Makamu wa Rais, Elimu (VPE) ana jukumu la shughuli za kielimu za klabu na ana shughuli nyingi tofauti na majukumuu ambayo yana athari za moja kwa moja mikutano ya klabu.
Kwa klabu kubwa, inafaa kuwa na VP wa Elimu zaidi ya mmoja.
Panga Mwaka wa Elimu
Kuna shughuli za kielimu nyingi, nyingi ambazo zimeelezewa kwenye Mpango wa Kielimu wa Agora, na orodha inaendelea kuongezeka. Haviwezi kufanywa vyote kwenye mkutano mmoja. Na ni rahisi pia kuzoea seti za shughuli za kawaida na kutokujaribu zingine ambazo zinaweza zikawa za kielimu zaidi na za kusisimua zaidi. Matokeo yake ni mikutano ambayo inajirudia, inaboa, na haivutii sana kwa wanachama wakonge.
Kwenye nafasi yako ya VPE, una kazi ya kupanga Mwaka wa Kielimu - kuamua ni shughuli gani unataka kuwa nazo na ngapi. Ili kufanya hivyo, unahitaji kufahamu kwa kina shughuli zote, muda ambao kila shughuli unachukua, na maandalizi yake yana gharama gani.
Tafadhali kumbuka kuna kiwango fulani cha chini kinachotakiwa kufanywa, na baadhi ya majukumu ambayo yanatakiwa kuwepo ili kuhakikisha kuwa kuna aina ya uthabiti kwa kile wanachama wa Agora wanachopitia duniani kote. Hivyo vinavyoelezewa kwa kina kwenye ukurasa wa
Vigezo ya Uendeshaji.
Kumbuka pia hauzuiwi na shughuli ambazo zipo kwenye mpango rasmi. Kiuhalisia, tunakuhimiza kutafiti, kuunda, na kujaribu majukumu na shughuli mpya, ili mradi zinaweza kutumika kwa lengo la kielimu na zinaendana kiujumla na dhamira na malengo ya Agora Speakers International. Unaweza kusoma zaidi kuhusu ufafanuzi wa majukumu maalum hapa.
Anza kwa kuangalia kwa ujumla shughuli zipi kubwa, zinazotumia muda mwingi unataka kuwa nazo ndani ya mwaka (zile ambazo hazichukui zaidi ya dakika 20 kufanya na kuchukua muda mwingi wa mkutano wote). Kwa mfano:
- Midahalo mitano (5)
- Hotuba za papohapo kumi (10)
- Makongamano kumi (10)
- Warsha tano (5)
Zisambaze shughuli hizo kati ya mikutano ya mwaka, alafu jaza muda uliobaki wa mikutano kwa shughuli ndogo.
Mpango wako wa mwaka unatakiwa uwe unaweza kunyumbulika kidogo ili kuweza kuruhusu hali zisizopangwa au matukio yasiyopangwa ambayo yanaweza kuzuia klabu kukutana - haiwezekani kabisa kutabiri, miezi mitano (5) kabla, kuwa katika mkutano wa 21, utakuwa na hotuba nne (4) zilizoandaliwa na washiriki wanne (4) kwenye majadiliano.
Hivi ndio jinsi mpango wako unavyotakiwa kuonekana:
Japokuwa ni vizuri kuunda mpango wa mwaka, daima unatakiwa kuwasikiliza wanachama wako pia: Labda ulipanga Majadiliano kumi (10) na Makongamano (10) kwa mwaka, lakini baada ya robo ya kwanza ya mwaka unaona kuwa wanachama wanapenda Makongamano zaidi, kwahiyo itakuwa ni wazo zuri kubadilisha.
Kama klabu yenu ina uwepo kwenye mtandao, itakuwa rahisi zaidi kuweka mpango wa elimu kwenye mtandao, pamoja na viunganishi vya maelezo ya "wiki" ya shughuli hizo za kielimu.
