Kama Makamu wa Rais, Masoko, una kazi ya kuunda na kutekeleza sera za masoko na vyombo vya habari za klabu ili kuongeza nguzu ya klabu, uanachama wake, na fursa za uzungumzaji na uongozi wa wanachama nje ya klabu.
Tengeneza bajeti ya masoko na mpango wa masoko
Unaweza ukafanya vitu vingi kutangaza klabu, lakini daima, kuna muda mdogo, fedha pia ni ndogo pia (au hata hazipo kabisa), na unahitaji kuamua ni nini utazingatia zaidi.
Bila shaka, "nini cha kuzingatia" itategemea na nini unachotaka kufanikisha na jinsi zilivyolingana au zinavyofaa kwa kila shughuli kuelekea malengo yote. Ni muhimu pia kuwa usiendelee kubadilisha malengo. Kama utakuwa unabadilisha njia ya malengo kila mara, utakuwa tu unafanya mizunguko mingi, lakini katika duara, na mwishoni, utakuwa pale pale ulipoanza.
Hii ni baadhi ya miongozo ya kiuhalisia ya jinsi ya kuunda mpango wa masoko:
1. Soma nakala hii na mawazo yote kwa kikamilifu.
2. Andika ni wapi klabu ipo sasa na masuala gani ni changamoto kwa klabu. Kwa mfano:
Tunapata mgeni mmoja au wawili kila baada ya wiki chache - hii inaumiza ukuaji wa klabu na inapunguza utajiri wa mikutano.
3. Weka seti ya malengo ambayo yanapimika (angalia nakala maalum ya malengo ya "SMART"). Kwa mfano, haya yanaweza kuwa malengo hayo:
1. Ningependa kuongeza mzunguko mwishoni mwa muhula kuwa wageni wapya 6 kwa kila mkutano wa wiki.
2. Ningependa kuongeza ufahamu wa klabu yetu kwenye jamii ili japo watu wawili (2) kati ya 30 ambao watakaoulizwa bila mpangilio mtaani wawe wanatujua.
Hakikisha kuwa kila lengo lina vipaombele maalum au umuhimu. Kama ungechagua kati ya kufanikisha lengo (1) na lengo (2) hapo juu, ni lipi moja ungechagua?
4. Badilishana mawazo na maofisa wenzako na wanachama wa klabu kuhusu mawazo mengine ya kimasoko ambayo wanaweza kuwa nayo ya jinsi seti ya malengo ya hapo juu yanaweza kufanikishwa.
Shughuli zako za kimasoko hazitokuwa zinafanyika pekee yake tu. Utakuwa unapigania umakini wa watu dhidi ya mashirika mengine ya kibiashara na yasiyo ya kibiashara au dhidi ya shughule nyingine. "
Kwanini niende kwenye klabu badala ya kwenda kuangalia filamu nyingine, au badala ya kwenda sinema au darasa la yoga"?
Moja ya shughuli muhimu ambazo unahitaji kufanya katika kipindi hiki ni
kuweka alama teule ya mshindani. Hii inaamnisha:
- Kutambua, kwa kila moja ya malengo, ni nani unashindana nae.
- Kutambua ni jinsi mshindani anapata umakini wa umma uliolengwa na hoja gani wanatumia
- Ni aina gani ya matangazo wanatumia
- Ni kwa ufanisi gani wanafanikisha lengo hilo
Tafadhali weka akilini ufanisi wa baadhi ya mawazi na matendo yanategemea sana eneo. Kwa mfano, makundi ya meetup.com yanafanya kazi vizuri sana Madrid, lakini vibaya sana kwenye baadhi ya nchi nyingine. Matangazo ya Facebook yanafanya kazi vizuri sana barani Asia na Afrika, sio sana Ulaya, na vibaya sana nchini Urusi, ambapo mitandao ya kijamii kama vk.com au Instagram zimetawala zaidi.
