kikamilifu (kama vile kuwa na uwezo wa kufikia nyenzo za kielimu au kuwasilisha hotuba nzima), watatakiwa kujiunga.

Katika kila mkutano, hakikisha kuwa vifurushi vya kuwakaribisha wageni vipo. Pia, jiandae kujibu maswali yoyote ambayo watakuwa nayo baada ya mkutano, na kuwa tayari kuwasaidia kama hawana uhakika na mlolongo wa kujiandikisha.

Kwa kawaida, ni bora zaidi kuzingatia manufaa ya kuwa mwanachama wa klabu, na ujuzi wote ambao watu watajifunza, na mitandao ambao watajenga kuliko kusisitiza kuwa klabu ni bure au ina ada ndogo sana. 

Watu wengi sana wanahusisha "bure" na kuwa "ubora mbaya".  Pia, mara nyingi sana, watu hawawezi kuamini kuwa kitu ni cha bure kweli au gharama ndogo bila kufikiria kuwa kuna mtego au nia mbaya sehemu - msemo wa kawaida "kama haulipii bidhaa, basi wewe ndio bidhaa."

Kama utakutana na kipangamizi hiki au ukihisi hili litakuwa tatizo, una baadhi ya mifano bora zaidi ya kuonyesha hili:
 
  • Wikipedia ni ensaiklopidia bora zaidi duniani, na ni bure.
  • Mozilla Firefox ni moja ya kivinjari bora zaidi, na  ni bure.
  • Linux ni moja ya mfumo wa uendeshaji mzuri zaidi, na ni bure. 
  • Vyuo vikuu vya juu vya duniani - MIT, Stanford, nk. wanachapisha kozi zao nyingi bure (MIT Open Courseware, Stanford Free Courses, nk.).
  • Tovuti bora za kielimu za bure, kama vile Coursera au Khan Academy.
  • Shirika la Programu la Apache limetengeneza bidhaa za ubora wa hali ya juu za wazi mara nyingi sana ambazo ni za bure na zinaendesha makampuni makubwa duniani.
  • Na kuna programu nyingi sana za wazi na bure kabisa - kutoka kuhariri video mpaka michezo. 
  Wazo kuu hapa ni kuwa kuna vitu vingi vya bure kwasababu ni kazi zilizotengenezwa na watu wengi kwa shauku na mapenzi, na sio zinazoendeshwa kwa maslahi.

 

Kuwa na kitabu cha wageni na kuwafuatilia

Moja kati ya fursa inayokoswa ni kutokupata taarifa za mawasiliano za wageni, na kuwafuatilia. 

Sio kila mtu yupo tayari kujiandikisha hapo hapo baada ya mkutano wa kwanza. Baadhi ya watu wanahitaji kukumbushwa polepole na kiasi kidogo cha kusukumwa.

Waulize wageni kuhusu majina yao na barua pepe zao mwanzoni mwa mkutano, kuliko kusubiri mwishoni. Vinginevyo, unaweza ukapoteza wale ambao wanaondoka mapema au kwa haraka.

Pia, jaribu kuuliza taarifa za ziada zaidi ya jina na barua pepe, na labda wapi walijifunza kuhusu klabu. Kila taarifa ya ziada unayouliza itaongeza ukinzani wa kutoa chochote.

Mara utakapokuwa na taarifa za mgeni, hakikisha kuwa unawapa taarifa za mikutano mipya. Usiwasukume kujiunga na klabu - weka njia nyepesi na ya wazi ya mawasiliano kwa kuwatumia mialiko ya mikutano, makala zinazovutia mara kwa mara, nk.

 

Kuwajali wanachama

Ni mara nyingi sana unakuta VPM anazingatia sana kwenye kupata wanachama wapya na kusahau kuwajali ambao tayari wapo. Hili haliishagi vizuri.

  • Ongea mara kwa mara na VPE ili kuhakikisha kuwa wanachama wanaendelea kwenye njia yao ya kielimu. Kama mtu hafanyi hivyo, wanaweza kuwa na masuala ambayo yanahitaji kuzungumziwa.
     
  • Jaribu kuongea mara kwa mara kwa faragha na wanachama wote kuwauliza wanajisikiaje, kama klabu inawapa kile wanachokihitaji, kama wanakua kibinafsi na kitaalamu, na kama kuna masuala yoyote wangependa kuzungumzia.
     
  • Andaa warsha ya ndani ya klabu na mada za Agora, ukielezea jinsi Agora inafanya kazi, majukumu tofauti, ni jinsi gani wanachama wanaweza kupata zaidi kutoka klabu, nk.