Kufafanua Ajenda za Mkutano
Kama VPE, una jukumu pia la kuandaa ajenda ya mkutano kwa kila mkutano. Hii inamaanisha - kuamua ni vipengele vipi vya mkutano unatakiwa kuwa navyo, jinsi vitakavyoandaliwa ndani ya mkutano, na idadi yake. Kwa mfano:
Majukumu Yaliyopo |
---|
Hotuba Iliyoandaliwa #1 |
Mtathmini wa Hotuba Iliyoandaliwa #1 |
Hotuba Iliyoandaliwa #2 |
Mtathmini wa Hotuba Iliyoandaliwa #2 |
Hotuba Iliyoandaliwa #3 |
Mtathmini wa Hotuba Iliyoandaliwa #3 |
Mkuu wa Hotuba za Papohapo |
Mtathmini wa Hotuba za Papohapo |
Mzungumzaji #1 wa Leo Tunasafiri Kwenda |
Mzungumzaji #2 wa Leo Tunasafiri Kwenda |
Mtunza Muda |
Mwanasarufi |
Mtathmini wa Lugha ya Mwili |
Mtathmini wa Umakinifu |
Mtathmini wa Usikilizaji |
Mtathmini wa Mkutano |
Sio jukumu lako kama VPE kujaza ajenda (kutafuta watu ambao watajitolea kufanya majukumu haya) - hiyo ni kazi ya Kiongozi wa Mkutano wa mkutano huo. Bila shaka, unaweza kumsaidia kama unataka, lakini hili linatakiwa kuwa jukumu lao la msingi, kwasababu kuandaa mkutano maalum ni sehemu ya kujifunza kuwa Kiongozi wa Mkutano.
Hii inamaanisha, unatakiwa kuhakikisha kuwa Kiongozi wa Mkutano daima anachaguliwa mapema zaidi (kiuhalisia, mwishoni mwa kila mkutano uliopita) ili waweze kutangaza ajenda, kupokea maombi ya watu ambao wanataka kushiriki, na kupata muda wa kutafuta watu wa kujitolea kwa ajili ya majukumu mengine.
Kama viongozi wa mkutano wanapata matatizo mara kwa mara ya kujaza nafasi hizi za usaidizi - kwa kawaida Mtunza Muda, Mwanasarufi, Mwezeshaji, nk. - unaweza kuongea na maofisa wengine ili kutambulisha vigezo vya kushiriki kwenye majukumu maarufu zaidi. Kwa mfano, "Kutoa hotuba iliyoandaliwa inahitaji uwe umekuwa na jukumu la usaidizi tangu hotuba yako ya mwisho uliyoandaa".
Kuhimiza Wanachama Wapya
VPE ana jukumu pia la - pamoja na Makamu wa Rais wa Uanachama - kuwafanya wanachama wapya wajisikie wako huru na kuwahimiza kuanza kushiriki haraka iwezekanavyo.
Lakini, fahamu kuwa, kila mtu anaendelea kwa mwendo wake mwenyewe. Unaweza ukasukuma, lakini hautakiwi kumlazimisha mtu yoyote kwenye jukumu ambalo hawalitaki.
Baadhi ya vitu ambavyo unaweza kufanya ni:
- Wafikie wanachama wenye aibu na uwatambulishe kwa wanachama wengine ambao wamepitia njia sawa.
- Waonyeshe (sambaza) video za "kabla" na "baada" za wanachama wazoefu ili wanachama wapya waweze kuona mabadiliko.
- Kutegemea na hali yao, pendekeza wachukue majukumu rahisi kama vile Mtunza Muda au Mwanasarufi.
Kusimamia Maendeleo ya Kielimu ya Wanachama
Japokuwa mikutano ina sehemu kubwa ya kijamii, kama VPE, daima unatakiwa kukumbuka kuwa Agora ni Shirika la Kielimu na Mpango wetu wa Kielimu ni kiini. Mara nyingi wanachama wanakuwa wanakwama kwenye majukumu ya usaidizi au utathmini kwa sababu tofauti, kama vile:
- Hawana muda wa kutosha wa kuwekeza kwenye kuandaa hotuba na wanapendelea majukumu ambayo hayahusishi kufanyiwa kazi baada ya mkutano (Hotuba za Papohapo, Majadiliano, nk.)