5. Kadiria ni jinsi gani mawazo hayo yanalingana na malengo yako au jinsi gani unafikiria zinaweza zikakusaidia kwa kila lengo. Isipokuwa kama klabu ina hifadhi nzuri ya historia ya mipango na shughuli za masoko zilizopita, itakuwa vigumu kuweka idadi maalum ya kila shughuli na lengo - tumia baadhi ya alama kama vile "0", "+", "++", kuonyesha ni kiasi gani shughuli hiyo maalum inaweza kusaidia na lengo. Kama una bahati ya kupata shughuli za masoko zilizopita na matokeo yake, kwa vyovyote vile, tumia taarifa hizo kama pointi ya kuanzia.
Kwa mfano, kwenye matriki ifuatayo, VPM alikadiria kuwa matukio kwenye meetup.com yatasaidia sana kuleta wageni, lakini sio kwa kuifanya klabu kufahamika zaidi kwenye jamii.
Matriki ya masoko |
---|
Shughuli ya Masoko |
|
Kuongeza wageni kufikia 6/mkutano (Umuhimu: 4) |
Kuongeza ufahamu kuwa 2 kati ya 30
(Umuhimu: 1) |
---|
1. Kushiriki kwenye Marathoni za Agora |
|
0 |
0 |
2. Tangazo kwenye gazeti la eneo |
|
++ |
++ |
3. Tangazo la tukio kwenye meetup.com |
|
++ |
0 |
4. Matukio kwenye Facebook |
|
+ |
+ |
5. Kuweka klabu kwenye Ramani za Google |
|
0 |
+ |
6. Kufanya mikutano kwenye maeneo ya hadhira |
|
+ |
+ |
... |
|
|
|
6. Kwa kila shughuli, onyesha kiwango cha juhudi na fedha ambazo zinahitajika.
Matriki ya masoko |
---|
Shughuli ya Masoko |
Juhudi(saa)/
$ (mwaka) |
Kuongeza wageni kufikia 6/mkutano
(Umuhimu: 4) |
Kuongeza ufahamu kuwa 2 kati ya 30
(Umuhimu: 1) |
---|
1. Kushiriki kwenye Marathoni za Agora |
1 / 0 |
0 |
0 |
2. Tangazo kwenye gazeti la eneo |
5 / $600 |
++ |
++ |
3. Tangazo la tukio kwenye meetup.com |
2 / $150 |
++ |
0 |
4. Matukio kwenye Facebook |
1 / $100 |
+ |
+ |
5. Kuweka klabu kwenye Ramani za Google |
2 / $0 |
0 |
+ |
6. Kufanya mikutano kwenye maeneo la hadhira |
0 / 0 |
+ |
+ |
... |
|
|
|
7. Inayofuata, weka kipaombele shughuli ambazo zinaleta matokeo zaidi kuliko zile ambazo hazina.
8. Mwisho, chagua shughuli zipi utafanya, na zisambaze zote kwenye muda uliopo.
Pima matokeo yako
Hatua yoyote utakayochukua - kutoka kutuma tangazo mpaka tukio la milango wazi, daima lazima uwe na seti maalum ya malengo kabla na uyafuatilie na kupima matokeo ya shughuli. Usijiambie tu kuwa "ilienda vizuri", na kuendelea kurudia kitu ambacho ni dhahiri hakileti mabadiliko.
Tumia "Malengo ya SMART" na mbinu za kuendeleza maendeleo.
- Shughuli iligharimu kiasi gani? (sio tu kuhusiana na fedha, lakini pia muda, juhudi, na idadi ya watu waliohusika)
- Malengo maalum ya shughuli yalikuwa ni yapi?
- Kuongeza wageni kwenye klabu? - Ni wangapi zaidi ulipata?
- Kukusanya fedha? - Ni kiasi gani cha fedha kilikusanywa?
- Kuongeza kutazamwa kwa kurasa? - Mabadiliko yalikuwa yapi?
- Nk.
- Ulipata mafunzo gani? Maoni yalikuwa yapi?
- Ufanisi wa shughuli utaongezeka vipi kama utarudiwa (kama italeta maana kurudia)
Kama utarudia kampeni au kitendo, jaribu kufanya mabadiliko machache yaliyothibitiwa. Kama utabadilisha vitu kumi na ufanisi utaongezeka kwa asilimia 10 (10%), hautoweza kutambua ni kipi kati ya vitu kumi vimesababisha mabadiliko.
Zana za Msingi za Masoko
Kwenye kipengele hiki, tutaelezea zana za msingi na mawazo ambayo unaweza ukataka kutumia kwenye klabu yenu:
Pata Barua pepe ya klabu.
Moja kati ya majukumu ya kwanza kama VP wa Masoko itakuwa ni kuhakikisha kuwa klabu ina barua pepe yake yenyewe, tofauti na barua pepe yako binafasi. Vigezo vya kuingia barua pepe vinatakiwa kuwa wazi kwa maofisa wote wa klabu.
Ni maamuzi yako mwenyewe kuamua wapi itakuwepo - inaweza ikawa @gmail.com, @outlook.com, nk. Hakikisha kuwa jina la barua pepe lina jina la klabu. Kwa mfano, kama jina la klabu ni "The Silent Hills Speakers", chaguo mazuri yanaweza kuwa [email protected], [email protected], nk.
Barua pepe ambazo zinaingia ni muhimu na zinatakiwa kusomwa kila siku. Ikiwezekana - kwa kusaidiwa na maofisa wengine - jaribu kujibu maombi yote ya barua pepe siku hiyo hiyo, pale tu utakapozisoma.
Kama unaweza kupata msaada wa Msimamizi wa Jamii, litakuwa ni wazo zuri pia kuunda akaunti kwenye mitandao ya kijamii kadhaa kama vile Twitter, Instagram, Facebook, nk.
Ni afadhali kutokuwa na uwepo kwenye mtandao fulani wa kijamii kuliko kuwa na akaunti iliyotelekezwa. Usijaribu kuwa kwenye sehemu nyingi ambazo utashindwa kuhudumia baadae. Kiuhalisia, anza na mtandao wa kijamii ambao ni maarufu zaidi nchini kwako na wanachama walengwa, alafu pale itakapokuwa thabiti na inawekwa maudhui kila mara, unaweza kufungua akaunti nyingine.
Chapisha barua pepe kwenye tovuti ya klabu na mitandao ya kijamii ili mtu yoyote aweze kuwasiliana na klabu.
Tafadhali kumbuka kuwa unaweza tu kutumia nembo ya klabu yako kama avatar/picha ya akaunti kwenye akaunti hizo za mitandao ya kijamii, na sio nembo ya Agora Speakers International. Tafadhali angalia
Mwongozo wa Chapa kwa ajili ya maelezo ya kina ya matumizi ya nembo.
Kuunda bango la klabu
Kuwa na bango sio hitaji la lazima kwa Klabu za Agora. Lakini, inasaidia kuwa na moja:
- Nyenzo zote za klabu (picha na video) zitaonekana tofauti zaidi na kimasoko zaidi kama bango litakuwepo.
- Utakuwa na uwezo wa kupeleka bango la klabu kwenye mashindano na makongamano
- Kwa ajili ya wageni wa nje na makampuni, klabu zenye bango zinaonekana ni za kudumu zaidi na za kitaalam.
Bango la klabu linahitajika kuchapishwa kutumia
muundo wa kawaida, kwenye nyenzo inayodumu (kama vile plastiki ngumu au nguo), na saizi maalum (sm 76 x sm 122 au 2.5' x 4'). Unaweza ukapakuwa kiolezo kwenye
Tovuti ya Chapa yetu. Unaweza pia ukatumia
Kitengeneza Rasilimali chetu kuweza kuitengeneza kwa ajili yako bila ya kutumia programu.