- Wanaogopa kuthathmini.
- Hawana maarifa ya jinsi ya kutumia teknolojia au vipengele vinavyohitajika kwa ajili ya mradi (kwa mfano, mradi wa "Kutumia Programu ya Uwasilishaji")
- Hawana mawazo tena ya mada za hotuba.
- Hawana uhakika wa nini kinafuata kwenye maendeleo yao ya kielimu au wana mashaka nayo.
Ukiona mtu amesimama kwenye maendeleo yake, jaribu kumtafuta na ujue ni nini kinaendelea. Kwa utaratibu wahimize kuendelea, waonyeshe nyaraka za mawazo ya mada za hotuba, jinsi ya kusimamia wasi wasi mwingi, kuandaa warsha za jinsi ya kutumia teknolojia, panga muda kwa wanachama kuweza kujifunza na zana, nk. Haya majukumu sio ya kwako tu: pale utapofahamu tatizo, watafute maofisa wengine wakusaidie au kupata mapendekezo.
Japokuwa unaweza kuwatania au kuwahimiza watu, kwa mzaha kama "angalia, Martha yupo miradi miwili mbele yako", usigeuze maendeleo ya kielimu kuwa mashindano. Hamna haja ya kufanya haraka. Ni afadhali zaidi kama wanachama wakiendelea taratibu lakini kwa uhakika na maarifa yao yawe kutokana na waliyopitia.
Kuwahi kupata pointi/vyeti/chochote kile unachopata mwisho wa siku haitomaanisha chochote kwenye ulimwengu wa kitaaluma, ambapo kitu pekee cha muhimu ni maarifa halisi ambayo unaweza kuyafanyia kazi.
Kuhakikisha Maoni Bora
Sehemu muhimu ya Mfumo wa Kielimu wa Agora ni maoni kutoka rika walioitumia. Ili hii iweze kuwa fanisi, maoni yanatakiwa kuwa na vigezo vyote ambavyo vimetolewa kwenye Maoni Fanisi.
- Wahimize wanachama kusoma nyaraka kuhusu maoni
- Simamia maoni kwa ujumla ili yasije kuwa yasiyo na maana ("kila kitu kilikuwa barabara") au ya ukali sana ("haukufanya chochote cha maana") au hayahusu mada ("Sikubaliani na wewe kabisa").
- Fanya warsha zinazohusu Utathmini.
- Tafiti na sambaza (wape) video, vitabu, na makala za jinsi ya kutoa maoni fanisi na ya kujenga.
- Toa maoni ya faragha kwa watathmini
Kusimamia Mpango wa Ushauri
Klabu zote zinatakiwa kuwa na Mpango wa Ushauri ambao unakutanisha wanachama wapya na wale ambao wana ujuzi zaidi ambao wanaweza kuwasaidia na miradi ya kwanza, na pia kuwasaidia kuwaunganisha na klabu pamoja na tamaduni zake.
Kama klabu yako ndio kwanza imeanzishwa na wanachama wako wote ni wapya, na hamna mtu mmoja wa kuwa ni "mwanachama mwenye uzoefu zaidi", jisikie huru kufikia jamii pana ya Agora kupitia mitandao ya kijamii na kuwaomba wanachama wengine kuwa washauri wa wanachama wako waliojiwekeza zaidi, ili pale watakapokuwa na uzoefu zaidi, watakuwa washauri kwa wengine.
Mfumo wetu wa usimamizi wa mtandaoni utakapokuwa tayari, utaweza kufanya hivyo moja moja kutoka kwenye dashibodi ya VPE.
Kuandaa warsha
Warsha ni shughuli ambayo inathaminiwa sana na wanachama. Unaweza kuandaa warsha za ndani - ambapo mwanachama wa Agora anawasilisha hotuba ya kuhusu mada fulani, au unaweza kumualika mzungumzaji kutoka nje azungumze kwenye klabu. Unaweza ukatumia fedha za klabu kama hiyo itahitajika, na kama wazungumzaji hao watataka malipo.