Kwa kawaida, gharama za kuchapa bango hazitakiwi kuzidi $30.
Kutengeneza Nyenzo za Matangazo
Jukumu jingine la VP wa Masoko ni kutengeneza nyenzo zote muhimu za matangazo ya klabu. Hii inajumuisha kuwaongoza na kuwasaidia mpiga video na mpiga picha na majukumu ya mkutano na kukusanya, kuainisha, na kutumia nyenzo zote za vyombo vya habari (mawasiliano).
Ni lazima ufuate kanuni zote za chapa wakati wa kutengeneza nyenzo za matangazo.
- Kuunda nyenzo za matangazo.
- Kubuni na kutekeleza kampeni za matangazo na ufikivu wa shughuli za klabu (aidha kupitia mikutano ya kawaida, mikutano ya "milango wazi", au mashindano).
- Pamoja na msaada wa Makamu wa Rais wa Elimu, kupanga mikutano ya "milango wazi" kwa ajili ya hadhira ya kawaiad na kampeni nyingine za kujenga uanachama.
Kujenga maktaba ya rasilimali ya habari ya klabu
Maktaba ya rasilimali ya habari ya klabu ni zana muhimu kwa ajili ya kutangaza klabu na kutoa ushahidi wa kuwa mfumo unafanya kazi. Vifuatavyo ni vitu vya kujumuisha kwenye maktaba ya rasilimali ya klabu:
- Rekodi na picha za mikutano
- Video maalum zilizoandaliwa za "Kabla" na "Baada", zikionyesha mwanzo na maendeleo ya sasa ya baadhi ya wanachama.
- Skrinishoti au rekodi za Ushuhuda
- Skrinishoti au picha au rekodi za video za ushirikiano wa vyombo za habari.
Jenga orodha ya anuani za barua pepe na nembo
Orodha ya anuani za barua pepe ni zana muhimu sana ya kutangaza klabu na kwa kumsaidia VP wa Uongozi wa Jamii kutafuta fursa za uzungumzaji wa hadhira na uongozi kwa ajili ya wanachama wenu.
Kwa kawaida, mtoa huduma wako wa intaneti anaweza kuongeza msaada wa orodha ya anuani za barua pepe bure au kwa gharama kidogo. Kama hapana, unaweza ukatumia watoaji huduma wa mtandaoni kama vile emailDodo ambao wana chaguo la bure kwa orodha ndogo na mashirika yasiyo ya biashara (japokuwa utahitaji kuelezea sababu ya kutaka kuendesha orodha, kuelezea ni wapi umepata barua pepe, na usubiri ruhusa)
Ukumbusho kuhusu faragha
Klabu zote, bila kujali maeneo waliyopo, lazima wawe na sera za faragha ambazo zinafuata EU GDPR. Hii inamaanisha kuwa unahitaji kupata idhini ya kumuweka mtu kwenye orodha ya anuani za barua pepe, na lazima uelezee wazi ni shirika gani linakusanya taarifa hizo (hapo itakuwa klabu), jinsi unavyotegemea kutumia taarifa ulizokusanya, na kuwapa watu wote waliojumuishwa uwezo wa kuomba marekebisho ya taarifa zao na pia kuondolewa kwa ujumla kwenye orodha kama wakitak hivyo.
Hakikisha unaweka nakili ya rekodi ya idhini.
Shughuli za masoko za gharama nafuu
Haya ni baadhi ya mawazo ambayo unaweza kutumia ili kutangaza klabu:
Matukio ya Milango Wazo - Pamoja na VP wa Elimu, panga matukio ya milango wazi ambayo yatatangazwa kwenye jamii.
Warsha - Tengeneza warsha maalum kuhusu mada za hotuba na uongozi. Ni vizuri zaidi kama utaweka warsha hiyo kama sehemu ya tukio ambalo litajumuisha mkutano wa klabu baada ya warsha ili uweze kuwaalika waliohudhuria kubaki na waweze kujionea mfumo ulivyo.
Tengeneza akaunti ya bure ya Google MyBusiness - Hii itaweka klabu kwenye ramani. Hata kama mnakutano mtandaoni kwa sasa, ni sehemu nzuri ya kuonekana.
Marathoni za Agora - Kushiriki kwenye matukio ya baina ya klabu kama vile Marathoni na mashindano ya kirafiki
Kushirikiana - Tafuta mashirika mengine ambazo zina shughuli sawa (uzungumzaji wa mbele ya hadhira, uongozi, midahalo, umakinifu) na pendekeza kushirikiana
Hakikisha kuwa ni dhahiri kuwa hauungi mkono shirika unaloshirikiana nalo, kwasababu itakiuka kanuni ya Kutokuwamo.
"Tag" au "@mention" (wataje) watu wanaovutia kwenye posti za klabu kwenye mitandano ya kijamii ya klabu - (Shughuli hii inatakiwa kuratibiwa na Msimamizi wa Jamii). Kutag watu ambao wanaweza kuvutiwa (vyombo vya habari, viongozi, watu mashuhuri, wanachama watarajiwa, nk.) kwenye posti zinazovutia ni njia nzuri ya kupata umakini wao, maadam inafanywa kiangalifu.
Tengeneza bidhaa za kuvaa - Ni bei rahisi kutengeneza fulana, fulana za polo, au barakoa. Kuna hata vifaa ambavyo unaweza kutumia nyumbani ili kufanikisha hili, ukitumia mashine ya chapa ya kawaida.
Toa tuzo na vyeti za kiwango cha klabu - Wanachama kwa kawaida wanapenda kuposti mafanikio yao kwenye akaunti zao za mitandao ya kijamii.
Tangaza mikutano ya klabu kama matukio kwenye majukwaa ya kukutana mitandaoni - Kuna majukwaa mengi sana - Airbnb, Meetup, CouchSurfing, Internations, nk. Tangaza mikutano ya klabu huko na wahimize watu kujiunga. Ni wazi kwamba, unatakiwa kufanya hivyo kwenye mitandao ya kijamii ya kawaida (kwa mfano.:Facebook events)
Tengeneza Kalenda ya Google yenye ratiba ya mikutano ya klabu na isambaze kwa wote - Hii itaruhusu watu kuona kirahisi ni lini na wapi klabu inakutana na kuongeza matukio haya kwenye kalenda zao wenyewe kwa urahisi.
Acha vipeperushi ndani ya shule, vyuo vikuu, maktaba, maduka ya vitabu, vituo vya kitamaduni na jamii - Kwasababu Agora ni shirika la kielimu lisilo la kibiashara, taasisi nyingi zina tukaribisha kufanya nae kazi na kusaidia klabu za maeneo hayo.
Wasiliana na makampuni ya eneo lenu - Wasiliana kiufanisi, pamoja na VP wa Uongozi wa Jamii, na makampuni ya eneo lenu. Uzungumzaji wa hadhira wa kibiashara na mipango ya uongozi kwa kawaida inagharimu maelfu ya dola, na utakuwa unawapa mbinu zinazofanya kazi kwa pesa ndogo. Hii inaweza kuleta sio tu wanachama wapya kwenye klabu lakini pia klabu mpya ya shirika ndani ya kampuni, na pia fursa mpya kwa ajili ya wanachama: kutoka nafasi za uzungumzaji kwenye mazingira ya kitaaluma mpaka nafasi za kimtandao za kupata kazi. Kwa kawaida utataka kuongea na HR (meneja wa rasilimali watu) au idara ya mafunzo ndani ya makampuni.
Tengeneza pini na himiza wanachama kuzivaa kwenye matukio yasiyo ya klabu.
Tengeneza bidhaa - stika, vikombe, fulana. nk.