Kulingana na wingi wa kuingia wa wanachama wapya, utataka kurudia baadhi ya warsha mara kwa mara:
- Taratibu za Klabu
- Kupata zaidi kutoka Agora Speakers
- Utathmini Fanisi
- Kusimamia wasi wasi
- Kujibu Maswali ya Papohapo
- Kufanya kazi na Jukwaa la Mtandaoni
Neno la tahadhari
Agora Speakers inajivunia kuwa na msingi thabiti kwenye Sayansi, na kwa ukweli, ni sehemu ya sheria zetu. Kila pendekezo na shughuli ya kielimu ambayo tunaweka mbele ina tafiti imara, iliyojaribiwa na rika, yenye hadhi ambayo inaunga mkono ufanisi wake. Tunawafunza wanachama wetu kutumia mbinu ambazo zina zimethibitishwa kufanya kazi kwenye dunia ya kweli, kwa kuaminika na kwa kurudiwa.
Kwa bahati mbaya, mara nyingi haiwi hivi. Medani ya uzungumzaji mbele ya hadhira na uongozi zimejaa ushauri ambao hautathminiwa, wa kutiliwa mashaka, na mara nyingine wa uongo kabisa. Kuna sekta kabisa ambayo inatengeneza vitabu unavyovihitaji na mwandishi anatumia maudhui yale yale na kufungasha tofauti aina hii ya maudhui kwa ujumla na ushauri usiokuwa na maana.
Mara nyingi unasikia, kwa mfano, kuwa unatakiwa kujitahidi usiwe na maneno yanayojaza sentensi wakati tafiti zinasema kitu kingine tofauti kabisa - kutokuwa na maneno yanayojaza sentensi kabisa inaharibu uaminifu wako kabisa. Unaweza pia kusikia mara kwa mara kuhusu mpangilio wa Mfuatano wa Kuhamasisha wa Monroe ni muundo kamilifu wa hotuba za kushawishi, na ushauri huu umerudiwa kutoka kitabu mpaka kitabu, kutoka kozi mpaka kozi, kutoka hotuba mpaka hotuba. Kiuhalisia, tafiti pia zinaonyesha kuwa hamna kitu maalum kuhusu mfuatano wa Monroe - haina ushawishi wa zaidi au pungufu kuliko mpangilio mwingie wa kuandaa hotuba ili mradi una maudhui ya lazima.
Wakati wanachama wengine wana uhuru wa kuwasilisha hotuba zilizoandaliwa kuhusu mada yoyote ambayo wanaitaka, bila kujali ni ya ajabu vipi (ili mradi ni maudhui ya hotuba yanayokubalikwa), warsha ni shughuli zisizo lingana ambapo mtu moja anainuliwa kwenye kipengele cha mtu ambaye ana maarifa ambayo yanadhaniwa kuwa ya kweli na wengine.
Warsha ambazo zina mawazo ya sayansi yasiyo ya kweli au ya uongo kuhusu maeneo ambayo tunayafunza haziruhusiwi.
Tunapendekeza kutumia TEDx Mwongozo za Maudhui (haswa kwenye kipengele cha "Sayansi Mbaya") kwa ajili ya kuhakiki wazungumzaji wa nje na maudhui ya warsha zao. Tunapendekeza pia hii barua kwa jamii kutoka TEDx kuhusu kugundua sayansi mbaya.
Jibu maswali ya wanachama yanayohusiana na Mpango wa Kielimu.
VPE ni mtu wa kumfuata kuhusu maswali yanayohusiana na Mpango wa Kielimu.
Viongozi wote wazuri wanaelewa kuwa "kuongoza ni kuhudumia", kwahiyo jaribu kupatikana na kuwahimiza watu kuuliza maswali yoyote ambayo wanayo. Hii aimaanishi kuwa unatakiwa kujibu kila swali ambalo watakuwa nalo. Ni sawa kukubali kuwa haujui lakini utaangalia na kuwarudia. Kama una maswali yoyote kuhusu Agora ambayo huna majibu yake, jisikie huru kututumia ujumbe.