Kama klabu haina Msimamizi wa Jamii, utatakiwa kufanya baadhi ya majukumuu haya.
Unaweza pia ukatumia mawazo yote yaliyoelezewa kwenye kipengele cha "Kuanzisha klabu mpya - Uundaji wa Timu".
Unaweza ukatamani kutangaza kwenye rasilimali (makundi, majukwaa, nk.) ya mashirika mengine yaliyo sawa na Agora. Hii kwa kawaida haifanyi kazi vizuri, kwahiyo endelea kwa tahadhari. Mashirika mengi ya kidini, katika suala bora zaidi, utakuwa umepoteza muda na pesa, lakini katika suala baya zaidi, utapata kesi za kisheria.
Ukiunda mawazo ambayo yanafanya kazi vyema, tuambie ili tuweze kuyaongeza hapa na kuruhusu klabu zingine kunufaika nazo.
Hakikisha Uadilifu
Kama VP wa Masoko, ni jukumu lako kuhakikisha kuwa klabu inazingatia Mwongozo wa Chapa na Mawasiliano wa Agora. Hii inajumuisha sio tu kuwa mwangalifu na mawasiliano yako, lakini pia yale ya Msimamizi wa Jamii wa Klabu (kama yupo) na yale ya wanachama pale ambapo wanapojihusisha na shughuli za Agora za nje ya klabu kama vile kuwasilisha hotuba au warsha, wakitembelea mashirika mengine, au wakiongoza miradi ya jamii.
Kufikia Vyombo vya Habari
Kufikia vyombo vya habari vya eneo ni muhimu kwa ajili ya kuongeza uonekano/ufahamu wa klabu na shirika kwa ujumla. Kwa kuongezea, shughuli hii inasaidia kwa ukubwa sana kazi ya VP wa Uogozi wa Jamii na VP wa Uanachama:
- Ni rahisi zaidi kwa VP wa Uongozi wa Jamii kuonyesha huduma za klabu kwa mashirika ya nje kama klabu imetajwa (mara kadha) kwenye vyombo vya habari.
- Ni rahisi zaidi kwa VP wa Uanachama kuvutia wanachama wapya
Siku hizi, vyombo vya habari ni zaidi ya "vyombo vya habari vya kiasili". Vyombo vya habari inajumuisha waandishi wa habari wa kujitegemea, watu mashuhuri wa blogu/vlog, washawishi, nk.
Jinsi ya kuwafikia
- Tengeneza orodha ya mawasiliano ya vyombo vya habari, kuwa na mtazamo wa vitu wanavyopendelea au kuwavutia, ni aina gani ya hadhira au mashabiki ambao wanayo na jinsi wanvyojihushisha, nk.
- Tengeneza uhusiano na watu wa vyombo vya habari kabla haujawahitaji.
- Kuwa na thamani. Usifikirie tu kuwa ni nini unakihitaji kutoka watu hawa, lakini pia ni jinsi gani unaweza kuwasaidia kwa kuwapa vitu ambavyo hadhira yao inaweza kupendelea au kuvutiwa nayo.
- Kanuni zote za Ethos, Pathos, Logos zinatumika kwenye mawasiliano na vyombo vya habari, lakini katika suala hili, anayetakiwa kuthibitisha uaminifu, uthabiti, nk ni klabu yenyewe.
- Kulingana na yaliyosemwa hapo juu, hakikisha kura unahakiki chochote utakachotuma. Siku hizi kuna zana nyingi sana za mitandaoni ambazo zinafanya kazi nzuri sana ya kuhakiki maneno na sarufi, ni uzembe usio na sababu kutuma chochote kikiwa na makosa hayo.
- Usimtumie kila mtu habari au ujumbe mmoja. Unda ujumbe tofauti kwa kila chombo cha habari kulingana na mahitaji yao.
- Kuwa mstahimilivu lakini usichukize au usisumbue. Usikate tamaa kama hautopata matokeo ukijaribu mara ya kwanza.